EWURA: Serikali imerekebisha tozo mbalimbali kwa taasisi zote zinazotoza tozo kwenye biashara ya mafuta hapa nchini

EWURA: Serikali imerekebisha tozo mbalimbali kwa taasisi zote zinazotoza tozo kwenye biashara ya mafuta hapa nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika kukabiliana na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia, Serikali imerekebisha tozo mbalimbali kwa taasisi zote zinazotoza tozo kwenye biashara ya mafuta hapa nchini.

Uamuzi huo ulifikiwa leo, tarehe 5 Oktoba 2021, baada ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuitisha kikao cha kujadiliana namna bora ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini na kuhakikisha kunakuwepo na utangamano wa hifadhi ya mafuta (security of supply), lakini pia kuwahakikishia wafanyabiashara wa mafuta hapa nchini wanafanya biashara katika na mazingira mazuri.

Baada ya maagizo hayo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatoa taarifa kwa umma juu ya tozo ambazo Serikali imepunguza kwa ajili ya kukabiliana na ongezeko kubwa la bei za mafuta hapa nchini kama ilivyoainishwa hapa chini:-

Serikali imebadilisha tozo ya matumizi ya miundombinu ya bandari (wharfage) ambayo inatozwa kwa dola za Marekani (USD 10/MT + VAT) kwa tani, na sasa itatozwa kwa shilingi ya Tanzania; na pia tozo hiyo imepunguzwa kufikia shilingi 15 kwa lita kutoka wastani wa shilingi 22 kwa lita na kuondoa VAT katika tozo hii. Hii ni kwa sababu sehemu ya tozo hii iliwekwa kwa ajili ya ujenzi wa boya la kupokelea mafuta baharini (Single Bouy Mooring - SBM) ambao kwa sasa umekamilika na hivyo kiasi cha shilingi 15 kwa lita kinachopendekezwa kinaweza kutumika kwa ajili ya matengenezo (maintenance). Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 23.15 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Serikali imepunguza tozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuchakata nyaraka (Customs processing fees) kutoka shilingi 4.8 kwa lita na kuwa kiwango maalumu cha shilingi milioni ishirini (20) kwa kila meli ambapo kwa wastani, meli 7 huleta shehena ya mafuta kila mwezi. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 14.79 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Serikalli imepunguza tozo ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kwa shilingi moja kwa lita na kuwa tozo ya kiwango maalumu ambacho ni shilingi milioni 7 kwa kila meli badala ya kutozwa kwa kila lita. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 2.85 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Serikali pia imepunguza tozo ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ya kupima ubora wa mafuta yanayoingizwa nchini kutoka shilingi 1.24 kwa lita na kutozwa kwa kiwango maalumu ambacho ni shilingi milioni 12.8 kwa kila meli. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 3.21 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Serikali imebadilisha mfumo wa utozaji wa tozo kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kutoka shilingi 3.54 kwa lita na kuwa tozo ya kiwango maalumu ambacho ni shilingi milioni 20 kwa kila meli. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 10.45 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Tozo kwa ajili ya shughuli za udhibiti za EWURA nazo zimepunguzwa kutoka wastani wa shilingi 5.54 kwa lita hadi shilingi 3.06 kwa lita. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 3.45 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Serikali pia imefuta tozo ya huduma (Service Levy) inayotozwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Halmashauri za Temeke na Kigamboni (Dar es Salaam), Tanga na Mtwara kwa wafanyabiasha wa jumla ambao wana maghala ya kuhifadhia mafuta ya jumla. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 19.82 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Pia, Serikali imepunguza gharama za kuweka vinasaba kwenye mafuta kutoka shilingi 14 kwa lita hadi shilingi 7 kwa lita. Mabadiliko haya yataleta nafuu kwa watumiaji mafuta kwa wastani wa shilingi bilioni 23.92 kwa mwaka kutokana na matumizi ya lita bilioni 3.42 kwa takwimu za mwaka 2020.

