EWURA: Serikali imerekebisha tozo mbalimbali kwa taasisi zote zinazotoza tozo kwenye biashara ya mafuta hapa nchini

EWURA: Serikali imerekebisha tozo mbalimbali kwa taasisi zote zinazotoza tozo kwenye biashara ya mafuta hapa nchini

Eeehh mbona yamepanda? Jamani, nilijua mafuta yatashuka kidogo, mmmhh, kuna tatizo mahali, aisee
 
Kuna tozo za Taasisi za Serikali, ambazo kimsingi hutoa huduma ambayo ni ya udhibiti, zingefutwa kabisa, kama ifuatavyo:
1) Tozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuchakata nyaraka (Customs processing fees)
2) Tozo ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA)
3) Tozo kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)
4) Tozo kwa ajili ya shughuli za udhibiti za EWURA
You are very right, vinginevyo kilichofanyika ni ujinga mtu. Hivi Euwra anachukua fedha zote hizo za nini wakati hawezi kudhibiti chochote!
 
Bora ingekuwa hata 2000 kamili ingetosha lakini kwa bei hii mpya nadhani hakuna mabadiliko yeyote
 
Ujinga mtupu,wanatuwekea matozo kibao sijui imepunguzwa kutoka ngapi hadi ngapi halafu bado mafuta yanapanda sasa sisi inatusaidia nini?

Kwahio sasa hapo serikali ilitegemea tuipongeze sio? ni vichekesho tu
 
Upuuz mtupu huu ..Sasa hi taaruki wailoileta kwa wananchi inasaidia nn baada ya kusikiaaimeshuka nikaanza kuaanda bajeti ya kutengeneza gari langu
 
Ndio matatizo ya kuanzisha taasisi ambazo ni ‘cost centres’ kwa serikali matokeo yake kujiendesha inabidi wabuni tozo.

90% ya majukumu yote yanayo fanywa na taasisi mbali mbali yanawezwa fanya na EWURA pekee, ukitoa machache kama upkeep ya miundombinu ili kupunguza idadi ya tozo.

Halafu waache kutumia terminalogies out of context, ‘security of supply’ measures means kuhakikisha mafuta ayakauki nchini not so much kupanda kwa bei.

Mwezi June tu tuliona upungufu wa mafuta kisa yanaponunuliwa refinery awakutegemea a surge demand, ni tatizo la muda mfupi kwao ila kwetu lilileta shida ambazo wahusika awafuati ushauri wa ‘International Energy Agency’. Kila nchi inatakiwa iwe na miundombinu ya kutunza mafuta kwa miezi mitatu (minimum) sisi hatuna ya kutunza ata kwa mwezi mzima.

Matokeo yake tatizo dogo la kama week mbili mzalishaji kujirekebisha, lilileta shida kubwa Tanzania ndani ya mwezi.

Kasheshe sasa point of entry can be accessed na mafisadi watu wanatoa mafuta nyumba ya jirani halafu unazumgumza mambo ya ‘security of supply’, sasa kama watu wana fikia sensitive infrastructure kama hiyo wakililipua kuna madhara gani kwenye uchumi.

Hayo ndio mambo ya kuja JF unaokota terminologies na kuzitumia bila ya kuelewa what exactly they imply.
 
Yaani nikajua wese litashuka hadi 1800tshs hivi
 
IMG_0151.jpg

Huo ni mfano wa utitiri wa kodi kwenye kila lita ya mafuta. Nchi hii inachezewa sana na sisiyemu na wanatumia kama mtaji kunufaisha chama chao. Nchi jirani mafuta ni bei nafuu
 
Huu unafuu uko wapi?

Mimi mpaka sasa bado najiuliza ni kitu gani kilisababisha nishati ya mafuta ya diesel, super/petrol na taa kupanda kwa supersonic speed mara baada ya kifo cha Magufuli katika miezi 4 au 5 tu kwa kiasi cha wastani wa Tsh. 500/litre..?

NDIYO. Magufuli amekufa mwezi March, 2021 bei ya nishati ya petrol [reja raja] ilikuwa ni ya wastani wa Tsh. 2,000/= nchini kote...

