Mimi sikujua kama hii ni hoja.
Unapokuwa katikati ya involuntary choice of life and harm/death halafu unapiga kelele jamii ikusaidie, sikudhani kama hiyo ni hoja kwa sababu hata nilichoandika kwangu mimi siyo hoja.
Mimi siko hapa kurumbana na wewe kwa sababu kwangu hii siyo hoja. Nilikuwa najaribu kujibu kilio chako. Tatizo unataka kutulazimisha tukubaliane na mawazo yako wakati hata hao unadai waliokugongea usiku wa manane (UK police) hawakukueleza yule anayetaka kukudhuru kimwili au psychologically.
Mkuu, Usitake kutufunga kimawazo na kama hukubaliani na scrutiny basi ungejifungia ndani ya dunia yako badala ya kuleta maisha yako hapa JF ili tujue nini kinachoendelea.
I'm sorry, kwa maisha yako kuwa hatarini but IF THIS IS NOT A MADE UP STORY. Afterall, THIS IS JAMII FORUM, WHERE PEOPLE DARE TO TALK OPENLY.
Nadhani ndugu yangu una ajenda yako binafsi.Hakuna mahala nilipopiga kelele,let alone kutamka tu, kuwa ninaomba msaada jamii inisaidie. Bandiko husika hapa JF ni matumizi ya haki yangu kama mwanachama wa ukumbi huu tangu mwaka 2006 kubandiko chochote ninachodhani kinafaa alimradi simtukani au kumkwaza mtu.
Inanishangaza unapodai kuwa upo hapa KUJIBU KILIO CHANGU.How can you respond to kilio kisicho-exist? Pia unanishangaza unapodai kuwa tatizo langu ni kutaka watu wakubaliane na mawazo yangu.Nitendee haki tafadhali.Hivi kuna mahala popote nimejaribu kumshawishi mtu aafikiane nami?
Narudia tena: sikuandika makala hiyo kwa minajili ya kutaka huruma ya mtu au kumwaminisha yeyote kuwa tukio hilo lilinitokea.Nimekuwa nikiandika makala kwa bloguni na magazetini kwa muda mrefu sasa,na kamwe sijawahi kutumia maandiko yangu kutaka kuwaaminisha wasomaji kitu wasichoamini.Actually, binafsi sijioni kama mwandishi bali a conversationalist,na maandiko yangu ni maongezi tu in printed form.
Sijakufunga kimawazo bali umeamua kwa hiari yako kufanya hivyo.Nimfunge mtu kimawazo ili iweje? And who are you to tell me what to post or not post hapa JF?
Yes,JF is allabout daring to talk openly lakini kichekesho ni kwamba pamoja na kutambua dhima hiyo uhuru wa kuongea kwa uwazi bado unajaribu kujenga impression kana kwamba nimetenda kosa la jinai kuweka bandiko husika.
Naomba sana unielewe kuwa bandiko langu halikuwa na dhamira ya ku-seek sympathy. Kadhalika, at no point, nimejaribu kumshawishi mtu yeyote yule kuamini au kutoamini nilichoeleza.So far, nilichotumia ni haki yangu ya uanachama wa JF kubandika makala ya jarida la RAIA MWEMA ambayo coincidentally inanihusu.
Nitaendelea kuheshimu uhuru wako wa kutafsiri habari hiyo kwa mtizamo wowote ule.