Niliingia mpaka ndani huku nikiwa na bapa yangu nimeikumbatia kwapani kwenye mkono wakushoto,niliivuta nakuisogeza tena Kisha nikaiweka usawa wa macho yangu nikiiangalia kwa lile jicho la tamaa mbele mauti nyuma!.. Wala hata sikungoja niliduguda tena kwa pigo moja nakujikuta nikifumba macho huku nikikunja sura Kisha nikaiangalia tena nakujikuta nikijisemea "machozi ya mamba haya!"
Kabla hata sijakaa sawa ndipo punde hiyohiyo nikaona mwanga kwa nje ukijitahidi kutaka kupita ktk mlango wa chumba changu!,kikapita kimya masikio yangu yakanasa muunguro wa gari Kisha hapohapo nikasikia honi ya gari hilo ikihanikiza mara kadhaa!.
Nilijua huu ulikuwa ni ugeni wangu lakini haukuwa na taarifa kwa mara nyengine tena nikaitazama saa yangu ilionyesha ni saa tano nadakika hamsini na tano!,nikajikuta nikiropoka nani tena huyu..? Honi nazo ziliendelea kufikia masikio yangu nakuleta kero ambayo sikupenda kuisikia!.
Kwauchovu wakilevi nilijivuta na kuufungua mlango wangu napo nikalakiwa na mwanga wa taa za gari lile!,nikalifata na ndipo nilipogundua garini alikuwa ni Eve!
Kwasauti yakilevi niliyojitahidi kuificha nilimuuliza "mbona umerudi mrembo..?"
Alinitazama na kisha akafungua mlango wa gari nakunifata niliposimama.. "I need your company jonas!" Alijibu huku akinikaribia.
"Company..?" Nilihoji kwa mshangao huku nikimtupia macho ya maswali.. Mara hii alikuwa ameshanikaribia zaidi mpk niliyasikia marashi yake mazuri aliyokuwa amejipulizia,marashi yaliyoonekana kuwa ya gharama yaliyoishinda harufu yangu ya vimiminika vya vilevi nilivyovitungua usiku huo!.
Eve akaongeza "yes company ningeomba unisindikize kwenye birthday party ya rafiki yangu!"
Niliguna na kisha nikaitazama saa yangu nakuonyesha Kama mtu mwenye wasiwasi juu ya ombi lake,nikabaki kutafakari kidogo nilipomtazama kwa mara nyengine nilikuta macho yake yakiangaliana na macho yangu!,nilimtazama kwa tuo nakugundua alikuwa akinitazama kwa hamu kama mtoto alieona sukari ikipitapita mbele ya uso wake!. Kabla sijanena chochote akaongeza kwa sauti ya kudeka
"Please Jonas I need your company!"
Mara hii nikaliangua usoni kwangu tabasam hafifu nakujikuta nikimezwa na uzuri wake hapohapo mawazo yangu yakaanza kunilaumu kwa kuchelewa kuchukua maamuzi! Niliwaza "Hii bahati yako!" Wazo jengine likatamalaki "Mbuzi kafia kwa muuza supu!".
Mpaka hapo sikuwa napingamizi nilimuangalia Eve nakumjibu "sawa!" Alifurahi na kunijibu "ahsante"
Punde nilikuwa ghetoni nikiangalia nini chakuvaa usiku ule ili nimsindikize mrembo yule mahali ambako sikupajua!,Kuna muda niliona Kama nimemkubalia kirahisi ombi lake Tena mtu ambae nimemfahamu hivi punde tu! Nilijishangaa!! Lakini tena nikajiuliza "kwa uzuri ule naachaje kuwa company yake..?" Wazo jengine lakijinga likanijia "Kama unaenda kunyonywa damu je..?"
Niliguna nakulitupia mbali wazo hilo,hapohapo ikanijia na twasira yake vile alivyokuwa amevalia, kigauni cheusi kifupi chenye marumaru yang'aayo kwa mbali huku chini akiwa ametupia viatu vyeusi vya mchuchumio!. Nilitafakari nakuamua nami nivalie vipi ili niendanenae.
Ilinichukua dakika sita nikawa tayari nimeshatupia jeans nyeusi na tisheti ya kijivu huku nikisindiikiza na mkoti mweusi ambao niliuachia wazi bila kufunga zipu yake,chini nikavalia raba nyeusi zenye mistari myeupe kwa chini.
Nilipotoka alinipokea kwa macho yake mazuri nakutupia neno fupi tu "Nice" nami sikuwa nyuma hapohapo nikamsindikiza na usemi "hiyo marumaru yako yanitia kihoro!" Aliangua kicheko huku akiwa mkabala na mlango wa gari tayari kwaajili ya safari...
