Shehullohi
JF-Expert Member
- Jul 21, 2020
- 3,753
- 3,685
Mwaka 2016 wakati Waziri wa Habari na Utamaduni wa wakati huo, Nape Nnauye akitoa sababu za kusitisha matangazo ya Bunge live, pamoja na gharama alisema watanzania wengi mchana wako maofisini na wengine wanajenga taifa hivyo wakaamua kutengeneza kupindi maalum usiku kuonesha 'Edited clips' za Bunge ili wapate fursa ya kuona.
Leo Bunge 'LIVE' limerejeshwa na kamati ya Bunge huku Waziri akiwa yuleyule na hoja za kusitishwa zikiwa bado hazijayeyuka. Tofauti sasa, mamlaka ya kulirudisha inatoka mhimili tofauti. Katiba yetu bhana.
JIONEE
Anaye mlipa mpiga zumari ndiye huchagua wimbo gani uimbwe. Huyu mheshimiwa ni mpiga zumari tu hana namna.