Lakini kuanzia April - July bei ikaongezeka ghafla kwa wastani wa kati 250 - 400 na sasa huu ni mwezi oktoba ongezeko ni karibu Tsh. 650/litre nchini kote.....!

Why..????
Mnajifanya mna data lakini kwenye soko la dunia hamujui nini kinaendelea.
 
Tuihoji ewura,?
Ina wafanyakazi wangapi?
Wana elimu gani?
Vigezo vya ajira yao ikoje?

Mishahara yao ipoje?

Kwa makusanyo hayo mapya ni karibu 10 bil.je wanaifanyia nini hii yote?
Je haiwezekani wakarudishwa serikalini na kulipwa kama grade za serikali?
 
Mnajifanya mna data lakini kwenye soko la dunia hamujui nini kinaendelea.
Wewe unayeelewa kwani kuna ubaya gani ukieleza nini kinaendelea?

Hivi ni kwanini watu wengine mnakuwa wajinga kiasi cha kutoelewa hata maana ya mjadala...???

NARUDIA TENA: Eleza unachokielewa wewe kunachoendelea huko SOKO LA DUNIA au la kaa kimya wasome wengine!!!
 
Uku kwetu mwaka huu mafuta yalifika adi 1500/L, dah bodaboda walifurahi kinoma. Doh ile bei ilidumu ndani ya siku 6 tu mara ikaanza tena kupanda ad ikafika apa ilipo.
 
Jukumu la urais ni zito sana, maybe uyu mama hajui yupo nchini kama nani,. Uyu mama dhaifu sana hayajui majukumu yake kama rais...
 
Kuna tozo za Taasisi za Serikali, ambazo kimsingi hutoa huduma ambayo ni ya udhibiti, zingefutwa kabisa, kama ifuatavyo:
1) Tozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kuchakata nyaraka (Customs processing fees)
2) Tozo ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA)
3) Tozo kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)
4) Tozo kwa ajili ya shughuli za udhibiti za EWURA
Mkuu nimemsikia Prof Ngowi wa Mzumbe University akihojiwa na Azam anasema kwa jumla kuna tozo 16 ambazo hufanya bei ya mafuta kuwa mara mbili ya bei yake halisi yanapoingia bandarini (ambapo bei ikiwa na CIF ni kama sh 1100 hivi). Ina maana kusingekuwa na huu utitiri wa hizi tozo pengine mafuta yangekuwa sh 1500 kwa lita kama huko Zambia na kwingineko.
 
[emoji1787] [emoji1787] Hii nchi vituko haviishi Tozo zimepunguzwa alafu hapo hapo Bei ya mafuta imepandishwa kwa sh. 12
Nchi ya mazuzu!!hii, hangaisha bwege!!hili uishi na bwege vizuri Unatengeneza tatizo watu wanapiga kelele, unajifanya tena kuwa umelitatua ki ujanja ujanja, tayari bwege analizika.
 
Mkuu nimemsikia Prof Ngowi wa Mzumbe University akihojiwa na Azam anasema kwa jumla kuna tozo 16 ambazo hufanya bei ya mafuta kuwa mara mbili ya bei yake halisi yanapoingia bandarini (ambapo bei ikiwa na CIF ni kama sh 1100 hivi). Ina maana kusingekuwa na huu utitiri wa hizi tozo pengine mafuta yangekuwa sh 1500 kwa lita kama huko Zambia na kwingineko.
Sio mafuta tuu ni kila kitu,fungua kiwanda utafunga kabla ya kuanza uzalishaji au utaishia kuwa mpiga deal tuu kama wahindi, kodi zinaua maendeleo Tanzania na sijui kwanini viongozi hawalioni hilo, fanya research ya biashara ya Hotel Tanzania hautaamini utakachokutana nacho kwenye kodi
 
[emoji1787] [emoji1787] Hii nchi vituko haviishi Tozo zimepunguzwa alafu hapo hapo Bei ya mafuta imepandishwa kwa sh. 12
Nimenunua mafuta kwa shilingi 2,373 Lake Oil jana Morogoro sasa sijaelewa haya mazingaombwe yanavyofanyika, kwamba tozo zimepungua
 
Back
Top Bottom