Kiujumla marekebisho haya yatawanufaisha Watanzania kwa kupunguza matumizi ya fedha kwenye manunuzi ya mafuta kwa shilingi bilioni 102. Mfano, bei za petroli kwa Dar es Salaam kuanzia tarehe 6 Oktoba 2021 zilitakiwa ziongezeke kwa shilingi 145 kwa lita lakini kwa hatua zilizochukuliwa na Serikali, bei hizo zimeongezeka kwa shilingi 12 kwa lita.

Kutokana na hatua hizi bei za mafuta kuanzia kesho Jumatano ya Tarehe 6 Oktoba 2021 zinakuwa kama ifuatavyo:-

BEI ZA REJA REJA ZA MAFUTA KUANZIA TAREHE 6 OKTOBA 2021

MJI
BEI KIKOMO
PetrolI
(TZS/Lita)
Dizeli
(TZS/Lita)
Mafuta ya Taa
(TZS/Lita)
Dar es Salaam
2,439
2,261
2,188
Arusha
2,535
2,301
2,272
Arumeru (Usa River)
2,535​
2,301​
2,272​
Karatu
2,553​
2,320​
2,290​
Longido
2,546​
2,312​
2,283​
Monduli
2,540​
2,307​
2,277​
Monduli-Makuyuni
2,545​
2,311​
2,282​
Ngorongoro (Loliondo)
2,619​
2,386​
2,363​
Pwani (Kibaha)
2,443
2,266
2,192
Bagamoyo
2,450​
2,272​
2,199​
Bagamoyo (Miono)
2,480​
2,303​
2,229​
Chalinze Junction
2,453​
2,275​
2,202​
Chalinze Township (Msata)
2,457​
2,279​
2,206​
Kibiti
2,459​
2,281​
2,208​
Kisarawe
2,446​
2,268​
2,195​
Mkuranga
2,448​
2,271​
2,197​
Rufiji
2,466​
2,289​
2,215​
Dodoma
2,497
2,320
2,246
Bahi
2,505​
2,327​
2,254​
Chamwino
2,493​
2,315​
2,242​
Chemba
2,524​
2,346​
2,273​
Kondoa
2,530​
2,353​
2,279​
Kongwa
2,495​
2,317​
2,244​
Mpwapwa
2,498​
2,321​
2,247​
Mpwapwa (Chipogoro)
2,510​
2,333​
2,259​
Mtera (Makatopora)
2,516​
2,339​
2,265​
Mvumi
2,504​
2,326​
2,253​
Geita
2,604
2,427
2,353
Bukombe
2,593​
2,415​
2,342​
Chato
2,625​
2,448​
2,374​
Mbogwe
2,642​
2,465​
2,391​
Nyang'hwale
2,619​
2,442​
2,368​
Iringa
2,503​
2,325​
2,252​
Ismani
2,508​
2,330​
2,257​
Kilolo
2,507​
2,330​
2,256​
Mufindi (Mafinga)
2,513​
2,335​
2,262​
Mufindi (Igowole)
2,521​
2,344​
2,270​
Kagera (Bukoba)
2,654
2,477
2,403
Biharamulo
2,628​
2,451​
2,377​
Karagwe (Kayanga)
2,670​
2,493​
2,420​
Kyerwa (Ruberwa)
2,676​
2,499​
2,425​
Muleba
2,654​
2,477​
2,403​
Ngara
2,642​
2,464​
2,391​
Misenyi
2,663​
2,485​
2,412​
Katavi (Mpanda)
2,647
2,469
2,396
Mlele (Inyonga)
2,666​
2,488​
2,415​
Mpimbwe (Majimoto)
2,639​
2,462​
2,389​
Tanganyika (Ikola)
2,664​
2,487​
2,413​
Kigoma
2,670
2,493
2,419
Uvinza (Lugufu)
2,682​
2,505​
2,431​
Buhigwe
2,659​
2,482​
2,408​
Kakonko
2,627​
2,450​
2,376​
Kasulu
2,656​
2,479​
2,405​
Kibondo
2,634​
2,457​
2,383​
Kilimanjaro (Moshi)
2,524
2,291
2,261
Hai (Bomang'ombe)
2,528​
2,294​
2,265​
Mwanga
2,517​
2,284​
2,254​
Rombo (Mkuu)
2,541​
2,308​
2,282​
Same
2,511​
2,277​
2,248​
Siha (Sanya Juu)
2,531​
2,298​
2,268​
Lindi
2,468
2,293
2,246
Lindi-Mtama
2,473​
2,297​
2,265​
Kilwa Masoko
2,492​
2,317​
2,221​
Liwale
2,504​
2,328​
2,267​
Nachingwea
2,488​
2,313​
2,276​
Ruangwa
2,494​
2,319​
2,277​
Manyara (Babati)
2,569
2,335
2,310
Hanang (Katesh)
2,579​
2,346​
2,321​
Kiteto (Kibaya)
2,584​
2,351​
2,321​
Mbulu
2,582​
2,348​
2,323​
Simanjiro (Orkasumet)
2,601​
2,368​
2,342​
Mara (Musoma)
2,617
2,440
2,366
Musoma Vijijini (Busekela)
2,658​
2,480​
2,407​
Rorya (Ingirijuu)
2,626​
2,449​
2,375​
Rorya (Shirati)
2,661​
2,483​
2,410​
Bunda
