Eti kuanzia 2015 Wanafunzi wa sekondari..

Eti kuanzia 2015 Wanafunzi wa sekondari..

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2009
Posts
5,101
Reaction score
1,952
...wa kidato cha nne watatakiwa kufanya mtihani wa computer! Nimesikia sasa hivi (saa mbili usiku) taarifa ya habari Radio One.

My take:
Ukitilia maanani ni chini ya 10% ya Watanzania wenye access ya umeme, ni shule ngapi kati ya zilizopo ambazo wanafunzi wake watafundishwa?
Ni waalimu wangapi wa sekondari wana uwezo wa kutumia computer achilia mbali kuweza kufundisha? Lini mitaala imetayarishwa, computer zimenunuliwa lini?

Serikali hii haishi kunishangaza, unapodhani wamefikia kiwango cha chini kabisa (even by their own pathetic standard ) cha kukosea wanaweka standard ya chini zaidi ya mtu wa kawaida anavyoweza kufikiri!
 
Eehhe sema kwa upande mwingine itaongoza ajira kwa vijana weng wa IT
 
Kama nakumbuka sawasawa mukulu alishawahi kutoa ahadi ya kila mwanafunzi wa shule ya msingi kupata access to computer! Nadhani hata wanaokaa chini watapewa iPad zinazotumia mwanga wa jua manake ni convenient kutumia kuliko desktop na laptop!
Viva la JK!! Tumethubutu, tumewezwa, tunazidi kuyoyoma!
 
Hivi kumbe Tanzania ni nchi, daah sikujua hilo kabla.
 
duu kweli mipango sio matumizi ngoja tuone..

Ndetichia, huu haustahili hata kuitwa "mpango". Nimeshafundisha sekondari (tena Dar es Salaam) kwa hiyo nawafahamu waalimu wengi mno wa sekondari. With due respect to them, wanaoweza kushika mouse ya computer hawafiki 10%, so kama hali ndiyo hiyo kwa Dar es Salaam, what about kwa Sumbawanga, Singida, Tabora, Kahama, Igunga n.k?

Sijawahi kuona wazo la hovyo kiasi hiki! Wanashindwa kutoa wanafunzi wanaomaliza shule za msingi wakijua kusoma na kuandika leo wanafikiria wataweza kufundisha computer ili form four wafanyie mtihani tena within next three years (which means form one wa mwaka huu waanze kufundishwa)? Hii serikali inatuabisha Watanzania tuonekane woote kabisa hamnazo!
 
Hapo serikali imekurupuka ingawaje mtaala upo na vtabu vipo ila resources kama umeme, computer na walimu, ingawaje tangu 2007 vyuo vya ualimu vinafundisha computer, lakn kutokana na ukweli kwamba wanafunz wengi wa kibongo tunasomea mtihani (tunakariri) ndio maana tatizo bado lipo.
 
Tatizo la viongozi wa nchi hii ni wasahaulifu sana! Wakishapata uongozi na kuhamia dar, wanasahau walipotoka na kuona dunia nzima ipo kama Upanga!

Nimebahatika kufanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa ya shule za kata yalizojengwa chini ya miradi ya Tasaf mwaka 2010 katika vijiji vyote vya wilaya ya Mpwapwa, Kongwa, Mbulu na Karatu. Shule nyingi zilizoanzishwa chini ya ujenzi wa shule za kata hazina vyoo, maji, ofisi za waalimu, maktaba, maabara na hata madarasa hayatoshi! Umeme ni hadithi ya kusadikika na si wa leo wala kesho. Waalimu ni mmoja au wawili na wanasaidiwa oa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo! Ndio maana nashangaa kauli kama hizi!

Nadhani ni wakati wa wananchi kuchagua viongozi wanaoishi jimboni kwao. Maana nadhani haya ni madhara ya kuchagua mtu anayeishi masaki, kasoma Olimpio, kisha Feza!. Chuo kasoma Tumain Dar, kazi kapata TRA. Miaka miwili - mitatu anaenda kugombea ubunge Katavi na tunamchagua kwakuwa tu baba yake alizaliwa huko na kuishi kipindi fkani. Huyu hawezi kujua shida na mazingira tunayoishi. Ndio wanaotudanganya watatuletea computer kwenye shule zetu akidhani zipo kama alizosoma yeye kumbe hata wiring hazina! Sio tu wanajidhalilisha bali wanatudhalilisha na sisi!

Tusirudie makosa haya uchaguzi ujao. Mwerevu ni yule anayejifunza kwa makosa na kuhakikisha kutokuyarudia. Tufanye uchaguzi sahihi mwaka '15!
 
hii nchi ina vituko sana, huko udsm kwa mfano computer lab udbs kuna computer nzima kama 20 tu pale CASS hazizidi 5. sasa huko vijijini achilia mbali umeme hizo computer zinapatikana? Nakumbuka wakati nasoma undergraduate pale mlimani, wakati Maghembe akiwa waziri wa elimu alisema wanafunzi wa vyuo wanapenda anasa, pesa ya meal allowance wananunua tv na computer. Swali langu ni je hawa viongozi wetu wanaona kama mwanachuo kuwa na computer ni anasa watasema nini kwa wanafunzi wa sekondari kutumia hizo computer? au watafundisha tu theory? Au ndo mambo ya CPU, click itatokea blue. Ama hakika wanaofikiria masaburi ni wengi sana nchi hii
 
Eehhe sema kwa upande mwingine itaongoza ajira kwa vijana weng wa IT
Itapunguza ajira kwa vijana wa IT kwasababu wengi waliosoma watakuwa computer literate hivyo baadhi ya kazi za IT zitakuwa zinaweza kufanywa na wafanyakazi wote kutokana na ujuzi wao wa computer. Huko tunapoelekea, computer itakuwa sio option tena bali ni lazima uwe na ujuzi,,,,,
 
Wasiwasi wangu hili litakelezekaji katika sekondari za kata
 
Back
Top Bottom