EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta, Petroli na Dizeli bei yapanda kuanzia Aprili 3, 2024

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta, Petroli na Dizeli bei yapanda kuanzia Aprili 3, 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo ya mafuta zilizoanza kutumika leo Aprili 3, 2024 ambapo kuna ongezeko la bei ya nishati za Petroli na Dizeli huku Mafuta ya Taa bei ikibaki kama ilivyokuwa Machi 2024.

Upande wa Dar es Salaam bei ya Petroli ni Tsh 3,257 ikiwa ni ongezeko la Tsh 94, Dizeli ni Tsh. 3,210 kuna ongezeko la Tsh. 84, Mafuta ya Taa bei ni Tsh. 2,840 sawa na ilivyokuwa mwezi uliopita.

Baadhi ya sababu zilizotajwa na EWURA kuchangia mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la Dunia kwa wastani wa 3.94% kwa Petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya Dizeli, kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kwa 3.19% kutokana na ongezeko la matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa.

Snapinsta.app_434755144_18003577694448430_3965863413850170261_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434759607_18003577703448430_4628624481358424397_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434771302_18003577718448430_3590069934400772263_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434403073_18003577721448430_8487461925216309638_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434757807_18003577730448430_8088428897526966752_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434763803_18003577739448430_3687619561893758444_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434404649_18003577748448430_5980745173819346193_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434722367_18003577757448430_1134368585674837338_n_1080.jpg

 

Attachments

  • Snapinsta.app_434771302_18003577718448430_3590069934400772263_n_1080.jpg
    Snapinsta.app_434771302_18003577718448430_3590069934400772263_n_1080.jpg
    176.2 KB · Views: 9
Daah Ewura kila tangazo lao limeegemea kwa Wafanyabiashara tu kazi ipo yakishuka yanashuka mia moja yakipanda ni zaidi ya ilichoshuka. Waliwahi pandisha Tsh 500 baadae wakashusha Tsh 75 huku soko la Dunia bei ikiwa imeshuka sana.
 
Daah Ewura kila tangazo lao limeegemea kwa Wafanyabiashara tu kazi ipo yakishuka yanashuka mia moja yakipanda ni zaidi ya ilichoshuka...waliwahi pandisha Tsh 500 baadae wakashusha Tsh 75 huku soko la Dunia bei ikiwa imeshuka sana..
Upatikanaji wa dollar nao ni changamoto
 
Kwanini petrol inakuwa ghali kuliko diesel?
Tofauti na nchi zingine ambapo diesel ndio inatumika kwenye biashara zaidi na petrol anasa?
Sisi huwa akili zetu tunazijua wenyewe
 
Back
Top Bottom