Eti wanawake wenye ndevu wana-akili sana!?

Eti wanawake wenye ndevu wana-akili sana!?

Ndevu hazina uhusiano na tabia au akili ya mtu, kama ana akili ana akili tuu lakini si kwasababu eti ana ndevu.
 
Nani kakudanganya ndevu za wamama zinachipusha akili? Nakusihi mchukulie huyo mpenzi wako kama wanawake wengine.
Ndevu, Sharubu, Sharafa, Zivuma havihusiki na hilo. S a w a s a w a ?
 
Lisemwalo lipo.., ila fanya utafiti wa kisayansi ndio unaoweza kukupatia jibu la uhakika. Mwanamke kuwa na ndevu kunachangiwa na kuwa na homoni za kiume kwa wingi. Najua wajua kuwa me/ke wote tuna homoni ila ipi inamzidi mwenzie ktk kutengenezwa ndiko kunakotufanya tuwe na tabia au pengine muonekano tulio nao. Je ushawahi kumuona mwanaume mwenye matiti?
 
atakuwa hajausikia ule wimbo wa kupata ni majaliwa, ng'ombe amenyimwa ndevu lakini mbuzi kapewa.


BT, umeacha kumkimbiza mwizi kimya kimya?
Staili yako ya uchaingiaji ilikuwa inanifurahisha, kimya kimya bila makelele


sikujua kuwa nilikuwa na swaga za kimya kimya loh!!!!
 
Si ndo hapo sasa!!! Mtu badala amfahamu vizuri mhusika mwenyewe jinsi alivyo....anakimbilia kwenye vigezo vya bahati nasibu!!


hawa ndo wanaoangalia ndevu, vidole sita, sijui wanatumia mashoto...... Halafu siku mbili wanalalamika wenza wao wamewatenda....... Wamesahau uzuri wa mwanamke ni tabia......
 
kweli bhana, hii ishu ipo kwetu kagera huko, kwamba ukioa mwanamke mweny vindevu (sio nyingi lakin) utakuwa tajiri. i mean vindev vinaleta utajiri. (sina uhakika sana)
 
Hawana akili ila wanapenda kutoa nyuma,chunguza utagundua
 
mi nimesikia wana bahati za pesa
but zamani
sikuhizi wengi wanaota ndevu sababu ya vipodozi...
 
hufa haraka kwa matendo yao ya kumchukiza Mungu na si ndevu za wake zao!
kufa haraka si matokeo ya kumchukiza Mungu bali ni matokeo ya kupendwa zaidi na Mungu. @ mtoa mada kama hiyo maneno ni kweli, basi wanawake wa mbeya watakuwa na soko sana!
 
Nimesikia hizi habari siku moja kwamba ukipata bahati ya kuoa mwanamke mwenye ndevu za asili (sio wale wanaoota ndevu kwa sababu ya kuchubua na madawa mengine) huwa wanaakili sana za kimaisha na jinsi ya kuishi na wengine. Niataka kukubaliana nalo hili sababu nimekutananao ni wapole na wanyenyekevu mno.
Je, ni kweli?

Inamaana ndevu na tabia ya mt vina uhusiano gani?
 
Mi nina ndevu hadi makwapani na bado akili zangu hazina akili.
 
Hiyo ni kweli kabisa. Wote ninaowafahamu wenye ndevu wapo makini sana katika kuzitunza ndoa zao na katika harakati za kujiletea kipato nyumbani. Hata handling ya mwanaume wapo juu sana. Nina jirani yangu ananyoa kabisa kidevu chake lakini namna ambavyo anaendesha mambo yake huwa namwona ni wa mfano kwa wote pale mtaani.
 
Back
Top Bottom