Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

France walikua ni overrated sana, nilizungumza mapima ila watu ni wabishi sana.

Defence yao ya kati ni utopolo, nilikua na uhakika kabisa ndio itakayo kuja kuwatolesha.

Ngolo Kante ndie mchezaji kilaza Zaidi kwenye timu yao, hakustahiki kabisa kuwa ni stater uwanjani.

Mbappe dogo kiburi kimemzidi kuliko hata uwezo wake, Nilishauri mapema Awekwe bench Giroud achukue namba.

Ila kocha aliwaogopa sana Kante na Mbappe japo kuwa alikua akielewa kuwa ni vimeo, hofu ya media na mafans wasiojielewa aliiogopa. Mwisho kabisa amevuna alichokipanda.
We sio shabiki wa mpira, hizi comment zinaonyesha ufahamu wako wa haya mambo ni mdogo sana.
 
Lile goli la Lampard ndio lilisababisha kuanzishwa GLT (Goal Line Technology)
Halaf hili goli nakumbuka lampard alipiga shuti kali kiasi kwamba ref na hata sisi watazamaji hatukuweza kuona kama ni goli
Nimeangalia tena sasa hv naona ni shuti la kawaida tu
 
We sio shabiki wa mpira, hizi comment zinaonyesha ufahamu wako wa haya mambo ni mdogo sana.

Nyinyi ndio wale washabiki mambumbumbu niliowakusudia

Nilichokizungumza mimi kina shida gani? Hukuona Kante alivyokua akizurura uwanajani kama chizi mpya bila ya msaada wowote kwenye timu?
 
Nyinyi ndio wale washabiki mambumbumbu niliowakusudia

Nilichokizungumza mimi kina shida gani? Hukuona Kante alivyokua akizurura uwanajani kama chizi mpya bila ya msaada wowote kwenye timu?
Mkuu unataka kusema Kante kwenye hii michuano hajaupiga mwingi??
 
Back
Top Bottom