Eti Kwanini Mapadre Hawaoi

Eti Kwanini Mapadre Hawaoi

Hodar

Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
16
Reaction score
8
Wanaopinga swala la mapdre kuacha kuoa nawashangaa sana je wamewahi kusoma haya maandiko yanayoelezea msimamo wa Yesu na Paulo katika vitabu hivi;

Maneno ya Paulo Mtume:
1Wakorintho 7:1.8
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo"

Maneno ya Yesu mwenyewe:
Mathayo 19:10-12,
"Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutoa kabisa.Lakini Yeye akawaambia 'si wote wawezao kulipokea neno hilo, ila tu wale waliojaliwa, maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako MATOWASHI waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako MATOWASHI WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI. Mapadre wameamua kujifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
 
hawaowi ila wanawatoto wa kutosha tu,,
ina maana wanazini sana,,
 
Back
Top Bottom