Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Asante mkuu,kwanza nilikuwa sijui unamaanisha nini nilipogoogle nikajua kumbe ni bendera ya LGBT
 
Aha kumbe lilileta matokeo makubwa tu? Yule refa cjui aliwaza nini kukataa lile goli.
Lilileta mapinduzi makubwa sana kwenye mpira. Refa alikuwa mbali na Lampard alipiga shuti la mbali maana hata Linesman nae alikuwa mbali sana.
Baada ya hapo waingereza kama unavyowajua waliongea zaidi ya mwezi kunyimwa goli hilo na FA ikatangaza tender ya kutengeneza goal line Technology ambayo mpaka sasa inafanya kazi.
 
Baada ya mkeka wa mwanzo kupitiwa na kisulisuli kilichoondoka na group la kifo.

Nimekuja na mkeka huu mpya.

Nafasi ya mshindi/bingwa itajazwa baadaye..
 
France walikua ni overrated sana, nilizungumza mapima ila watu ni wabishi sana.

Defence yao ya kati ni utopolo, nilikua na uhakika kabisa ndio itakayo kuja kuwatolesha.

Ngolo Kante ndie mchezaji kilaza Zaidi kwenye timu yao, hakustahiki kabisa kuwa ni stater uwanjani.

Mbappe dogo kiburi kimemzidi kuliko hata uwezo wake, Nilishauri mapema Awekwe bench Giroud achukue namba.

Ila kocha aliwaogopa sana Kante na Mbappe japo kuwa alikua akielewa kuwa ni vimeo, hofu ya media na mafans wasiojielewa aliiogopa. Mwisho kabisa amevuna alichokipanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…