Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Mpira bwana..yaani uholanzi wanautafuta kwa tochi! Washakufa mbili..
 
Waholanzi wamesaliti utamaduni wao wa 433 total football uliowapa heshima kubwa ulimwenguni kote.

Wacha warudi nyumbani wakajitathmini na kujipanga upya kuelekea Qatar 2022.
 
VP Netherlands v/s jamhuri ya check
Netherlands Wamepigwa 2 - 0 nafikiri kikosi chao bado hakijasimama sawia yani kinakosa wachezaji bora eneo la kiungo na ushambuliaji mtu kama de jong (aliestaafu) angewasaidia sana pia 9 yap sio nzuri waliochezq 9 leo depay na hata promes alieingia sub aio natural strikers ......

pili maturity ni ndogo refer red card na maamuzi ya kimpira bado wanachanfamoto.....pia hata mfumo wao wa 5 - 3- 2 sio mzuri
 
Czech wana historia na haya mashindano ndio maana niliwapa nafasi kabla ya mchezo.

Walibeba euro 76 kwa penati ya panenka, sio wakuja hawa.
Lakini hata Holland walibeba Euro 88 kwa kikosi kikali cha akina Gullit, Van Basten na Rijkaard ambao kwa pamoja walikuwa wanacheza Ac Milan na timu ya taifa ya Uholanzi
 
Mkeka wako vipi mkuu? Maana naona czech kawasha moto huko.
Mkeka wangu wa makuti ya Nazi Czech kaukanyaga juu kwa kiburi kilichotukuka kama baadhi ya viongozi wa awamu ya 5 katika Nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…