Watoto wasasa hawapati malezi ya wazazi kabisa.
Wapo hao wanaopelekwa boarding kwanzia wadogo na baada ya masomo ya sekondari wanakwenda Chuo. Huyu mtoto lazima kuna vitu vya kijamii, kitabia na kitamaduni mtabishana tu Kwasababu havikupandikizwa kichwani mwake. (Hapa ndipo wengi huibuka na kusema vijana wasasa hawaambiliki)
Ukiachana nahao kuna hawa wazazi pia ambao wanatafuta wadada wa kuwalelea watoto. Ukimuangalia mtu mwenyewe anaekwenda kulea mtoto bado anahitaji malezi.
Suala la uangalizi wa mtoto linahitaji ufatiliaji wa karibu kwenye ukuaji, mienendo, afya, tabia, lugha namengine mengi ambayo huyu muangalizi wala hayajui wala hana muda wa kuyafatilia.
Suala la malezi ya watoto kwanyakati hizi linaendeshwa hovyohovyo ndomana vijana wa sasa ni wahovyohovyo pia.