EU kutaka kesi ya Freeman Mbowe ifutwe hawajui kuwa Tanzania is a free State?

EU kutaka kesi ya Freeman Mbowe ifutwe hawajui kuwa Tanzania is a free State?

Hivi haiwezekani wachangiaji mada wakachangia bila matusi na name calling?
Watu wastaarabu huwa wanalumbana kwa nguvu za hoja ma sio hoja za nguvu na matusi.
Ukijadli hoja kwa feelings na sio logic na commonsense basi mwisho inakuwa matusi na kudhalilishana.
Tanzania ni yetu wote.Tupo kwenye mtumbwi mmoja pale kwenye changamoto na makosa tuelezane na kukosoana kwa hekima.
Napata tabu kuchangia mada ambazo mwisho wake ni matusi.
Tusiwe kama wapenzi wajinga wa Simba na Yanga.
Nobody is perfect.No society is perfect.Hakuna Nchi ambayo ni Utopia kama kitabu cha mwandishi Sir Thomas More kilivyojaribu kueleza kuhusu society ambayo ni Utopia.
CHADOMO NDIO ASILI YAO MKUU
 
Hapo siyo CDM nadhani ni masharti ya misaada tunayochukua kwao!
Wajifunze kutokuwa tegemezi kwa kila kitu. Hali ya haki za binadamu na demokrasia Rwanda ni mbaya; hatusikii wakimkoromea Kagame.

CCM angalieni, msipokuwa makini 2025 utakuwa ndio mwisho wenu kutawala nchi hii.
 


Tanzania ni nchi huru tena Uhuru wake ni wa miaka sitini (60) sasa

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine za EU inayo sheria,kanuni na taratibu za kuongoza watu wake ili waishi na kujiletea maendeleo yao kwa amani na Utulivu

Freeman Mbowe na wenzake wanatuhumiwa kutenda kosa la Ugaidi na kesi inaendelea Mahakamani tena mfululizo hili dunia inajua

Utawala wa Sheria duniani kote ikiwemo EU unatamka kuwa "Hakuna aliyejuu ya Sheria " No one is above the law,

Je! Can't it be applied to Mr Freeman Aikaeli Mbowe?

CHADEMA mnataka kusema Freeman Mbowe kwa kuwa ni Mkt wa Chama chenu hawezi kutenda kosa?

CHADEMA na EU mnataka kusema Freeman Mbowe ni malaika wa nuru asiyeshawishika wala kutenda kosa?

Tunafahamu bifu kubwa lilokuwepo baina ya aliyekuwa Mbunge wa Hai Freeman Mbowe na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya

Miamba hii miwili ya kisiasa ilikuwa ikipimana nguvu pale Wilaya ya Hai kwa njia halali na zisizo halali,Hili wote tunalijua na CHADEMA mnalijua zaidi

Tukubaliane kuwa njia alizotumia Freeman Mbowe kutaka kumdhibiti Lengai Ole Sabaya ziliwafanya Mbowe na Sabaya kuvunja Sheria za nchi na wanaoweza ku-approve au ku-disapprove hili ni mahakama pekee kama chombo cha juu kabisa cha kutoa haki na wala sio Rais Samia

Kitendo Cha CHADEMA kuanza kuisiliba nchi yao kimataifa licha ya Juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan katika kuirejesha nchi kidiplomasia halikubaliki na halitakubalika kamwe

Tujiulize, CHADEMA wanaogopa nini kama kweli Freeman Mbowe hana hatia Mbele ya Sheria?

Sote tunafahamu, CHADEMA ndio Chama chenye Mawakili wengi na nguli wa Sheria hapa Tanzania

Je? wamekwama wapi au nawao wamebaini ni kweli mteja wao anamakosa wanaamua kuigeuzia kesi hii Kisiasa kisa Freeman Mbowe ni mwanasiasa?

Kwanini leo wakimbilie kulichafua Taifa Kimataifa hata kabla ya hukumu yenyewe? Nini kimewasibu kwenye jicho la Sheria?

