Ewe kijana, Jenga ustaarabu na mahusiano mazuri na jamii.

Ewe kijana, Jenga ustaarabu na mahusiano mazuri na jamii.

Na wengi wanaosema hyo ukifatilia sana ni walimbukeni mkuu..

Seriously naonaga mtu mshamba sana anavokua anaongea msemo huo.

Yaani huu ni ushamba sana
Ndo wale vijana wa kuiga vitu kutoka kwa akina diamond bila kuangalia madhara yake.
 
Kabisa hawa wameharibu sana hiki kizazi ,vijana nao kwakujikuta wamechelewa kimbilio lao ni kamari. yaani uweke 1000 yako kesho uamke na million,sisemi haiwezekani,

Ila ni Kwa wachache mno huku wengine wakizidi kupotea na kupoteza zaidi
Washamba tu...
Mi huwa nashangaaa sana madogo wa sasa hvi wana ujanja wa kishamba sana.

Unakuta mtoto wa kike pombe, Bangi, na kutwa kucheza visingeli et
 
Salaam jamiiforum

Mimi ni mtu mzima sasa, Baba wa familia,naweza kuwa sipo sawa Kwa mambo mengi,ila nimeruhusu kukosolewa na kuimarisha uhusiano na jamii kiujumla.

Threads zangu nyingi zinamlenga kijana wa kiume,si kwamba nimemuacha mtoto wa kike,la hasha.

Nimeanza na shina kwanza ,kulingana na mabadiliko ya mwenendo wa Dunia na utandawazi uliopo,stori kuhusu kulegea Kwa baadhi ya vijana zimekuwq nyingi mno.

Shida ni nini?

Maisha ni magumu Sana?

Wazazi na walezi tumeruhusu vijana kuishi lifestyle yao?

Au maisha ni rahisi tofauti na zamani?

Haya ni maswali machache kati ya mengi kumuhusu huyu kijana wa thamani kwenye hii Dunia.

Lakini jamii nayo ni kama imeamua kukaa kimya na kila mtu kudili na mambo yake,

Nakumbuka zamani nikiwa mdogo nishawahi kupigwa na mtu ambaye si mzazi wangu,baada ya kuwa tunapanda juu ya mti na kujirusha chini ikiwa ni sehemu ya kufurahia michezo hiyo.

Baba yangu mzazi nilishuhudia mara nyingi akiwachapa watoto wa mtaani Kwa makosa mbalimbali na aliishia kupongezwa na wazazi wa watoto hao.

Lakini Kwa sasa si mjini si kijijini usirogwe ukamchapa mtoto wa mtu eti unamuonya , unaweza kuwalisha watu mwaka mzima na ukajuta.hali hii imesababisha kupatikana kizazi kilegevu na chenye kudeka hadi ukubwani.

Zifuatazo ni njia zitakusaidia kujenga heshima na uhusiano mzuri Kwa jamii,japokuwa hizi si Sheria unaweza kuishi utakavyo ikiwa tu huvunji sheria.

1.Acha kuvaa kaptura fupi ,

Kijana wa kiume kuonesha mapaja ,au mb**o imejichora na wewe huna hata habari ndiyo Kwanza una vi ipod
masikioni,badilika.

2.Acha kuvaa hereni

Wewe siyo ,msanii,siyo footballer,siyo star ,hereni za nini ,badilika.

3.Salimia watu,

Jenga utaratibu wa kusalimia watu,hata ukipunga mkono ni ishara nzuri tu,siyo muda wote earphone ,ukiulizwa vina faida gani huna majibu, badilika.

4.Usipende Kula mbele za watu

Upo zako kijiweni na wana hujui wenzio wapoje kipesa,we unaagiza wali Kwa mamantilie na kuanza kutupia huku ukifurahi mara ndizi,mara ununue hiki,mbaya zaidi unakula hukaribishi ikiweza nenda kwa wauza chakula piga msosi wako rudi kijiweni, badilika.

5.Toa msaada inapohitajika,

Hasa wazee waliotuzunguka waweza kumpokea mzigo,au kumsaidia kufanya hata kazi ikiwa muda unaruhusu.

6.Usipende kupiga mswaki nje ,

yaani watu wanapita,wewe mara usukutue hivi mara uteme hivi. siyo tabia nzuri.pamoja na kutema mate mbele za watu, badilika.

7.Jitahidi kunukia vizuri.

Uchafu siyo sifa,hata kama kazi zako ni za hivyo,jitahidi kuwa msafi mara baada ya kumaliza kazi zako.

8.Oga vizuri baada ya kujamiiana na mpenzi wako,

kuna wanawake wana harufu kali hivyo unaweza kuta ile harufu haitoki tu,ikiwa hutojisafisha vizuri.badilika

9.Ongea kwa ustaarabu na simu yako.

Hakuna sababu kila mtu kujua MBA Kula nini nyumbani kwenu,kama uko kwenye daladala basi kila mtu ajue unazungumzia nini,hata kama unamdai mtu au ,au unatoa maaagizo fulani.badilika.

10.Acha kukaa kwenye foleni zisizo za lazima,

Unakuta mtu kisa kachanga basi, lazima ale hiko chakula,au sehemu ya kulipia pesa kidogo ili upate haki yako, wewe unapanga foleni +kusukumana.
Badilika.
Sawa mkuu
 
Vijana pia tuwe humble mno..
Humbleness is pretending

Kama kijana kuwa na nidhamu Katika maisha yako.

Usijiingize katika mahusiano ambayo hayana faida kwako be mutually acha mazoea ya wanawake.

Achana na vijana wenye slogan za kipumbavu kama vile
""Tafuta pesa "".

Sikwambii usiwe na marafiki ila unapokua kijiweni acha kuchangia mada za ajabu ajabu ikiwemo kuongelea wanawake na mahusiano.

Linda sana afya yako maana kut mbea na wanawake wengi sio sifa na hakuna tuzo.

All in all kuwa na nidhamu
Nidhamu ni neno pana ila kuwa na nidhamu kwa kila kitu kwani nidhamu itakufundisha hekima...

Na kama ni kijana na jf hapa kaa mbali na makundi ya watu kama Vishu Mtata 😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄😄
Mimi ni kijana mwema, mfano wa kuigwa. Mtaani naitwa mtakatifu, bar naitwa mstaarabu, kanisani naitwa mtumishi.
 
Back
Top Bottom