Eti Magufuli alipigana vita na mabeberu, vita ya uchumi, ni vita gani alishinda dhidi ya Western Impelialism?

Upewe ulinzi
 
Magufuli alikuwa ana matatizo ya human rights kwa watu wake, hasa wale ambao walimbishia, hili lilikuwa ni kosa, ingawa nchi kama UAE, Saudi, China, Singapore vilevile huwezi kumbishia kiongozi ukaachwa, lazima ufe.

Ila tu namsifu kwa kitu kimoja, ile kuipenda nchi yake na kulinda heshima ya nchi, discipline, kutokopa madeni China, au world bank na IMF packages, huyu ndiyo Rais, hatokei mwingine. Hawa wengine wote hata itatokeaje hamna kitu. JPM alikuwa Rais, na hatokei mwingine, it happens in a lifetime.

Huyu wa sasa atawagalagaza hati mtasikia Habari yake; na ngojeeni kidogo tu; doom hiyoooooo!
 
Ivi Kuna raisi ukimwacha nyelele mwenye legacy kama late Jpm,mtu mwenye legacy Aachi kuzungumziwa
we unajua hata maana ya legacy? Kuna legacy ndani ya miaka 5? Mtu hakuweza kukamilisha hata mradi wa maana leo legacy. Km hamuelewi mambo bora mkae kimya
 
Afya ya akili ya Sukuma gang imekaa mbaya sana
 
kutokopa madeni China, au world bank na IMF packages,
Alikuwa anakopa wapi? Nobody knows maana alikuwa anaficha kila kitu.

Ongezeko la deni la taifa lazusha mjadala Tanzania​

Admin.WagnerD
09.11.20219 Novemba 2021
Wakati serikali ya Tanzania ikianisha jinsi itavyotumia mkopo wa zaidi ya shilingi trilioni 1.3, kutoka Shirika la fedha duniani IMF, kumezuka hoja mpya kuhusu deni la taifa linalodaiwa kuendelea kuongezeka.
 
MODS REKEBISHA SPELLING MISTAKE. LET IT READ IMPERIALISM
 
Wengi wenu mnaemtetea yule jamaa Hamna Data mnaongelea Emotion. Kwa Nchi hii linapokuja Suala la Maendeleo kuna Maraisi wawili tu Mkapa Na Kikwete hawa jamaa atleast Wameleta maendeleo yanayoonekana kwa Macho na Data

Hizi ni data za Pato la mtu mmoja mmoja kuanzia miaka ya 80 hadi leo,

YearGDP Per Capita (US $)Annual Growth Rate (%)
2021$1,0995.49%
2020$1,042-0.94%
2019$1,0524.06%
2018$1,0113.56%
2017$9763.58%
2016$9421.47%
2015$929-8.29%
2014$1,0136.02%
2013$95511.78%
2012$85511.13%
2011$7695.22%
2010$7317.28%
2009$6811.44%
2008$67224.57%
2007$53913.89%
2006$473-1.44%
2005$4807.32%
2004$4486.61%
2003$4204.83%
2002$4001.44%
2001$395-1.18%
2000$3992.29%
1999$3900.90%
1998$38755.59%
1997$24915.89%
1996$21521.32%
1995$17712.84%
1994$1571.91%
1993$154-10.35%
1992$172-9.48%
1991$19013.43%
1990$167-6.16%
1989$178-15.64%
1988$211-15.64%

-Mkapa anaingia Madarakani 1995 pato la mtu mmoja mmoja ni $177 ambazo ni kama laki 4 za sasa na anatoka Madarakani pato ni $480 ambazo ni kama 1, 100,000 za sasa. jamaa kaongeza Uchumi karibia mara 3 ya alivyoukuta,

-Kikwete naye Kaingia Madarakani 2005 kaanzia hapo $480 ilioachwa na Mkapa na Mpaka 2014 mwaka wake wa Mwisho Tukaingia Uchumi wa kati na kufika $1013 na wakati anatoka 2015 mwaka alioshea na Magu Uchumi ukashuka hadi $929, kiujumla Kikwete nae Aliongeza Uchumi wetu kwa asilimia 100.

-Kaja Magu sasa Mnaemsifia, Uchumi wa 2014 wa kikwete mpaka Magu Anafariki umeongezeka toka $1013 mpaka $1042 tu, miaka 6 kama Taifa tulisimama, ingekuwa kwa speed ya Mkapa ama Kikwete sasa hivi Tungekua range ya $1500-2000.
 
Leta evidence hap, maana kila mtu huwa anasema kuhusu haya, ukitaka evidence hakuna, pekua kote halafu leta, maana evidence ndiyo inakata Shauri.

Mimi siyo fun wa JPM, lakini comparatively; sijaona nchi yenye kiongozi nyolo nyolo kama JK au Samia inaendelea; lazima uwe na kiongozi shupavu, Magu alikuwa shupavu, all those countries which developed viongozi wao walikuwa shupavu, hasa kwenye utekelezaji na kufuata utaratibu, na kupenda nch yako. charismatic leaders
 
2015 inareflect kwa JPM? JPM itaanza reflection 2017, 2018, growth ipo, 2019 growth, Pamoja 2021 despite COVID; unataka kusema nini?
 
Upuuzi, wakati wa Mwinyi nchi ilifilisika, yaani 1992, kila kitu kilikuwa stagnant Mkapa akainua, growth gap ilikkuwa kubwa na gains zikawa kubwa wakati wa mkapa na JK, kufikia kwa JPM lile gap lilizibwa na growth ikawa normal. Usilete upuuzi hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…