Evelyn wa chumvi...

Evelyn wa chumvi...

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Ilikuwa ni weekend tulivu na yenye kibaridi chepesi nilichoamua nikichangamshe kwa kurukia maeneo ya starehe!. Hakuna starehe niliyoipenda Kama ya kunywa!,naam kunywa kile kimiminika chenye rangi ya dhahabu ambacho hubadilisha akili kuwa katika uchangamfu.

Ilikuwa ni mida ya saa mbili usiku baada ya kuangalia saa yangu akili changamfu ikanituma nitembelee banda lengine la wanywa kimiminika Cha dhahabu!,ktk kufikiri niliona nisitoke patapu nikaamua nijichukulia zile tabia za uswahili za kutoka na chochote kitu!. Punde nilikuwa nje ya banda nililopo huku mkono wangu wakulia ukiwa umeshikilia bia aina ya Serengeti lager!,kabla ya kuchukua uelekeo wa wapi niende nilijipima kwa kujipepesa ili nijue bado nipo ngangari kiasi gani!.. pepeso bado lilinena nipo fiti japo macho yangu yalikuwa tayari yakiashiria ulevi ndani yangu.

Baada ya kupata uelekeo nilipiga hatua zangu kwa uangalifu huku nikijitahidi kutoonekana kama mlevi niliekithiri!,funda zangu kadhaa za bia yangu tamu zilinifikisha mpaka kwenye lango fulani la kioo huku kwa ndani nikiona watu na harakati zao,wahudumu na wateja huku wengine wakilisakata rumba kwa michezo ya kilevu huku wakicheka bila sababu! Hapohapo nami bila sababu nikaliangua tabasamu huku mkono wangu ukiwa mkabala kuufungua mlango.. chakwanza nilikaribishwa na muziki mzuri uliokita katika masikio yangu,pili ndo Sasa zilifuatia sauti za walevi ambazo sikuzielewa zikisema nini bali niliona kama zinashindana na muziki ule mzuri uliokuwa ukipigwa.

Baada ya kuifikia kaunta nilipokelewa na macho yawatu kadhaa mengi yakiuliza "wewe ni nani...??" Yote niliyapotezea lakini lipo jicho moja la mlevi lenyewe lilinena tofauti tukiacha na yale mengine yaliyoonyesha mguno wa "ohoo" ama "Toba". La mlevi huyu lilikuwa ni jicho lenye uangavu na usaliti! Nalo nikajifanya silioni nikageukia kaunta nikakutana na mwanadada kapakia wanja uliokolea mithiri ya usiku wa manane wa wachawi kuwanga!.. mdomo wake wenye lips nyekundu ulinikaribisha kwa bashasha ukinena "karibu,nikuhudumie nini?"

Swali lake ndio kama lilinigutua kuwa nina bia mkononi!,nikafanya kuiinua kumuonyesha kuwa ningependa anipatie kinywaji Kama kile. Lakini katika kufanya hivyo ni Kama alikuwa hanielewi ndipo nikaamua nimwambie kwa maneno "nipatie Kama hii" napo hakunisikia ikabidi nipaze sauti kwa kushinda sauti za muziki na za walevi wengine! "Nipatie kama hii" wakati nikitamka hayo ndio wakati huohuo muziki ulikuwa ukifika tamati!

Hivyo kulifanya sauti yangu isikike kwanguvu kupita walevi wengine kitu kilichofanya wapunguze minong'ono na kugeuzia macho yao yakilevi maeneo ya kaunta!. Ilipita sekunde kadhaa wakarudia kelele zao huku wengine wakicheka na wengine wakiupokea muziki mwengine ulioanza kupigwa.

