Ewe DOLA, ikikupendeza 2025, Tuleteeni Luhaga Mpina

Gwaji labda atawale kwako.
 
Umesema kweli tupu!
 
Huyu mbona anakuwa dhaifu? Si aige akina Angela Makel!
 
M
Mpina ni double standard je anaweza kuheshimu katiba ya nchi? Nadhani Mbunge Msukuma amewahi kuweka wazi mapungufu yake mengi ya Mpina,sidhani ni mtu sahihi hata kama dunia ingebakiza mtu mmoja.
 
Hapo Ongeza Polepole ,Bashiru na Ndugai.
Hawa watu hata tukiwakataa Leo lakini maadam mwasisi wa nchi hii aliipanda Mbegu ya uzalendo na kapinga dhulma Iko siku atatokea Rais Mkorofi kuliko Sadam Huseni na wezi wote watasambaratishwa.


Mwaka 1995 Mwanza sangara walikua na ukubwa wa karibu futi nane . Sangara mmoja alikua anapakiwa kwenye Pick up na anatosheleza na kuinyanyu juu.

Mpina yupo sahihi. Hii nchi na nchi nyingine za Kiafrika haziwezi kuendelea Kwa kuongozwa kirafiki na kishkaji. Ni lazima atokee mtu mkorofi sana . Mtu anayeweza kumchapa makofi mwezi wa Mali za umma. Haiwezekani kuendelea kuwabembeleza wahuni kwenye nchi.
Nchi Ina rasilimali nyingi sana haiwezekani eti tunategemea tozo Toka Kwa maskini Kwa ajili ya kuwapa starehe watawala. Wazungu walikuja Karne ya kumi na Tisa nchi ikiwa gizani Totoro lakini wakitumia rasilimali walizozikuta na wakaijenga nchi Kwa Miaka hiyo na viwanda. Iweje Leo wasomi wapo lakini wanadhinda kwenye mabaa na starehe za Wanawake huku wakiangalia maslahi yao tuu halafu hawataki kutoka kwenye sanduku la kura.

Magufuli angefufuka Leo ( Mungu amrehemu Huko aliko ) watanzania wengi wangemchagua na asingepata mpinzani asilani.

Kosa lake lilikua ni kuwabebe sana CCM na kuwaacha Wakurugenzi kuvuruga uchaguzi mkuu . Na pia kuua upinzani lakini mambo mengine Kwa kweli Magufuli was the Best President ukilinganisha na walamba asali wengine kwenye suala la kulinda na kusimamia Rasilimali za Nchi yetu na kuwashughulikia Wezi waliojiunga na majizi ya Dunia kuangamiza nchi Kwa manufaa yao.
 
"Wewe Mpina, ni kichaa kama mimi, nimekupeleka Wizara ya uvuvi"

Unataka kusema Tanzania inatakiwa kutawaliwa na vichaa?
 

Toa Gwajima, weka Bashiru.
 
Duh, Mbona mada yako umeififisha mkuu!

Kichwa cha mada hukukishughulikia ipasavyo. Ulitakiwa uweke mkazo wako hapo, lakini badala yake ukapiga chenga chenga huku goli likiwa wazi na kushindwa kufunga goli!

Kama bado hunielewi ninachoandika hapa, ... hao uliowaorodhesha hapo chini ndio akina nani hao kuhusu maswala yako uliyopiga chenga nyingi nayo?
Lakini, Hata Gwajima, ni Gwajima yupi huyo, lakini wote wawili niwafahamuo sioni sababu ya kuwaweka hapo!
 
Kwani alianza yeye kuchoma nyavu nchini?,moja ya adhabu za uvuvi kharamu ni kuteketeza zana hizo kwa mujibu wa sheria.
Wewe unapendekeza wavuvi kharamu washugulikiwe vp wakamatwapo?
 
Sio sisi tu, Bali mwenye Sifa thabiti, uthubutu , Haki, Maono ,Mzalendo a k.a mfia Nchi ,mtu wakunitoa Muhanga kwaajili ya wengi japo atachukiwa na wahuni , Mwenye Hofu ya Mungu .
Mpina hana sifa yoyote kati ya hizo ulizozitaja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…