Eto'o: Okocha alikuwa ni bora zaidi ya Ronaldinho

Eto'o: Okocha alikuwa ni bora zaidi ya Ronaldinho

Kwangu mimi binafsi bila kusikiliza porojo za mabeberu au vyombo vya habari nasema gaucho kamuacha okocha mbali sana.uwezo wa okocha labda umlinganishe na zidane na kawapita kidogo sana pirlo au watu kama kina iniesta ila sio gaucho.Gaucho ndiye fundi wa soka aliyeondoka uwanjani na vionjo vyake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ronaldhinho wamemuanzishia mpaka kombe lake huko brazil
Okocha nchini kwake wamemfanyia nn kumuenzi
Ronaldinho alikua ni balaa nyingine wadada mpaka walikua wanajua ratiba za mechi za barcelona
 
Kuna jambo linaitwa management, msione watu wanatoboa toboa tu, kwa soka la okocha angefika zaidi ya pale, kuna vitu alikosa. Dinho mwenyewe kawahi kukiri okocha ni moto wa kuotea mbali, ila alifeli pale kukimbilia Uingereza kutimiza ndoto zake za kucheza epl.
Ukishakua na uwezo mkubwa management nzuri itajiset yenyewe.kwahiyo lazima uanze kwanza kua na uwezo kisha ndo management ifwate.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Lawama kwa wazungu. Waafrika wazee wa kujilizaliza. Playing victim

Africa kapewa tuzo gani? Maana kwa dunia wamemuonea.
 
Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Real Madrid, Chelsea, Everton na timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto'o Fils amesema kwake yeye Okocha alikuwa na uwezo zaidi ya Ronaldinho.

Tulichokiona kinafanywa na Ronaldinho kilishafanywa miaka 10 mpaka 15 iliyopita na Okocha. Hata walipokuwa wote PSG Okocha alikuwa akimuweka benchi Ronaldinho.

Ila kwakuwa Okocha anatokea Afrika, hawakuweza kumpa sifa zake hivyo nadiriki kusema Okocha alikuwa bora kuliko Ronaldinho. Aliongeza Eto'o

Mwanamichezo unakubaliana na Eto'o? Kwako wewe nani alikuwa yuko vizuri zaidi?

Okocha ni bora zaidi ya ronaldino.
 
Hivi wakuu tunamzungumzia Ronaldinho huyuhuyu alokipiga PSG, Barca kisha AC Milan au tunamzungumzia Ronaldinho yupi?

Etoo akumbuke Game walompiga Madrid 3-0 pale Santiago Bernabeu. Goli mbili alizoweka Gaucho, ikabidi mashabiki wa Madrid wampgie makofi Gaucho.

Kama tunazungumzia Talent yenye manufaa, tumuwekeni pembeni Gaucho.

Tukizungumzia overall kwa wachezaji wooote ulimwenguni, toka soka lianze, tumpe heshima yake mtu mmoja tu hapa duniani, ni LIONEL ANDRES MESSI.
 
Tukizungumzia overall kwa wachezaji wooote ulimwenguni, toka soka lianze, tumpe heshima yake mtu mmoja tu hapa duniani, ni LIONEL ANDRES MESSI.

Kwa huyu hakuna ubishi aise, sidhani kama atakuja kutokea kama Messi. Wakina Ronaldo wengi, gaucho wengi. Ila kwa Messi no comment
 
Dah sijui nan kamzid mwenzake lakin hao jamaa walikuwa wanacheza na ufundi wa kuuchezea mpira na unakubali wenyewe
 
Back
Top Bottom