Kurudisha jicho langu kwa muhudumu nilikuta akinisubiri nigeuke ili anijibu lakini kabla hajafanya hivyo alikatishwa baada ya kuona mtu nyuma yangu akunishika bega!. Niligeuka kwa pupa maana ilikuwa ghafla! Alikuwa na mmoja kati ya mlevi aliekuwa akilisakata rumba kama mtu anataka kukatika viungo vyake vyote!. Uso wake wa ulevi ulinilokea kwa tabasamu la kinafki nililoliona toka hapo awali lile jicho lake angavu na lenye usaliti ama uchochezi ndani!.. aliongea kwa pupa "we ndama umefata nini humu..?" Sauti yake ilikuwa kali iliyogutua baadhi ya watu.. kabla sijajibu aliiangalia chupa yangu ya bia huku akiisonta na kusema
"Hizi hazipo humu!" Akaongeza "huoni kila mtu anaglass?"

Ndipo jicho langu likaambaamba na kuangalia huku na huko nikagundua ayasemayo ni kweli! Niliporudisha macho yangu kwake akaendelea "wewe mtu mwenye sauti ya ndama umekuja kutufanyia fujo humu!"

Niliguna na kuitazama bia yangu kabla sijanena chochote Kisha nikapiga pafu nyengine nzito niliyogugumia huku nikimuangalia mlevi yule alienibatiza jina la ndama!

Nilipomaliza sikuonyesha kuwa na muda nae nikamgeukia mhudumu ambae alionyesha bayana alifatilia maongezi yale.. nilimtolea jicho kisha nikamuuliza

"Ayasemayo huyu mlevi mkorofi yanaukweli?" Kabla hajajibu mlevi yule alinivuta tena begani kwanguvu! Nilipomgeukia alitaka kunena lakini kigugumizi kikamzuia kwa sekunde mbili,punde akalipata neno alilotaka kunena. Kwa sauti kubwa alinena "Amekuja kutufanyia fujo huyu!" Walevi wengine wakanitumbulia macho kodo! Akaongezeka na mlevi mwengine nae akiunga hoja na kupiga zogo "mfanya fujo kaingia!"

Mfadhaiko ukanipata baada ya mlevi mwengine nilipomsikia akinena "Atatuua huyu!" Sikujua walinena hayo kwasababu gani bali kelele zao zilinitia hasira ndipo nikamshika yule mlevi wa awali na kumtia ngumi mbili nzito zilizompeleka chini akitapatapa na kupiga mayowe!,ilisikika sauti ikinena kwa nguvu "tobaaa" watu wote waligeuka na kuona mlevi mmoja yupo chini hapohapo yule alienena atatuua huyu akanena zaidi kwa mayowe "nilisema mimi!"

Macho yote yalinitazama na punde waliingia mabaunsa wawili wakinifata mgubegube! Tahamaki nimebebwa na kwenda kutupwa nje huku nikisindikizwa na matusi mazito!

Narudi..
 
Eve wa Munyu
giphy.gif
 
Niliinuka mzimamzima wakati huo nikiangalia mlangoni huko kwa ndani mlevi yule mkorofi niliemtia ngumi alitaka kunifata kwa fujo huku wengine wakijaribu kumzuia wakimvuta kwa nyuma na kumsihi arudi baada ya dakika mbili alirudi na kuendeleza kasheshe zake!.

Niliirudia saa yangu na kukuta mishale ikisoma saa tatu na robo za usiku,akili yangu ikanena nitafute kiwanja chengine! Lakini likanijia swali kwanini nisichukue vilevi na kwenda kunywea gheto..? Nikaona hili wazo lapili ndo linalofaa zaidi.. katika kujivuta nikaona nishike njia ya kwenda gheto nitanunulia huko mbele yasafari!.. kibaridi chepesi bado kiliendelea kupiga ktk namna isiyokera bali kuhamasisha zaidi.
Katika njia hii ya rami nilipita pembezoni kabisa mwa barabara huku yakikatiza magari machache na pikipiki kadhaa,lakini baada ya tembea yangu ya kama dakika kadhaa nyuma yangu ilikuja gari iliyokuwa ikinikaribia!.. nilishitushwa kidogo baada ya kuona gari ile ikinikaribia na kunipiga mwanga wake,ilipofika mkabala na mimi ilipunguza mwendo nami nikaipa attention nikasogea karibu na kuchungulia ndani yake!.. nilipokelewa na sauti tamu yakike ikinena "Mambo" sikujibu haraka bali nilibaki nikitafakari kitu ambacho hata hakikuwa na maana!! Dada wa watu akanena tena "Mambo kaka" Mara hii nikagutuka na kujibu poa huku nikijilaumu mawazoni kwa kushindwa kujibu salamu yake yakwanza!.. alikuwa ni mwanadada mwenye jingi tabasam na sura fulani yenye kunena umboga Saba!. Punde Tena sauti yake ikakita masikioni pangu ikinitaka niingie garini Kama sitajari anisaidie kunifikisha mahali niendapo!. Sikutaka kukubali haraka nionekane kama boya fulani!,nikaligeuza shingo langu ili nitizame siti za nyuma nione Kama kuna viumbe wengine lakini hakukuwapo kiumbe zaidi yake tu!.

