Huku Ulaya hii ni wiki ya maadhimisho ya haki za mashoga, wasagaji, waliobadilisha jinsia na wengine wote kwenye hilo kundi.
Zoezi huwa linahitimishwa kwa maandamano makubwa ya kitaifa alafu moja ya kufa mtu yanaandaliwa katika nchi moja mwanachama wa jumuiya ya Ulaya. Hayo maandamano yanahudhuriwa na watu kutoka mataifa mbali mbali ya Ulaya na wanajisajili kama washiriki wa Kili marathon vile.
Kila nchi mwanachama inapeperusha hiyo bendera wiki mzima katika baadhi ya halimashauri na miji.
Waajiri wakubwa kwa wadogo wanatoa zawadi zilizopbwa na rangi hizo.
Ndo maana unaiona huko kwenye runinga. Wiki ijayo hazitaonyeshwa.