kalisheshe
JF-Expert Member
- Mar 19, 2020
- 2,477
- 5,096
Afrika ni bara lenye utajiri mkubwa wa watu wenye akili, vipaji, na uzalendo. Lakini cha kushangaza ni kuwa mara nyingi watu hawa hawathaminiwi, badala yake wanabaguliwa, kudhulumiwa, au hata kupotezwa. Je, kosa lao ni kupenda haki, kusema ukweli, au kutotaka kujipendekeza?
Tunawaona waandishi wa habari wakinyamazishwa kwa kuandika ukweli. Tunawaona wasomi na wataalamu wakikimbilia nje ya nchi kwa sababu mawazo yao hayathaminiwi. Wapo waliopigania haki, wakapotea au kufungwa mwisho wa siku Jamii na familia zao zimebaki na majonzi.
Hali hii inaleta hasara kubwa kwa bara letu. Badala ya kutumia akili na weledi wao kuleta maendeleo, tunawasukuma waende mbali au kunyamaza. Vijana wanaona kuwa kusema kweli ni hatari, na kujipendekeza ndiyo njia pekee ya kufanikiwa.
Afrika, huu si wakati wa kuwaadhibu walio waaminifu. Ni wakati wa kuwakumbatia, kuwapa nafasi, na kuwatumia kama msingi wa kuijenga Afrika mpya. Tusipoteze hazina yetu kwa sababu ya hofu au siasa.
Tujifunze kuheshimu weledi. Tuwape heshima wanaosema ukweli kwa nia njema. Hapo ndipo Afrika itang'aa kweli.