Sikujibu chochote bali nilifungua mlango na kutumbukiza roho yangu katika gari lile aina ya Benz nyeusi.. mrembo alikanyagamoto na gari ikaendelea kukanyaga rami.. kilipita kitambo kidogo tukiwa kimya ndipo mrembo yule akaamua avunje ukimya!.
Nilikuwepo mule!
Nikauliza wapi..?
Kule ulipoitwa ndama!
Kabla sijanena chochote akaendelea "Mule hawatumii bia bali wanakunywa wine!"
Nilikubali kwa kusemo "ohoo mi sikujua!" Likafata swali jengine
"Kwani we ni mgeni huku..?" Nikajibu hapana isipokuwa sio mwenyeji eneo lile ni mara ya kwanza kuwepo pale!..
Wakati nikimjibu hayo alikuwa akinitazama huku akiliangua tabasam hafifu,macho yake yakiwa hayajatulia yakitazama mbele huku akinigeukia tena mimi!. Kilipita tena kimya Kisha akaniuliza " unaitwa nani..?" Kabla sijajibu nilitafakari nikinaribu kufikiri nimpe jina bandia au halisi!. Lakini nilitupilia mbali ubandia nikaona nimpe kile kilicho halisi!.. "naitwa Jonas"
Tabasam lake likachanua zaidi! Huku akitupia kiingereza "such a good name!" Bila hiana nikaachia kiingereza changu chakilevi " thanks".
Mara hii ndio ulikuwa muda wangu wa kuanza kumfaidi mrembo huyu kwa macho yangu yakilevi!. Nilitupia jicho katika viunga vya mwili wake aliouvisha kigauni chepesi chekundu kilichoishia magotini ila kilivyo na purukushani za kikorofi kilijivuta kidogo mpaka juu ya mapaja yake hivyo kufanya mtazamaji kukata kiu cha macho!.
uzuri wa mapaja yake tu ulitosha kuanza kunitia dosari za tamaa nilizozikata kwa kuanza kumuangalia usoni ambako sura yake nzuri ilijihamasisha kuangalia mbele tu!,niliyafanya haya kwa kuibia nisijeonekana fisi mfilisi!.
chengine kilichonivutia zaidi ni ule weupe wake ambao haukuwa wa kununua madukani!,hata lips zangu hazikupakwa marangi ya husuda kama ukuta wa jiji!.

kimya kidogo nikaona usiwe tabu nikatupia swali nami kutaka kulijua jina lake "mrembo unaitwa nani..?" Alitabasam nakujibu "naitwa hivyohivyo mrembo!" Alijibu hivyo huku akisindikiza na kicheko chepesi!.
nikaongeza "ohoo ni haki yako hata hivyo kuitwa hivyo!" Akaguna na kuuliza tena "kwanini.?"
Nikajibu "kwasababu hata ile nywele yako moja tu inatosha kuhubiri kuwa wewe ni mzuri!!"
alicheka huku akiunyonga usukuni kuelekea upande wakulia ambapo alikata kona iliyonifanya niwe natuswali hafifu juu ya mabadiliko hayo! Alilitambua hilo hapohapo akanena "sorry napita hapo supermarket Kuna vitu vichache nachukua!" Nilikubali kwa kutikisa kichwa..

Narudi..
 
Back
Top Bottom