EU kutaka kesi ya Freeman Mbowe ifutwe hawajui kuwa Tanzania is a free State?

EU kutaka kesi ya Freeman Mbowe ifutwe hawajui kuwa Tanzania is a free State?

Tanzania ni nchi huru tena Uhuru wake ni wa miaka sitini (60) sasa

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine za EU inayo sheria,kanuni na taratibu za kuongoza watu wake ili waishi na kujiletea maendeleo yao kwa amani na Utulivu

Freeman Mbowe na wenzake wanatuhumiwa kutenda kosa la Ugaidi na kesi inaendelea Mahakamani tena mfululizo hili dunia inajua

Utawala wa Sheria duniani kote ikiwemo EU unatamka kuwa "Hakuna aliyejuu ya Sheria " No one is above the law,

Je! Can't it be applied to Mr Freeman Aikaeli Mbowe?

CHADEMA mnataka kusema Freeman Mbowe kwa kuwa ni Mkt wa Chama chenu hawezi kutenda kosa?

CHADEMA na EU mnataka kusema Freeman Mbowe ni malaika wa nuru asiyeshawishika wala kutenda kosa?

Tunafahamu bifu kubwa lilokuwepo baina ya aliyekuwa Mbunge wa Hai Freeman Mbowe na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya

Miamba hii miwili ya kisiasa ilikuwa ikipimana nguvu pale Wilaya ya Hai kwa njia halali na zisizo halali,Hili wote tunalijua na CHADEMA mnalijua zaidi

Tukubaliane kuwa njia alizotumia Freeman Mbowe kutaka kumdhibiti Lengai Ole Sabaya ziliwafanya Mbowe na Sabaya kuvunja Sheria za nchi na wanaoweza ku-approve au ku-disapprove hili ni mahakama pekee kama chombo cha juu kabisa cha kutoa haki na wala sio Rais Samia

Kitendo Cha CHADEMA kuanza kuisiliba nchi yao kimataifa licha ya Juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wetu Mhe Samia Suluhu Hassan katika kuirejesha nchi kidiplomasia halikubaliki na halitakubalika kamwe

Tujiulize, CHADEMA wanaogopa nini kama kweli Freeman Mbowe hana hatia Mbele ya Sheria?

Sote tunafahamu, CHADEMA ndio Chama chenye Mawakili wengi na nguli wa Sheria hapa Tanzania

Je? wamekwama wapi au nawao wamebaini ni kweli mteja wao anamakosa wanaamua kuigeuzia kesi hii Kisiasa kisa Freeman Mbowe ni mwanasiasa?

Kwanini leo wakimbilie kulichafua Taifa Kimataifa hata kabla ya hukumu yenyewe? Nini kimewasibu kwenye jicho la Sheria?

CHADEMA acheni kulichafua Taifa letu Kimataifa,mlisingizia Magufuli Leo tena Samia lazima mtambue Sisi hatuna nchi nyingine zaidi ya hii

Mnatuumiza sana sisi watu wa chini

Sisi hatuna uwezo wa kuishi huko Ughaibuni Ubelgiji,Canada wala Scotland kama ninyi na familia zenu

Mnanenepa na kung'aa kuwazidi hata Wazungu kwa gharama za nchi yenu hakika hii ni mbaya sana brothers

Hiyo misaada mnayotaka tunyimwe na EU ndio inawafanya watoto wa Shangazi zenu wajengewe madarasa elfu 15 na Rais Samia Suluhu

Plze Brothers & Sisters STOP IT

WAAMBIENI "EU" TUTASIMAMIA SHERIA ZETU KWA GHARAMA YEYOTE,TAIFA HILI NI KUBWA KULIKO MISAADA YA EU,.

Pia, soma=> Bunge la Ulaya(EU) lajadili hali ya kisiasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

View attachment 2030228

View attachment 2030229

...Kwanza kabisa naomba usimfananishe Mbowe na taka za chooni aka Sabaya jambazi,hawa wawili ni anga na ardhi.

...Elewa hakuna uhuru usio na mipaka,Tanzania iko duniani na haina sayari yake ivyo lazima sisi kama nchi ni lazima tutii taratibu za dunia hasa haki za binadamu. Sisi sio kisiwa.

...Wazalendo wa kweli kama Tundu Lissu kutusemea uko nje sisi tunaoteswa na haya mashetani tuliyoyafuga wenyewe sio kuchafua taifa bali kuliponya,Nyerere aliitangazia dunia tulipokuwa tunanyanyaswa na wakoloni ndio maana tulipata uhuru.

...Uhuru wa kweli dhidi ya mkoloni mweusi utapatikana leo hii kwa kuielezea dunia uovu wa mkoloni mweusi,najua wanyampala wa mkoloni mweusi hampendi uhuru huu upatikane ila nakuhakikishieni soon tutaupata.
 