Ilituchukua Kama dakika kadhaa tu mpk kufika ktk moja ya hotel kubwa iliyofahamika kwa jina la king's hotel,baada ya kupaki tuliingia mpaka kwenye ukumbi tuliokuta watu kedekede waliovaa nadhifu huku wengine wakionekana tayari ktk hali za macho remburembu.. eve alinivuta hadi upande wa kushoto kulipokuwa namakochi mawili yaliyopangiliwa huku katikati kukiwa na meza ndogo ya kioo!. Aliniomba niketi Kisha akaniambia anarudi hivi punde.
Nilitulia huku nikitupia macho huku na kule nakuona watu kadha wa kadha wakiwa ktk makundi wakipiga stori mbili tatu. Mbele yangu niliiona maneno makubwa yakinakshiwa vizuri huku yakiwa yameandikwa "HAPPY BIRTHDAY MARRY" mapambo mengine yalihanikiza huku taa za marumaru nazo zikiwa hazipo nyuma ktk kufanya manjonjo yake!.
Mawazo yakaikumbuka ile bapa yangu niliyoiacha gheto nakujikuta nikijiona kama msaliti wa kinyaji changu ambapo mpaka sasa midugudo ile kadhaa bado iliendelea kutamalaki ktk viungo vya mwili wangu!. Kelele hafifu za maongezi ya watu zilinigutua Tena kurudisha fikra zangu ktk ukumbi ule! Dj aliukamata umakini wangu baada ya kucheza nyimbo moja wapo ya msanii wangu pendwa aliefahamika kama mfalme wa pop!
Alikuwa ni Michael Jackson na kibao chake cha "you rock my world" taratibu mguu wangu wakulia ulianza kwenda namapigo ya wimbo ule huku napo mkono wangu wakuume niliouegemeza kochini ulianza kutikisika vidole vyake!.. punde Eva alinigutua huku akitupia sentensi "samahani kwa kukuacha mpweke" aliyanena hayo huku akiniangalia kwa kitabasam chokonozi!.
Nilimuambia kuwa haina shaka..
Tofauti ya ujio wake huu alikuja na mgeni mmoja wapo!,mgeni ambae alikuwa amemshikilia kwa mkono wake wa kulia huku mkono wake wa kushoto akiwa na glass mbili ndogo!.
Alimtua mgeni yule mezani kisha akaziweka glass zile karibu na mgeni wetu mpya aliesomeka kwa majina "saint addo!" Kwa bashasha Eva alinikaribisha "karibu tujitibu" wakati akiyanena hayo mikono yake ilikuwa bayana ikiifugua kifuniko cha kinywaji kile kilichokuwa na rangi nyeusi! Alimimina katika glass zote mbili Kisha akanishikisha yangu nae akaishika yake!.. wakati akiyafanya hayo alikuwa amesimama ila baada ya kuishika glass yake alikuja kukaa mkabala namimi nakujikuta miili yetu ikigusana kwa namna ya watu ya kinamna!..
Baada ya kupiga funda moja ya kinywaji kile radha nisiyoielewa ilinienea ktk kinywa changu! Eva akaniangalia kwa tuo na kuniambia "hichi ni kinywaji changu pendwa" nami nikamuitika kwa kumwambia "sijazoea Mambo ya hivi" alicheka na kutupia utani "we umezoea yale ya kuitwa ndama..?" Mara hii tulijikuta tukicheka kwa pamoja!.
Ilikuwa ni taswira nzuri katika ukumbi ule ambao ulisheheni watu kadri muda ulivyozidi kwenda lakini ktk punde hii tuligutuliwa na sauti ya kiume iliyosikika katika spika ikituomba watu wote tusimame kwaajili ya kufanya kile kilichotuleta maeneo yale.. Alionekana binti aliependeza haswaa akiwa amevalia gauni la blue lenye kufunika miguu yake, taratibu huku akisindikizwa aliikaribia meza kubwa iliyokuwa imepambwa kwa marumaru na mioto iliyoonekana ikiwaka juu ya keki kubwa iliyovutia machoni.. ni wakati huu mc wa sherehe alimkaribisha mrembo huyu akakate keki yake huku akituomba tuimbe ile nyimbo ya happy birthday.. ukumbi ulilipuka kwa shangwe na bashasha Eva nae hakuwa nyuma mara hii akiwa amesimama pembeni yangu huku akiikamatilia glass yake alionekana kuwa mwenye shangwe na uchangamfu ambao sikumuona nao hapo kabla!.
