Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Vijana na watu wazima walishirikiana katika mchezo wa kamari (kwesa nsimbi). Mchezo huu pia ulitegemea ruhusa ya mtemi, maana mara kwa mara yaliweza kutokea matata ya kuuana wao kwa wao.
Kwa kuwa fedha haikuwapo wakati huo walitumia majembe na kauri, pembe za tembo na watu, yaani watumwa. Kila mchezaji alijipatia simbi nne au vipande vinne vya vigae vya vyungu vilivyofanywa kuwa duara hasa; na huleta ada au dau lake atakalotoa. Na iwapo mtu fulani aliweza kufutwa au kufilisiwa kabisa, aliweza hata kumweka mke na watoto wake (kuvega); kwa bahati mbaya labda alifutwa tena; basi alichagua kuweka njia rehani, na iwapo hata njia atafutwa, ilimlazimu kupita porini tu mpaka hapo atakapopata ukombo wa kuweza kuikomboa njia.
Yaani, alipoiweka njia rehani, ndiyo kusema kuwa yeye hakuwa na ruhusa kufuata au kuipita njia yo yote katika kijiji chao. Lakini wengine baada ya muda fulani walikaidi masharti hayo wakaanza kuzitumia njia bila ukombo wo wote. Watu wa namna hii walishtakiwa mabarazani wakalazimishwa kulipa na deni likaongezeka zaidi.
Jambo hili la kamari lilileta mauaji kadha wa kadha kwa ajili ya uchungu wa mali au kupotelewa na mke na watoto. Wengi walipoona dhiki kama hizi, walijifunza uaskari ili waende kwingine kuteka nyara na kupata watumwa kuwa ukombo wa jamaa zao. Lakini wao ambao waliumua ugomvi tu, kwa kuzivunja sheria za mchezo huo, walishtakiwa barazani wakatozwa faini.