Eti nawaza Nchi hii ili ule mema yake unatakiwa kutosema uovu hasa linapogusa walao keki

Eti nawaza Nchi hii ili ule mema yake unatakiwa kutosema uovu hasa linapogusa walao keki

Milazetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2025
Posts
300
Reaction score
270
Wadau wenye kunishauri na ujinga wangu mnishauri na kunielimisha ila mwenyewe nimekwama.

Eti nawaza Nchi hii ili ule mema yake unatakiwa kutosema hili ovu hasa linapogusa walao keki ili usiharibu utulivu wao wakati wa kula,Ili uwe salama na ujenge urafiki nao hutakiwi kusema hili liende vile hasa ukiwa maskini kama mimi,

Wajinga kama mimi ndiyo tunaotakiwa sana hata unaweza kukaribishwa kwenye sahani ya wenye mamlaka wakakupa keki nawe uonje. Ukimaliza elimu ya juu au ya kati ama hujasoma kama sisi we jiingize kwenye kubeti na boda usiwaze yaliyo juu ya meza ukiwa hivi utapendwa yani wajinga kama mimi ndiyo tunapendwa na usalama tunao,

Ujinga wangu unauoga ndani yake mana eti naambiwa ukiwa mwelevu kwenye mambo muhimu ya taifa hutokuwa na amani sana kwahiyo wajinga kama mimi tunatulia na wenye meza nzuri wakituona tunahangaika na yasiyo muhimu kwa taifa ndiyo wanajuwa amani yetu ipo hapo.
 
Back
Top Bottom