Eti ualimu ni kimbilio la waliofeli?

Eti ualimu ni kimbilio la waliofeli?

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Kuna wimbo nikiusikiza najisikia vibaya pale anaposema ualimu na upolisi ni kimbilio la waliofeli,sa hivi hii kauli ni ya kweli.Roma Mkatoliki
 
Kuna wimbo nikiusikiza najisikia vibaya pale anaposema ualimu na upolisi ni kimbilio la waliofeli,sa hivi hii kauli ni ya kweli.Roma Mkatoliki

ndiooooooooo.............................
naunga mkono hoja. lkn hii ni kwa tz tu.
 
Kwa walimu ngazi ya cheti na diploma wengi huwa ni failures lakini ngazi ya shahada wengi wao huwa wamefaulu vizuri tu.
 
Mantiki Sio kwamba waliopo huko wote wamefeli ila kutokana na kutowajali hawa watu mtu binafsi anakwenda kule sio sababu anapenda hio kazi bali anakwenda kama hakuna option nyingine.

In short ni mipangilio mibaya katika jamii yetu kutokutoa incentives kubwa ili kila mtu akimbilie huko, lakini waalimu wa kweli ni wale wenye wito, pia kufeli form four sio kwamba pia atakuwa amefeli baada ya kutoka Chuoni (sababu hapo anafuliwa upya).
 
Tatizo sio kifeli ila wanaenda huko ili wapate kazi
 
kuna mwalimu nlikuwa namdharau sana naona amepata ajira PCCB na kuna washikaji walikua smart sana ila wameachwa kuna kitu nimejifunza kuhusu waalim
 
Ila hapa chuo kikuu watu wana one F6 na wanasoma ualimu
 
Irumba chuo gani

sitaki kukitaja ila kama upo chuo hicho hiz sehemu ni maarufu kwa kupata msosi:,makanyagio na pale kwa babu je ni kwel?.kama nimekosea utaniwia radhi Bumija.
 
Si Kweli, Kazi Hii Mimi Naipenda Na Nilifaulu Vizuri Tu
 
Watu wamefikra kama walimu ni wale watu ambao ni failures nawapa pole sana, maana watoto zao wote wanafundishwa na hao walimu na wao kama wazazi wanakubalije kulipa ada tena zaid ya milion 2? Walimu wa cheti, na stashahada ndio hao hao wanao jiunga na chuo kikuu na kupata degree, sema watu wanawadharau walimu ndio maana wanasema walimu ni failure ila sio kweli. Nyerer alikuwa mwl na sio failure mtu anae wafundisha wanafunzi mpaka wanakuwa engineers, dactari, famasia n.k wanaitwa "walimu", sasa mwalimu failure ni yupi?
 
Kila mtu ameanza shule akiwa hajui hesabu za kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya lakini baada ya kumaliza shule, tumeweza kufanya milinganyo kibao ya hisabati. (that is the positive change).

Huenda ukaona walifeli hao watu, lakini ushawahi kuchukua vyeti vyao vya chuo na kuangalia ufaulu wao?

Hawa watu huwa wanaufaulu mzuri sana zaidi ya unavyofahamu. (maana huko chuoni wanasoma masomo ya ualimu pamoja na masomo watakayo fundishia)

Kitu kingine ni kwamba, entrance qualifications za kujiunga na chuo chochote kile cha ualimu ziko juu sana kulinganisha na field nyingine.

Mfano kwa upande wa certificate, vyuo vingi vya ualimu wanachukua div. IV ya 30 kushuka chini lakini wizara ya afyawao wanachukua pointi zaidi ya hapo.


Nkizipata data halisi nitaziweka.
 
Kwa ngazi ya cheti ni kweli kwani sijawahi ona wala kusikia mtu mwenye division one au two form four kaenda kusomea ualimu ngazi ya cheti.
Ila kwa ngazi ya degree si kweli kwani wanaosomea ualimu wapo walofanya vizur kama vile division I-6.

Halafu Watu wanapaswa kuheshimu fani za wenzao kwani kila fani inaumuhimu wake ndio maana ikawepo.
 
Back
Top Bottom