EU ni jumuia inayoundwa na watu, wenye uakilishi hapa nchini, tena wanajua hata shule zetu zinaupungufu wa vyoo wanajenga, unadhani wanaweza kushindwa kujua kinachoendelea kwa swala la mbowe na wenzake! Kama ni EU imeitaka serikali ,hapo Chadema wanaingiaje? Jumuia nyingi duniani ziliitaka serikali ya makaburu wakati huo imuachie Mandela, hawakutumwa n'a ANC hapana. Kama ni swala la kuonyesha dunia jinsi hali ya nchi yetu ilivyo kwenye upande wa haki ,uhuru na hata uvumilivu wa mawazo yanayopingana na serikali,hiyo siyo kazi ya Chadema tu ni kazi ya watanzania wote wapendao haki.
CHADOMO HAMIENI BASI NA NYINYI EU
 
Eti EU haijali demokrasia Africa! Demokrasia gabi iko Tanzania? Unajua maana ya demokrasia wewe?
 
...Kwanza kabisa naomba usimfananishe Mbowe na taka za chooni aka Sabaya jambazi,hawa wawili ni anga na ardhi.

...Elewa hakuna uhuru usio na mipaka,Tanzania iko duniani na haina sayari yake ivyo lazima sisi kama nchi ni lazima tutii taratibu za dunia hasa haki za binadamu. Sisi sio kisiwa.

...Wazalendo wa kweli kama Tundu Lissu kutusemea uko nje sisi tunaoteswa na haya mashetani tuliyoyafuga wenyewe sio kuchafua taifa bali kuliponya,Nyerere aliitangazia dunia tulipokuwa tunanyanyaswa na wakoloni ndio maana tulipata uhuru.

...Uhuru wa kweli dhidi ya mkoloni mweusi utapatikana leo hii kwa kuielezea dunia uovu wa mkoloni mweusi,najua wanyampala wa mkoloni mweusi hampendi uhuru huu upatikane ila nakuhakikishieni soon tutaupata.
Hebu tuambie maana ya Uzalendo
 
Tutasimamia sheria na taratibu tulizojiwekea kwa gharama zote.

Kama MWANACCM SABAYA YUKO JELA MBOWE NI NANI MBELE YA SHERIA?
Sabaya alikuwa jambazi na kila mmoja anajua hata huyo mtoto wako wa mwisho anafahamu

Na kila raia aliyepata sulubu amethibitisha.

Kwa mbowe ukitoa hawo mashahid wa kuchongwa ambao ushahidi wenyewe unatofautiana tutajie raia wanaomlalamikia kwamba mbowe ameumiza watu Kwa ugaidi wake.

Hebu oneni aibu ndugu.

Wewe ndiye mtekaji,ndiye mfungua kesi,ndiye shahidi, ndiye mpigaji kwasbaabu Mbowe anamtazamo tofauti na ccm sasa utaaminika vipi.
 
Acheni mahakama itoe uamuzi,
 
Hebu tuambie maana ya Uzalendo
Kwa kifupi sana uzalendo ni kuipenda nchi yako.

Huwezi kusema unaipenda nchi yako uku unafumbia macho maovu yanayofanywa na kikundi cha watu wachache kinachoua,kutesa na kuonea raia wake,kilichojaa rushwa,dhulam nk

Tetea nchi yako kwa kutetea maslahi ya wengi na hasa ya taifa na sio kutetea kikundi cha waovu na kupata ugali wa siku,Mandela na Nyerere wanakumbukwa na wengi kwa ajili hii sio wachache.
 
Sio tu nchi yako mkuu, Na Rais wako pale anapostahili
 
Hebu tuambie maana ya Uzalendo
Kwa kifupi Uzalendo ni kuipenda nchi yako...

Ivyo kama unaipenda nchi yako huwezi kukaa kimya dhidi ya rushwa,uonevu,uuaji na utesaji unaofanywa na kikundi cha wachache dhidi ya walio wengi. Lazima utawapigania kwa gharama kubwa.

Ndivyo walivyofanya Nyerere na Mandela na dunia inawaheshimu na kuwaenzi kwa hili.

Kutetea kundi la waovu wachache ili kukidhi haja za tumbo lako ni usaliti kwa nchi na ni kinyume kabisa na uzalendo.
 
Chadema ni jamii Frani ya nyoka yenye vichwa viwili ,hawangalii madhara yanayoweza kuwapata Watanzania hasa WA kipato cha chini, wao ni kubwatuka tu. Wanasheria Bora na wabobezi Wapo chadema Sasa wanaogopa nini, kesi IPO Mahakama pambaneni vidume
Akili za lumumba umaskini umekaa hadi kwenye bongo zao ona sasa huyu
 
Najaribu kuwaeleza wengi kuwa duniani imesonga mbele hatua moja. Siku hizi huwezi kujitetea kuwa nchi iko huru huku unavunja haki za binadamu. Tangu mauaji ya Rwanda dunia imejifunza kuwa kutojali uvunjaji wa haki za binadamu mwisho wake ni mauaji makubwa, machafuko, a failed state na wakimbizi kukimbilia nchi zenye demokrasia. Tangu hapo ikawa uhuru wa nchi haujalishi kama kiongozi anavunja misingi ya haki za binadamu, demokrasia. Soma Koffi Anan 'The right of intervention'.
Sasa hapa Tanzania nyie endeleeni na ushenzi tu badala ya kujifunza ustaarabu. Wengine tutakuwa wa mwanzo kuunga mkono uingiliaji kati. Kama hatuwezi kujitawala kwa ustaarabu acha tupate msaada wa waliostaarabika!
 
Back
Top Bottom