Wacha kuchekesha wewe, ni nchi gani ambayo uchumi wake upo na mizizi mirefu katika ukanda huu, uchumi wa Tanzania umebebwa na:
1) Kilimo, Uvuvi na Ufugaji: Tanzania ndiyo nchi pekee yenye ardhi kubwa na yenye rutuba kwa ajili ya kilimo, Tanzania ndiyo nchi yenye ukanda mkubwa wa bahari ya Hindi, na Maziwa matatu makubwa kwa ajili ya Uvuvi, Tanzania ndiyo nchi yenye mifugo mingi nyuma ya Ethiopia.
2) Utalii, katika hili sina sababu ya kuelezea uimara wa utalii wa Tanzania
3) Madini, hapa sihitaji kusema lolote, nadhani unajua kuhusu wingi wa madini Tanzania.
4)Natural gas; Unafahamu wingi wa gesi iliyopo Tanzania.
5) Uzalishaji wa viwandani: Ninadhani unaona ni kiasi gani bidhaa za viwandani za Tanzania zinavyosambaa katika nchi Jirani, kuanzia bidhaa za Azam, Mo, na bidhaa zingine.
6) Usafirishaji; Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi, na Zimbabwe, hutegemea sector ya Usafirisha wa Tanzania kwa zaidi ya 8O% ya bidhaa zao.
Tafadhali taja uchumi wa Kenya umeshikiliwa na "Sectors"zipi ambazo ni strong zaidi ya " Remittances?"