CHADEMA acheni kulichafua Taifa letu Kimataifa,mlisingizia Magufuli Leo tena Samia lazima mtambue Sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya hii

Mnatuumiza sana sisi watu wa chini

Sisi hatuna uwezo wa kuishi huko Ughaibuni Ubelgiji,Canada wala Scotland kama ninyi na familia zenu

Mnanenepa na kung'aa kuwazidi hata Wazungu kwa gharama za nchi yenu hakika hii ni mbaya sana brothers

Hiyo misaada mnayotaka tunyimwe na EU ndio inawafanya watoto wa Shangazi zenu wajengewe madarasa elfu 15 na Rais Samia Suluhu

Plze Brothers & Sisters STOP IT

WAAMBIENI "EU" TUTASIMAMIA SHERIA ZETU KWA GHARAMA YEYOTE,TAIFA HILI NI KUBWA KULIKO MISAADA YA EU,.

Pia, soma=> Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe



View attachment 2030228

View attachment 2030229


Abarikiwe sana mzungu. Tena aongeze mbinyo zaidi. Kwenye hili la Mbowe mmeingia cha kike fully charged.

Kwenye hili la haki, usawa, uhuru na demokrasia tuko wengi mno tunaosimama na EU.

Mahakama ipi unayoiongelea wewe? Hii isiyotaka kuhakiki nyendo za kina Kingai, Jumanne, Mahita, Goodluck na Msemwa almaarufu kama wasiojulikana?

Mahakama inayosema Adamoo alikamatwa kwa mujibu wa sheria na akatoa maelezo yake kwa ridhaa yake pasipokuwa na shinikizo lolote?

Mahakama ipi unayoiongelea wewe? Hii iliyo na hukumu za kubambika kwenye kesi za kubambika?

Safi sana Tundu Lissu, Godbless Lema na wana harakati wote.

Na bado!

Barikiwa sana wazungu. Mnao utu kuliko ndugu zetu wa damu wanaoratibu na kutekeleza haya:

IMG_20211202_092804_863.jpg
 
Am telling you kwa Ujinga huu hamfiki mbali nyie jamaa,

Kweli Tanzania ya Samia hakuna demokeasia? Serious!!!!??

Kama demokrasia ipo si waruhusu hata mikutano ya ndani?

Kama demokrasia ipo waacheni wapinzani nao wawe na mikutano ya hadhara kama wafanyavyo ccm, uwoga wann?

intelijensia badala ya kudeal na uchumi, rasilimali za nchi, ushindani wa soko na viwanda kama wafanyavyo kenya tu jirani yetu, nyie kutwa kucha mnakimbizana na wapinzani.

wapinzani ni watanzania only wana hoja na mtazamo tofauti, ila ni tishio kwa wenye mamlaka na madaraka.
 
Tanzania ni donor country... wakati inatembeza bakuli na kunuka madeni...🚮🚮🚮🚮
 
Free state?!!free state inayo omba omba misaada hat ya kujenga vyoo!!
Hakuna Cha kesi pale,
Watawala wa ccm,wanaogopa mabadiriko yoyote yatakayo wapunguzia ulqji,wizi,na hata kuwatoa Madarakani,kila anaye hatarisha maslahi yao lazima apigwe rungu la kichwa anyamazishwe,Ili tabaka tawala,ndugu zao,marafiki,waendelee kula nchi watakavyo.
Na kwa sasa hv,Mbowe "is the thorn",in there flesh lazima wa mminye asipige kelele,

IMG_20211119_091739_123.jpg
 
Sikubaliani na hoja yako labda utoe mifano hai.

Kama kuna kiongozi mwanasiasa KATILI nchi hii ni Freeman Mbowe, kwa kauli na matendo yake, kiasi amewaambukiza viongozi wanasiasa wa CHADEMA. Hiki chama kikipata kuongoza nchi hii, hakuna shaka kutakuwa na utawala wa kidikteta.

Ushahidi ni tangu kimeanzishwa kimekuwa kwenye mlengo wa kujali maslahi ya wao viongozi. Dai lao kubwa la Katiba mpya nyuma yake ni Katiba ya kuwawezesha kupata madaraka ya Dola kwa ajili ya agenda zao binafsi.

Mwenye hoja tofauti na hii yangu, atoe japo jambo moja tu la Kitaifa, ambalo Viongozi wa CHADEMA wamefanya tangu kianzishwe ama kwenye Kata (madiwani), Majimbo (Wabunge) au Halmashauri walizoziongoza.

IMG_20211119_091739_123.jpg



IMG_20211130_082556_548.jpg
 
CCM wanapenda sana kuidharau hii Kamati ya Bunge la ulaya EU - mambo ya nje - haya nyie endeleeni tu hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom