EWURA yatangaza bei Kikomo za mafuta ya petroli zitakazotumika kuanzia Novemba 6, 2024, saa 6:01 usiku

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
KUMB: PPR/2024-11/01
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 6 NOVEMBA 2024
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano ya tarehe 6 Novemba 2024 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Novemba 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia Jedwali 1: Bei Kikomo za Rejareja (Shilingi Lita)






PIA SOMA
- EWURA yatangaza Bei Kikomo za Mafuta kwa Mwezi Agosti, yamepanda tena
 
Kuna bei za OPEC halafu kuna bei za TPA. Huwezi kuelewa kama huna D mbili😁

Hapo naanza kuhisi BRICS ina manufaa flani upande wa Nishati.
Vita ya Ukraine ikiisha najua mafuta yatashuka bei kama maji,vile vikwazo ya uchumi vikifunguliwa tutapata faida kubwa hasa Kwa nchi za Africa
 
Mkuu @LATRA mtushushie nauli za mabasi Asee mafuta yameshuka
 
Bei zikipanda haraka sana wadau hupandisha bei za bidhaa au huduma zao mfano nauli. Ila bei za mafuta zikishuka wadau walewale wanakuwa kimyaaaaaa...
 
Tukiachana na ubathirifu na ufisadi dizel na petrol inaweza kuuzwa 2,000/= kwa lita na kwa faida kabisa na kwa kufanya hivyo itasaidia kushusha gharama za usafirishaji na kuinua uchumi wa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…