SoC04 Ewe mwanamke jithamini

SoC04 Ewe mwanamke jithamini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mama Semeka

New Member
Joined
Jun 3, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Hapo zamani za kale jamii nyingi za kiafrika hazikumthamini mwanamke. Mwanamke hakupewa nafasi yeyote katika jamii. Mtoto wa kike hakupelekwa shule, hakuruhusiwa kumiliki mali, hakuweza kufanya maamuzi yeyote katika jamii yake zaidi zaidi Watoto wa kike walisubiri wakikua waozeshwe katika familia watakazochaguliwa na wazazi wao. Pia kulikuwa na mila potofu nyingi kama ukeketaji na nyingine nyingi.

Lakini kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia katika karne hii mambo yamebadilika. Wanaharakati wengi wamepigania haki za Watoto wa kike na kupinga mila potofu kwa ajili ya ustawi wa jamii za kiafrika. Harakati nyingi zinaendelea na mwanamke amekombolewa kutoka kwenye giza.

Kwa sasa katika jamii nyingi watoto wakike wanapewa haki sawa na Watoto wakiume. Watoto wakike wanasoma mpaka kufika vyuo vikuu, wanaajiriwa sehemu mbalimbali, wanasikilizwa, wanahusika kutoa maamuzi katika familia zao, wanamiliki mali na wanawake wengi ni viongozi katika nchi zao. Kwa sasa kupitia vyombo vya Habari tunaona watu mbalimbali wanachukuliwa sheria kwa makosa ya unyanyasaji hasa kwa watoto wa kike. Nchi yetu inazidi kumpa mwanamke nafasi zaidi hata wale wanafunzi wakike walioacha shule kwa makosa kama ya kubeba mimba wanapiganiwa ili waweze kurudishwa shule.

Kwa hakika haya ni mambo ya kujivunia kwani kwa sasa jamii inaona faida ya kuwapa nafasi Watoto wakike.

Kwenye neema hakukosi kasoro, mwanamke kwa sasa anathaminiwa, swali la kujiuliza ni Je?mwanamke anaitambua thamani yake?. Waswahili wanasema ukibebwa bebeka. Si wanawake wote wanajithamini na kujiheshimu.

Katika ulimwengu huu wa utandawazi maadili yamevunjika, taarifa nyingi zipo hadharani hasa mitandaoni. Kuna baadhi ya watoto wakike wameanza kusahau maadili yetu na kusahau juhudi zinazofanywa za kumuinua mtoto wa kike.

Kuna baadhi ya wasichana ni wasomi na waelewa lakini ndio wakwanza kuvujisha picha zisizofaa na video chafu kwenye mitandao. Sikuhizi ukipitia mitandaoni picha za utupu ni kawaida hasa za Watoto wakike. Watoto wakike tusisahau kama teknolojia inaishi. Picha , video chafu na maandiko mabaya yanayowekwa mitandaoni yatadumu. Mkiwa wazazi wa badae mtaonekanaje? Wasichana wengi wanasahau juhudi zinazofanywa mpaka na wazazi wao za kujinyima ili wao wapate elimu bora kwa ajili ya kukomboa familia zao.

Mavazi ya ovyo pia sikuhizi kwa Watoto wa kike imekuwa kawaida. Kiasi kwamba mpaka kwenye vyombo vya usafiri vya jumuiya mpaka wakati mwingine ni aibu mpaka kutazama. Unywaji wa pombe kupitiliza, uvutaji bangi na madawa pia umeanza kuathiri Watoto wa kike. Kitu ambacho zamani hakikuwepo. Kuna msemo wa utani unasema Zamani Watoto wakike walijua kupika kama mama zao lakini siku hizi wanalewa kama baba zao. Tabia hii na nyingine mbaya inaleta fikra mbaya kuwa kuwasomesha Watoto wakike ni hasara na hakuna maana.

Pia kuna mimba za wanafunzi mabinti wakubwa ambao wameshapata elimu za uzazi, uwepo wa mimba nyingi mashuleni ni uthibitisho kuwa wasichana hawa elimu wanayoipata haiwasaidii.

Jamii inamtegemea mama kulea familia. Sikuzote wanawake bora hulea Watoto wema. Kama tabia wasichana hawatabadilika basi kizazi kijacho kipo hatarini kuangamia kabisa kwasababu yule mlezi ambaye jamii inamtegema akishakengeuka hakuna wakuokoa kizazi kijacho.

Wapendwa Watoto wakike tusitumie nafasi tulizopewa vibaya. Tusijiinue tukaona tu zaidi ya wanaume,nafasi ya mwanamme hata katika familia zetu itabaki palepale na sisi tutabaki kuwa wanawake.

Nataka kuwakumbusha mabinti ya kuwa mtu wa kwanza kuijua thamani yako ni WEWE MWENYEWE. Mtapewa nafasi nyingi kama hujakubali kujithamini, kujiheshimu na kutambua thamani yako basi nafasi mlizopewa hazitakuwa na maana. Tutaleta msiba kwenye jamii badala ya maendeleo. Mtawapa nafasi maadui zenu ambao ni jamii iliyowazunguka kuwa wasichana hawakutakiwa kupewa nafasi kwa sababu badala ya kuleta faida kwenye jamii wanaleta aibu.

Jiulize matatizo uliyoyapata wewe kama binti nani kayasababisha? ,utakuta baadhi ya matatizo chanzo ni wewe mwenyewe kwa kutokutambua thamani yako na kuamua kufuata njia mbaya. Kazi ya nyoka ni kung’ata, ni jukumu lako kumkwepa. Ni kweli mnakutana na vishawishi vingi lakini kumbukeni mna nguvu kuyakwepa makwazo yaliyo mbele yenu.

Tumia akili yako vyema, tambua wajibu wako na kusudi lako katika jamii. Yale ambayo unaweza kuyaepuka ni vyema kukaa nayo mbali. Si kila kitu cha kujaribu au kwa kutokufuata baadhi ya mambo ambayo yawezekana wenzako wengi katika kundi lako wanayafanya si vibaya kama tu hutendi kosa.

Wewe ni mama wa badae. Je Ungependa binti yako awe na tabia kama zako? Au ungependa kijana wako aoe binti mwenye tabia kama zako. Ukikuta unasita kuijibu nafsi yako basi ni wakati wa kubadilika na kuamua kujipa thamani.

Kwa msaada wa Imani zetu, Ukristo na Uislamu zote zinatufundisha maadili mema. Hivyo tumieni dini zenu ili kusimama imara.

MUNGU AWABARIKI SANA
 
Upvote 0
Back
Top Bottom