Tatizo la viongozi wa nchi hii ni wasahaulifu sana! Wakishapata uongozi na kuhamia dar, wanasahau walipotoka na kuona dunia nzima ipo kama Upanga!
Nimebahatika kufanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa ya shule za kata yalizojengwa chini ya miradi ya Tasaf mwaka 2010 katika vijiji vyote vya wilaya ya Mpwapwa, Kongwa, Mbulu na Karatu. Shule nyingi zilizoanzishwa chini ya ujenzi wa shule za kata hazina vyoo, maji, ofisi za waalimu, maktaba, maabara na hata madarasa hayatoshi! Umeme ni hadithi ya kusadikika na si wa leo wala kesho. Waalimu ni mmoja au wawili na wanasaidiwa oa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo! Ndio maana nashangaa kauli kama hizi!
Nadhani ni wakati wa wananchi kuchagua viongozi wanaoishi jimboni kwao. Maana nadhani haya ni madhara ya kuchagua mtu anayeishi masaki, kasoma Olimpio, kisha Feza!. Chuo kasoma Tumain Dar, kazi kapata TRA. Miaka miwili - mitatu anaenda kugombea ubunge Katavi na tunamchagua kwakuwa tu baba yake alizaliwa huko na kuishi kipindi fkani. Huyu hawezi kujua shida na mazingira tunayoishi. Ndio wanaotudanganya watatuletea computer kwenye shule zetu akidhani zipo kama alizosoma yeye kumbe hata wiring hazina! Sio tu wanajidhalilisha bali wanatudhalilisha na sisi!
Tusirudie makosa haya uchaguzi ujao. Mwerevu ni yule anayejifunza kwa makosa na kuhakikisha kutokuyarudia. Tufanye uchaguzi sahihi mwaka '15!