2,608​
2,431​
2,357​
Bunda (Kisorya)
2,618​
2,440​
2,367​
Butiama
2,614​
2,437​
2,363​
Serengeti (Mugumu)
2,663​
2,485​
2,412​
Tarime
2,628​
2,451​
2,377​
Tarime (Kewanja/Nyamongo)
2,633​
2,455​
2,382​
Mbeya
2,546
2,368
2,295
Chunya
2,555​
2,378​
2,304​
Chunya (Makongolosi)
2,560​
2,383​
2,310​
Chunya (Lupa Tingatinga)
2,562​
2,385​
2,311​
Kyela
2,561​
2,384​
2,310​
Mbarali (Rujewa)
2,530​
2,352​
2,279​
Rujewa (Madibira)
2,543​
2,366​
2,292​
Rujewa (Kapunga)
2,540​
2,362​
2,289​
Rungwe (Tukuyu)
2,555​
2,377​
2,304​
Morogoro
2,464
2,286
2,213
Mikumi
2,479​
2,302​
2,228​
Kilombero (Ifakara)
2,501​
2,324​
2,250​
Kilombero (Mlimba)
2,524​
2,346​
2,273​
Kilombero (Mngeta)
2,513​
2,335​
2,262​
Ulanga (Mahenge)
2,512​
2,335​
2,261​
Malinyi
2,522​
2,345​
2,271​
Kilosa
2,482​
2,304​
2,231​
Gairo
2,482​
2,304​
2,231​
Mvomero (Wami Sokoine)
2,474​
2,297​
2,223​
Mvomero (Sanga Sanga)
2,464​
2,286​
2,213​
Turian
2,489​
2,311​
2,238​
Mtwara
2,455
2,279
2,260
Nanyumbu (Mangaka)
2,491​
2,316​
2,309​
Masasi
2,471​
2,295​
2,286​
Newala
2,476​
2,300​
2,292​
Tandahimba
2,469​
2,293​
2,285​
Nanyamba
2,469​
2,293​
2,285​
Mwanza
2,589
2,411
2,338
Kwimba
2,607​
2,429​
2,356​
Magu
2,597​
2,419​
2,346​
Misungwi
2,583​
2,406​
2,332​
Sengerema
2,621​
2,444​
2,370​
Ukerewe
2,648​
2,471​
2,397​
Njombe
2,531
2,354
2,280
Njombe (Kidegembye)
2,552​
2,374​
2,301​
Ludewa
2,569​
2,391​
2,318​
Makambako
2,523​
2,346​
2,272​
Makete
2,562​
2,384​
2,311​
Wanging'ombe (Igwachanya)
2,529​
2,351​
2,278​
Rukwa (Sumbawanga)
2,612
2,434
2,361
Sumbawanga Rural (Mtowisa)
2,612​
2,434​
2,361​
Kalambo (Matai)
2,619​
2,441​
2,368​
Nkasi (Namanyele)
2,625​
2,448​
2,374​
Ruvuma (Songea)
2,540
2,365
2,311
Mbinga
2,553​
2,377​
2,345​
Namtumbo
2,531​
2,356​
2,340​
Nyasa (Mbamba Bay)
2,578​
2,403​
2,355​
Tunduru
2,505​
2,330​
2,370​
Shinyanga
2,568
2,390
2,317
Kahama
2,581​
2,404​
2,330​
Kishapu
2,596​
2,418​
2,345​
Ushetu (Nyamilangano)
2,599​
2,421​
2,348​
Ushetu (Kangeme Village)
2,589​
2,412​
2,338​
Salawe
2,582​
2,405​
2,331​
Simiyu (Bariadi)
2,609
2,432
2,358
Busega (Nyashimo)
2,602​
2,424​
2,351​
Itilima (Lagangabilili)
2,612​
2,435​
2,361​
Maswa
2,600​
2,423​
2,349​
Meatu (Mwanhuzi)
2,607​
2,430​
2,356​
Singida
2,529
2,352
2,278
Iramba
2,541​
2,364​
2,290​
Manyoni
2,514​
2,336​
2,263​
Itigi (Mitundu)
2,529​
2,352​
2,278​
Ikungi
2,525​
2,347​
2,274​
Mkalama (Nduguti)
2,554​
2,376​
2,303​
Songwe (Vwawa)
2,555
2,377
2,304
Songwe (Mkwajuni)
2,562​
2,384​
2,311​
Ileje
2,559​
2,381​
2,308​
Momba (Chitete)
2,564​
2,387​
2,313​
Tunduma
2,559​
2,382​
2,308​
Tabora
2,547
2,369
2,296
Igunga
2,547​
2,369​
2,296​
Kaliua
2,560​
2,382​
2,309​
Ulyankulu
2,557​
2,380​
2,306​
Nzega
2,557​
2,380​
2,306​
Sikonge
2,556​
2,378​
2,305​
Urambo
2,557​
2,379​
2,306​
Uyui
2,553​
2,376​
2,302​
Mpyagula
2,578​
2,401​
2,327​
Tanga
2,478
2,245
2,234
Handeni
2,499​
2,265​
2,213​
Kilindi
2,514​
2,280​
2,248​
Korogwe
2,490​
2,257​
2,227​
Lushoto
2,500​
2,266​
2,236​
Mkinga (Maramba)
2,485​
2,252​
2,248​
Muheza
2,483​
2,250​
2,234​
Pangani
2,485​
2,251​
2,240​
BEI ZA JUMLA