Keki ilikatwa, champagne ikafunguliwa wenye Kunywa tukanywa na wenye zawadi wakatunuku,ilikuwa ni sherehe ambayo haikuchukua muda mwingi sana bali ilikuwa ni Kama starehe ya muda tu ndipo Sasa ukafika ule wakati wa dj kuzichangamsha nafsi za watu kwa kutumia ujuzi wake maridadi!.. santuri ziliitika na kufanya kila mmoja katika ukumbi ule kutokuwa mvumilivu nakujikuta sote tukinengulika kwa kufuata midundo ya muziki.. dj alirukia wimbo huu na ule na zote zilipokelewa kwa mayowe Kama si vifijo!.
Eve niliemfahamu muda mfupi hakuwa tena yule!,eve wasasa alikuwa mchangamfu kupita kipimo hakuna wimbo ulimpita!,kwa viungo vyake laini alicheza kwa madaha huku akinengua kwa pozi zilizokuwa zikionyesha dhahiri kile kinywaji cha "saint oddo" kilikuwa kimefika hatua za majinuni!.
Si kiuono chake tu bali mwili wake wote ulionyesha umaridadi katika kulisakata! Nilibaki nikimtumbulia macho nisijue niangalie kiungo kipi katika viungo vyake maana vyote vilionekana kucheza vizuri!.. eve alinitupia jicho nakuchanua tabasam alinisogelea nakunivuta huku akitupia maneno "acha ushamba"
Tulijikuta tumeshikana yeye mbele mimi nyuma yake tukilisakata kama wapenzi tuliobakiza siku chache tu tufunge ndoa!,mikito ya muziki ilizidi kunoga huku kila mmoja akijitahidi kuonyesha ufundi kwa mwenzake. Hakuna alietaka kushindwa! Kwa mikono yangu nilishika kiuno Cha eve kilichokuwa hakitulii kwa dansi za huku na huko! Niliona kama naenda kuzidiwa kete na kugawa ushindi kwa binti huyu niliyemfahamu kwa machache tu!.
Sikutaka iwe hivyo nami nikabadili namna ya uchezaji kwa kumgeuza anigeukie Kisha nikamsogeza karibu zaidi nakushika kiuno chake laini nae bila hiana akaweka mikono yake mabegani kwangu huku akinitazama kwa kurembua na kunikonyeza aliendeleza dansi ambapo mara hii aliniachia nafasi ya kuupapasa mwili wake,kitu kilichofanya nione nimepewa nafasi ya upendeleo hivyo hata kete za ushindi ziliegamia upande wangu!. Hakuna pigo la wimbo lililotushinda kucheza!,kila staili ilifana nakujikuta tukifika mbali na kuangaliana machoni kwa tamaa zilizowika zaidi na zaidi!..
Niliiangalia saa yangu nakugundua ilikuwa yapata saa tisa za usiku! Nilijinasua kwa eve nakumshika mkono wake wakulia Kisha nikamvuta pembeni,ndo kwanza alibaki akinitumbulia macho kwa kuona nikikatisha dansi aliyopenda kuona ikiendelea zaidi na zaidi!. Sikuyajali macho yake bali nilimkalibia kwenye sikio lake lakulia na kumwambia "turudi nyumbani!" Alinishangaa nakutupia neno huku akitoa sauti ya kilevi yenye deko
"mi nilijua tunakesha!"
Niliguna na kumtazama tena nikauona uso wake ulivyona husuda ya kutaka dansi tena na tena lakini majinuni mimi kwa minyweso niliyoichanganya leo mwili ulikuwa ushachoka na kibofu kuchoka kujaza vimiminika mbalimbali!.
"Hapana hatuwezi kukesha mi najihisi kuchoka!" Nilimwambia eve ambapo wakati huu alikuwa akiniangalia jicho la ushawashi zaidi akinitaka tuendelee kubaki!,nilijifanya kuangalia pembeni kwa sekunde kadhaa na kulipilotezea jicho lake chokozi kisha nikamvuta huku nikiongozananae kuelekea mlango wa kutoka nje! Ghafla kwa sauti ya deko akang'aka "tubaki bhana mi sijatosheka" nilipogeuka alionekana Kama mwenye huzuni kutokana na uamuzi wangu,lakini punde hii sikutaka kupelekwa kikondoo kama hapo awali!.. niliendelea kumvuta mpaka tukatoka nje!..
"Sasa ndo nini..?" Aliuliza huku akiuvuta mdomo wake!
"Imetosha eve" nilijibu
Kilipita kimya huku mwenzangu akionyesha Hali ya kununa! Ilikuwa ni picha ambayo waliyopita walituoa kama wapenzi tuliokwazana lakini bado tuliendelea kuhitajiana!.
Hatimae eve alinikubalia kishingo upande huku akinikabidhi funguo za gari na kuniomba mimi ndo niendeshe,tulijivuta mpaka kwenye parking ya magari nakuchukua gari yetu tukatokomea gizani kwa kuishika rami iliyotupeleka ktk njia tulitokujia lakini punde....
Narudi..😀