EWURA imetangaza bei mpya za Mafuta, Petroli, Dizeli, Mafuta ya Taa yashuka

EWURA imetangaza bei mpya za Mafuta, Petroli, Dizeli, Mafuta ya Taa yashuka

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Septemba 5, 2022 na Mkurungenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato bei za mafuta zimeonekana kupungua baada ya kupanda mfululizo kwa miezi mitano kuanzia Aprili mwaka huu.

Hadi leo katika mkoa wa Dar es Salaam bei ya petroli inaonesha inauzwa kwa Sh3, 410 kwa lita, dizeli Sh3, 322 na mafuta ya taa yakiuzwa Sh3,765 kwa lita.

Lakini kuanzia kesho Jumatano petroli itauzwa kwa Sh 2, 969, dizeli Sh3, 125 na mafuta ya taa yatauzwa Sh 3,335 bei hizi ni kwa mkoa wa Dar es Salaam baada ya ruzuku ya Serikali.

Kwa mujibu wa Lumato, kushuka kwa bei za bidhaa hizo kunatokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia ya mwezi Julai ambayo mafuta yanayotumika kuanzia kesho yamenunuliwa mwezi huo.

Ili kuendelea kupunguza athari za ongezeko la bei ya mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea Dizeli na pia kupunguza pengo kati ya bei ya Petroli na Dizeli, Serikali imetoa ruzuku ya Tsh. Bilioni 65 kwa bei ya mafuta ya Septemba 2022.

Kuingilia kati kwa Serikali na kutoa ruzuku hiyo kumepunguza bei ya bidhaa za Petroli kwa Septemba 2022 .

Jedwali hapa chini linaonesha Bei za Mafuta kabla na baada ya Ruzuku ya Serikali

1662483566251.png
 
Umendika kwa harakaa ka vile Tanesco wamekata umemee ukaona kiza na ku-post
 
Jioni hii nimetoka kuweka mafuta ya bei ya punguzo la TSH 180 pale kituo cha faya Kariakoo kuna bango limewekwa kubwa na magari yalikuwa foleni kuweka Kwa bei hiyo ya punguzo....

Hata hivyo kuanzia kesho angalau tutafuta machozi kwenye mafuta yaani kama bei imerudi Hadi 2960 MUNGU ni mwema
 
Na mtashukuru sasa kwa jinsi raia mlivyo wehu. Watu wanawachezea akili kwa kutumia pesa za kodi zetu na matozo ya kichawi then bado tunawashangilia.

Huu upumbavu tumalizane nao 2025. 2026 tuanze ukurasa mpya na chama kipya na katiba mpya.

Enough is enough with this garbage [emoji2781].
 
Serikali unachukua tozo kibao za mafuta ili bei ya mafuta iwe juu,
Halafu inatumia baadhi ya izo tozo Kama ruzuku kushusha kidogo Bei ya mafuta iliyopandishwa na tozo.

Tozo - Ruzuku = positive figure.
Hapa ndo tunapopigiwa
Ni kweli,jambo dogo kama hili wasomi wetu wameshindwa kufikiri, uwezo wa kuweka lita moja ya petrol iuzwe 2300 upo, hata kwenye mbs serikali ingekuwa organized wananchi tusingehangaika
 
Na mtashukuru sasa kwa jinsi raia mlivyo wehu. Watu wanawachezea akili kwa kutumia pesa za kodi zetu na matozo ya kichawi then bado tunawashangilia.


Huu upumbavu tumalizane nao 2025. 2026 tuanze ukurasa mpya na chama kipya na katiba mpya.

Enough is enough with this garbage [emoji2781].

Sent using Jamii Forums mobile app

Hiyo kumalizana nao kwa njia ya kura, labda kwa machafuko boss. Njia ya kura ni kupotezeana muda tu.
 
Mafuta yanatakiwa kuuzwa maximum tsh 2200. Kodi zimewekwa nyingi kwenye mafuta na bado huku mtaani wanakusanya tozo.

Halafu diesel inayobeba watu wa kipato cha chini na kuendesha mitambo haijashushwa.
 
Damu zetu zi juu yao na watoto wao
 
Back
Top Bottom