Petroli (TZS/Lita)
Dizeli (TZS/Lita)
Mafuta ya Taa (TZS/Lita)
DAR ES SALAAM
2,308.90​
2,131.57​
2,058.93​
TANGA
2,348.33​
2,115.34​
MTWARA
2,324.95​
2,149.78​






Mha. Godfrey H. Chibulunje

KAIMU MKURUGENZI MKUU

EWURA

TAREHE 5 OKTOBA 2021
 

Attachments

Duh yakipanda tena wataondoa tozo au?
 
Kuna tozo za Taasisi za Serikali, ambazo kimsingi hutoa huduma ambayo ni ya udhibiti, zingefutwa kabisa, kama ifuatavyo:
1) Tozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuchakata nyaraka (Customs processing fees)
2) Tozo ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA)
3) Tozo kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)
4) Tozo kwa ajili ya shughuli za udhibiti za EWURA
 
Duuu tozo zaidi ya 10 .Aiseee mlolongo ni mrefu kwa kweli kwa lita moja ya shs 2400/= tozo labda ni almost 40% ya bei
 
Nilitegenea huu upuuzu. Tukisema watendaji hamsikilizi maamuzi ya Rais, Siro na vijana wake mna kamata watu. Does it make sense kwamba mneagizwa bei za mafuta zishuke lakini nyie mmeongeza 2/-? Are you serious?

