Eti Train ya Umeme kununuliwa engine za Diesel ⛽

Eti Train ya Umeme kununuliwa engine za Diesel ⛽

Nchi hii haina Serikali wala watumishi wa Serikali, kuna kundi kubwa la wezi na mafisadi kuanzia juu mpaka chini ya ngazi ya utawala.!

Hivi unaanzaje kama kiongozi kuropoka kuwa utaagiza injini za hybrid kwenye reli ya umeme ambayo tayari manunuzi ya injini za umeme yameishafanyika?

Hii habari ya hybrid kwa nini haikuamuliwa hata kabla ya kuanza ujenzi? ... Mbona tuliaminishwa kuwa bwawa la umeme la Nyerere litatoa line kwa ajili ya SGR_TZ na linazalisha umeme tayari? Kwa nini sasa mnakuja na madai ya umeme wa jua?? 😲

Hivi hizo injini za backup tena hybrid zitasukuma au kuvuta zile EMU zilizopo au mnafanya manunuzi ya kutaka sifa?

Tumeonyeshwa mabehewa ya ghorofa ambayo nikiyaangalia kwa macho naona kama ni marefu kuweza kupita kwenye mahandaki ya Kilosa, nitakapoona yamepita nitaamini kuwa kweli kuna wasomi pale TRC vinginevyo, kwa mtindo huu wa utawala... Siamini mwanasiasa yeyote nchi hii.

Nikihitimisha, nasikitishwa na jinsi nchi inavyoendeshwa kihuni huku pesa za walipakodi zikitapanywa kwenye anasa na matanuzi. Mbaya zaidi hakuna anayejali, mfano mamlaka za leseni hazina haraka ya kukusanya maduhuri kwa kuhuisha leseni zilizoisha muda wake, Lengo ni hiyo pesa isifike Serikalini bali iingie mikononi mwa watumishi wa umma wabadhirifu.....
Nchi hii inahitaji kuwa na Dictator atakayeweza kutawala kwa mkono wa chuma kwa miaka kumi hadi tupate watawala waadirifu. 😢 😭
 
Tunaposema Tanzania inahitaji viongozi wenye maono,malengo na uzalendo wa kweli tunamaanisha. Ni juzi tu train ya umeme imeanza kazi huku Stigler gorge ikiwa imeanza kuchangia kiasi cha megawatt kwenye gridi ya taifa ila cha kushangaza na kitia huzuni ni kwamba badala ya kuwa na mkakati mahususi wa kuhakikisha umeme haukatiki kwa namna yoyote Ile hata kwa ku dedicate megawatt kadhaa just for train peke yake, viongozi wanakuja na mkakati wa kinunua engine za Diesel eti kwajili ya kuendesha SGR pale umeme unapokatika.

Hakuna mpango wowote unaowekwa mezani kuhakikisha umeme haukatiki, mabilion ya pesa yamewekezwa kwenye umeme pamoja na train ya kisasa ila naona viongozi wameamua ku sabotage na kurudisha Tanzania kwenye giza.

Viongozi wetu unapowaona wanapita na magari ya kifahari na suti nzuri za kuvutia unawezawaona kama ni watu wa maana sana ila kiukweli ni tofauti na vile tunavyowaona, wengi ni less creative, wapenda rushwa na madaraka, uwezo mdogo katika kifikiri na kutenda, na wengi hufikiria zaidi matumbo yao kuliko maendeleo halisi ya nchi ya Tanzania.

Mama Samia angalia sana watu unawapa nafasi za kubeba maono na ndoto za watanzania, wengi wa hawa viongozi wanatulazimisha kuwa umasikini, na ujinga kuwa sehemu ya maisha yetu.

Train ya SGR imetupa sifa kubwa kama watanzania duniani kote ila hili la kununua engine za diesel badala ya kuimarisha upatikanaji wa umeme unaenda kutunyong'onyeza, kutubagaza, kituaibisha na kutufanya tuonekane kituko kwenye Dunia hii ya sayansi na teknologia.

Naomba Rais Samia uchunguze kwa makini huyu aliyeleta wazo la kununua engine za Diesel Ili kujua nani ana ratibu mambo haya ya kihuni na aseme ni nchi gani duniani iliyonunua train za umeme alafu wakaagiza tena engine za diesel kwajili ya kuendesha train ya umeme.

Ila pia msichukie sana wananchi wanavyomsifu JPM kwa namna alivokuwa anapambana kwa nia ya dhati ya kuiletea Tanzania maendeleo ya kweli na heshima duniani. JPM asinge tolerate mambo kama haya.
View attachment 3175658
Tanzania tupo kama FUTUHI vile.

Hivi CCM wanatuonaje kwani? Uzuzu unazidi kuisha labda watupige limbwata lingine
 
Hizo ni injini za umeme na dizeli, mfumo mmoja ukifeli mwingine unaingia kati
Kwa nini hazikununuliwa hizo wakati wanatoa order ya injini? Kumbuka Kadogosa alilisemea sana hili jambo la umeme wa treni za SGR_TZ. Kwamba TRC ikikosa umeme wa kuendesha treni nchi nzima itakuwa gizani....Yalikuwa maigizo? 😲
 
Unaweza kushangaa CEO wa TRC amejiamulia bila kukaa meza moja na CEO wa TANESCO kuweka mikakati ya namna ya kuzuia umeme usikatike tena.
Nashindwa kuelewa ni wapi back-up ya umeme kwenye traction system imekuwa diesel engine?
Kama ni hivyo si umeme ukikatika train isimame tu mpaka itakaporudi kuliko kupoteza pesa za mafuta na kununua hizo engine.
Bwana Masanja Kadogosa nilikusikia siku ya Annual Engineers Day 2023 ukilalamika kuwa kuna wataalam wanaogopa kushauri na kuchukua maamuzi sahihi....kama utafanya huu ujinga utaingia kwenye list ya wajinga wengine. Tuambie taarifa ya TANESCO kuhusiana na matatizo ya umeme ya kuendesha SGR itadumu kwa muda gani?

Mbona line ya Ikulu umeme haukatiki? Inashidwa nini line ya SGR umeme usikatike?
 
Back
Top Bottom