Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Kizazi cha dhahabu cha Ubeleshi kinatoka patupu, mwakani kwenye world cup wachezaji wao wengi watakuwa wanacheza michuano mikubwa ya mwisho
 
Sielewi kabisa mnaposema Belgium ina kizazi cha dhahabu mkuu, au Mimi sijuhi kizazi cha dhahabu ni nini? yaani akina chadli, Lukaku, witsel n.k ndiyo kikazi cha dhahabu.
Hata hiyo kuwa ranked namba moja siwaoni hivyo...

Hakuna kizazi cha dhahabu pale, wako overrated sana!!
 
Italy hawana timu nzuri pia, wanaweza kupoteza hili game kabisa, ngoja Martinez afanye sub nzuri aingie Carasco,Mertens au Chadli

Timu ya Italy bado ni nyepesi sana na Vermaelen atolewe amefanya mistakes nyingi
Huwezi kukubali japo macho yanaona. Italy wanacheza mpira unaonekana kwa macho kabisa lakini unasema sio timu nzuri. Kuna watu walisema hivyo hivyo Italy ni mbovu ila wanaonekana wazuri kwasababu wamepangwa na timu mbovu ngoja akutane na Ufaransa. Cha ajabu timu hiyo hiyo iliyokuwa kundi moja na Italy ndio iliyomtoa Ufaransa. Tukubali tu kwasasa Waitaliano wapo vizuri sana. Hata falsafa yao imebadilika kutoka kwenye mpira wao wa kuwa wanyonge wa kusubiri mashambulizi mpaka kucheza mpira buradani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…