EWURA imetangaza bei mpya za Mafuta, Petroli, Dizeli, Mafuta ya Taa yashuka

EWURA imetangaza bei mpya za Mafuta, Petroli, Dizeli, Mafuta ya Taa yashuka

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Septemba 5, 2022 na Mkurungenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato bei za mafuta zimeonekana kupungua baada ya kupanda mfululizo kwa miezi mitano kuanzia Aprili mwaka huu.

Hadi leo katika mkoa wa Dar es Salaam bei ya petroli inaonesha inauzwa kwa Sh3, 410 kwa lita, dizeli Sh3, 322 na mafuta ya taa yakiuzwa Sh3,765 kwa lita.

Lakini kuanzia kesho Jumatano petroli itauzwa kwa Sh 2, 969, dizeli Sh3, 125 na mafuta ya taa yatauzwa Sh 3,335 bei hizi ni kwa mkoa wa Dar es Salaam baada ya ruzuku ya Serikali.

Kwa mujibu wa Lumato, kushuka kwa bei za bidhaa hizo kunatokana na kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia ya mwezi Julai ambayo mafuta yanayotumika kuanzia kesho yamenunuliwa mwezi huo.

Ili kuendelea kupunguza athari za ongezeko la bei ya mafuta nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea Dizeli na pia kupunguza pengo kati ya bei ya Petroli na Dizeli, Serikali imetoa ruzuku ya Tsh. Bilioni 65 kwa bei ya mafuta ya Septemba 2022.

Kuingilia kati kwa Serikali na kutoa ruzuku hiyo kumepunguza bei ya bidhaa za Petroli kwa Septemba 2022 .

Jedwali hapa chini linaonesha Bei za Mafuta kabla na baada ya Ruzuku ya Serikali

View attachment 2348019
shusha tena na nauli zishuke.
 
Soko la Dunia mafuta yameshuka sana mpaka jana yalikua 86usd kwa Barrel moja hii bei ilikua mwaka 2020 sidhani kwa kiwango ilichoshuka inawiana na bei waliyoshusha hao Ewura maana ilipanda kidogo ongezeko la mara ya mwisho ni 500 Tsh..Ewura wapo kwa ajili ya Wafanyabiashara na si walaji
 
JPM hasta siempreeeeeeeee
 
Back
Top Bottom