Eti wameniozesha dada wa mchumba wangu!

Eti wameniozesha dada wa mchumba wangu!

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
Wanajamii mpo? Wameniozesha Dada wa mchumba niliemchaguwa!

Baada ya kukaidi wazee na kuowa mwanamke ambaye walihisi hakutulia,nilimfumania na bwana mwengine hivyo tukaachana. Kwa kufuata ushauri wa wazee nilielekea kijijini kutafuta mchumba na nikamuona msichana mzuri tu na kuamuwa kumchumbia.
Si unajuwa uchumba wa vijijini tena sikuwahi kukutana kisasa na mchumba wangu bali mipango ya harusi iliendelea. Siku ya harusi pia ni ya kijijiji nayo ilikuwa usiku na kuchukua mke. Naam wanajamii mambo yalikuwa mazuri kwani nilifunguwa kitu na boksi yake mimi mwenyewe.
Kuamka asubuhi ndio mtando ule wa kiarusi uliponitoka na kubaini kuwa mke wangu sie yule niliemchumbia badala yake alikuwa ni dada yake.

Wenzangu bila shaka nilifanya uamuzi lakini sijui ingekufikeni nyie mgekuwa na uamuzi gani?
 
mkuu,we umepata ngekewa ya kufungua box mwenyewe unataka nini tena?songa mbele mkuu!
 
Mc Tilly Chizenga hata kama hampendi
Hata kama umefugua mwenyewe ila upendo haupo ndo uendelee tuu au ndio kusema yatajipa humo humo

Bwana Mwamba,wazee wajanja waliona kabisa Ngekewa kaingia chaka!

"tena Ngekewa nitoboe siri...mimi ni miongoni mwa wazee wa binti,yule uliyemchagua ni binti yetu tunamjua,kashachoropoa mimba 18 na nusu,na vipimo vyetu vya kijadi tumegundua anao anao!tumeona tukuepushe nae tumekupa dada yake..ni safi na makaratasi umefungua mwenyewe!anza kuanzia leo kujifunza kumpenda,sawa kijana"
 
La nyie wazee mzowea kudanganya! Mliona kuwa dada yake ameshakaa muda mrefu hajatokea mwengine na mila zenu zinasema kuwa akiolewa mdogo kabla ya mkubwa basi yule mkubwa hataolewa tena> Hata hivyo nakupongezeni kwa uwezo wenu wa kuvitunza vijambo (samahani mkwe) bikira!
 
mambo ya kijijini bana, usikute wameona aolewe mkubwa kwanza maana wengin wanaamini kwamba mdogo kuolewa kumwacha mkubwa ni kama nuksi hivi
 
Wanajamii mpo? Wameniozesha Dada wa mchumba niliemchaguwa!

Baada ya kukaidi wazee na kuowa mwanamke ambaye walihisi hakutulia,nilimfumania na bwana mwengine hivyo tukaachana. Kwa kufuata ushauri wa wazee nilielekea kijijini kutafuta mchumba na nikamuona msichana mzuri tu na kuamuwa kumchumbia.
Si unajuwa uchumba wa vijijini tena sikuwahi kukutana kisasa na mchumba wangu bali mipango ya harusi iliendelea. Siku

ya harusi pia ni ya kijijiji nayo ilikuwa usiku na kuchukua mke. Naam wanajamii mambo yalikuwa mazuri kwani nilifunguwa kitu na boksi yake mimi mwenyewe.
Kuamka asubuhi ndio mtando ule wa kiarusi uliponitoka na kubaini kuwa mke wangu sie yule niliemchumbia badala yake alikuwa ni dada yake.

Wenzangu bila shaka nilifanya uamuzi lakini sijui ingekufikeni nyie mgekuwa na uamuzi gani?

Weweeee! Umebadilisha story ya Yakobo na mjomba wake Laban kwenye Biblia ukajifanya ni yako. Plagiarism! Yeye Yakobo ndiye aliyeozwa Leah badala ya Rebecca kwa mtindo huu. Nakushauri na wewe "uwatumikie wakwe zako" miaka mingine 7 kama yeye ndipo wakuoze huyo mchumba uliyemtaka mwanzo. Then utakuwa na wake 2.
 
Hata hii kama ni stori basi ina ukweli ndani ya jamii yetu. Vipi hii inaweza kuhusiana na hiyo unayosema wewe siwezi juwa kwani nakiri kuwa sijawahipo kusoma Biblia na kusikia itakuwa kwako kwa mara ya kwanza. Mara nyingi post zangu zinakuwa ni exprience niliyoipitia au niliyoiona mwenyewe.
 
Back
Top Bottom