Tukisema mnadharau maagizo ya Rais tutakuwa tuna kosea?? Mwigulu ni tatizo.. Mh Rais muangalie huyu jamaa kwa jicho la pili. Bado huyu huja msoma.
 
Hivi mbona sioni mafuta ya kula??? Au nchi yetu ilishapiga marufuku mafta ya kula kuagizwa😀😀😀
 
Kuna tozo za Taasisi za Serikali, ambazo kimsingi hutoa huduma ambayo ni ya udhibiti, zingefutwa kabisa, kama ifuatavyo:
1) Tozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuchakata nyaraka (Customs processing fees)
2) Tozo ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA)
3) Tozo kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)
4) Tozo kwa ajili ya shughuli za udhibiti za EWURA
Sasa zikifutwa hizo huduma zitatolewa na nani au unatakaka wafanyabiashara wafanye fujoo
 
Pamoja na tozo zote kupunguzwa lakn Bado bei imepanda kwa tsh 12
 
Huu unafuu uko wapi?

Mimi mpaka sasa bado najiuliza ni kitu gani kilisababisha nishati ya mafuta ya diesel, super/petrol na taa kupanda kwa supersonic speed mara baada ya kifo cha Magufuli katika miezi 4 au 5 tu kwa kiasi cha wastani wa Tsh. 500/litre?

NDIYO. Magufuli amekufa mwezi March, 2021 bei ya nishati ya petrol [reja raja] ilikuwa ni ya wastani wa Tsh. 2,000/= nchini kote...

Lakini kuanzia April - July bei ikaongezeka ghafla kwa wastani wa kati 250 - 400 na sasa huu ni mwezi oktoba ongezeko ni karibu Tsh. 650/litre nchini kote!

Why?
 
Huu unafuu uko wapi?

Mimi mpaka sasa bado najiuliza ni kitu gani kilisababisha nishati ya mafuta ya diesel, super/petrol na taa kupanda kwa supersonic speed mara baada ya kifo cha Magufuli katika miezi 4 au 5 tu kwa kiasi cha wastani wa Tsh. 500/litre..?

NDIYO. Magufuli amekufa mwezi March, 2021 bei ya nishati ya petrol [reja raja] ilikuwa ni ya wastani wa Tsh. 2,000/= nchini kote...

Lakini kuanzia April - July bei ikaongezeka ghafla kwa wastani wa kati 250 - 400 na sasa huu ni mwezi oktoba ongezeko ni karibu Tsh. 650/litre nchini kote.....!

Why..????
Wajanja wamerudi kwenye usukani.
Mama haelewi game wanacheza naye kwenye makaratasi
 
hivi zile nfasi walizotoa washaita watu kwa interview?
 
Huu unafuu uko wapi?

Mimi mpaka sasa bado najiuliza ni kitu gani kilisababisha nishati ya mafuta ya diesel, super/petrol na taa kupanda kwa supersonic speed mara baada ya kifo cha Magufuli katika miezi 4 au 5 tu kwa kiasi cha wastani wa Tsh. 500/litre..?

NDIYO. Magufuli amekufa mwezi March, 2021 bei ya nishati ya petrol [reja raja] ilikuwa ni ya wastani wa Tsh. 2,000/= nchini kote...

Lakini kuanzia April - July bei ikaongezeka ghafla kwa wastani wa kati 250 - 400 na sasa huu ni mwezi oktoba ongezeko ni karibu Tsh. 650/litre nchini kote.....!

Why..????
Acha fix
 
Sasa zikifutwa hizo huduma zitatolewa na nani au unatakaka wafanyabiashara wafanye fujoo
Ni wajibu wa Serikali kudhibiti, hivyo igharamie huduma hizo, kwa jinsi ile ile Wizara zifanyavyo kazi. La, huduma hizo zirudishwe kwenye Wizara na kuunda Idara.

Ikiwa kila Taasisi ya udhibiti km kuna TARURA na TANROADS zikiwekewa tozo, hali itakuwaje?
 
Back
Top Bottom