Ewe Msanii/Kijana wa kitanzania sahau kuhusu mafanikio endapo huna nidhamu

Ewe Msanii/Kijana wa kitanzania sahau kuhusu mafanikio endapo huna nidhamu

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Nawasalimu kwa jina la Chama Pendwa (CCM).

Leo nimeamua niandike kuhusu suala zima la nidhamu kwa wasanii wetu pamoja na vijana wote wa kitanzania. Vilio ni vingi kuhusu hali ngumu ya maisha huku wanaofanikiwa wakiwa wachache. Sababu ni nyingi sana ila mimi nitajikita kwenye kitu kinaitwa NIDHAMU.

Chanzo kikuu cha hii thread ni sakata la kutupiana maneno kati ya komredi P Funk (Baba Paula) na WCB Wasafi. Kila upande unatuhumu upande mwingine kwa kile kinachoitwa unyonyaji na dhuluma kwenye maslahi ya wasanii. Tuhuma dhidi ya P Funk ndo zilinigusa zaidi.

Inasemwa kwamba wasanii wengi waliopitia usimamizi wa P Funk wameishia kuwa maskini huku watetezi wa P Funk wakidai hao wasanii walipata maslahi yao yote ila wakatumia vibaya.

Baada ya tafakuri ya kina huku nikijikumbusha hali za wasanii wengi wa zamani na wa sasa kiuchumi nikaona pamoja labda na kuwepo dhuluma kwenye haki zao ila nao pia walikosa au kupungukiwa sana NIDHAMU na kujikuta wanarudi kwenye ufukara. Inasikitisha sana.

Neno NIDHAMU liko kwa upana wa kutosha. Wengi wa wasanii waliofulia hawakuwa na nidhamu ya fedha wala nidhamu ya kawaida kwa watu waliokuwa wakiwashauri vyema.

Tukiangalia wasanii na vijana wengine waliofanikiwa hapa nchini utaona wengi wakiwa na nidhamu sana kwa wakubwa zao. Diamond kumheshimu Babutale, Sallam na Mkubwa Fella kunachochea mno mafanikio yake. Au Millard Ayo kuwaheshimu maboss zake wa Clouds na kwingine alikowahi kufanya kazi. Kwenye siasa nako vijana waliofanikiwa kama Zitto Kabwe, Mwigulu, Nape, Januari, Polepole, Bashe na wengine ni kwamba wana wanajiheshimu na kuheshimu wakubwa zao kwenye chama.

Nakusihi kijana wa kitanzania badikika anza kujiheshimu na kuwa na nidhamu kuanzia ngazi ya familia hadi jamii inayokuzunguka. Connection hutapata kama tabia zako hazieleweki.
 
Nidhamu ni kitu cha msingi kuelekea kwenye mafanikio
 
Saida karoli, Rose mhando hawakuw watiifu,
Diamond kuingia bitu na Ruge imakaaje.
Nidham ni mhim ila mafanikio ni zaid ya hilo.
 
Back
Top Bottom