EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta, Petroli na Dizeli bei yapanda kuanzia Aprili 3, 2024

EWURA yatangaza bei mpya ya mafuta, Petroli na Dizeli bei yapanda kuanzia Aprili 3, 2024

Upatikanaji wa dollar nao ni changamoto
Dollar Ndo sababu ya msingi sana inayofanya mafuta yapande?
Huenda ikawa ndivyo,lakini tuombe kwa Serikali iwe na huruma .
Kuliibuka kwa Ruzuku ya Mama Samia kwenye mafuta,Je! Wenye nayo waliichumua amma?
Tanzania inaharibiwa na wachache sasa
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo ya mafuta zilizoanza kutumika leo Aprili 3, 2024 ambapo kuna ongezeko la bei ya nishati za Petroli na Dizeli huku Mafuta ya Taa bei ikibaki kama ilivyokuwa Machi 2024.

Upande wa Dar es Salaam bei ya Petroli ni Tsh 3,257 ikiwa ni ongezeko la Tsh 94, Dizeli ni Tsh. 3,210 kuna ongezeko la Tsh. 84, Mafuta ya Taa bei ni Tsh. 2,840 sawa na ilivyokuwa mwezi uliopita.

Baadhi ya sababu zilizotajwa na EWURA kuchangia mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la Dunia kwa wastani wa 3.94% kwa Petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya Dizeli, kuongezeka kwa kiwango cha kubadilishia fedha za kigeni kwa 3.19% kutokana na ongezeko la matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa.

Huu nao sio utapeli wa ccm? Ni lazima bei zipande kila mwezi? Mwisho wake ni wapi?!!
 
hayupo wa kuzuia ongezeko au anguko la bei ya mafuta duniani. Soko la mafuta duniani hujiendesha lenyewe kulingana na uzalishaji, upatikanaji wa bidhaa yenyewe kwa wakati huo, gharama za usafirishaji, ongezeko la gharama za ubadilishaji fedha hususani dola ya Marekani na kuongezeka kwa matumizi ya EURO kulipia mafuta yaliyoagizwa, kama ambavyo EWURA wamebainisha 🐒🐒

sasa hapo anajitokeza mtu, oohh fulani haifai, sijui nini nani. huyo asie faa alikuako huko kwenye kwenye mafuta na hizo bei🐒

kulalamika ni mazoea tu hata kama bei ingeshuka bado malalamiko yangekuepo 🐒

so,
hiyo ni kawaaida hususani hapa Tz, na hakuna namna ingine, tunakwendra nayo hivyo hivyo, maana saa zingine hakuna jema kwa mwanadamu 🐒
 
Hili nalo mkalitazame, alisikika mkazi mmoja wa kizimkazi mwenye macho legevu!!.
 
Lusaka petrol ni K31 = TZS 3155. Diesel ni K28 = TZS 2850.
Wachumi watuweke sawa juu ya hili.
 
Daah Ewura kila tangazo lao limeegemea kwa Wafanyabiashara tu kazi ipo yakishuka yanashuka mia moja yakipanda ni zaidi ya ilichoshuka...waliwahi pandisha Tsh 500 baadae wakashusha Tsh 75 huku soko la Dunia bei ikiwa imeshuka sana..
Ona kitu
Kwani unakisima cha mafuta ndugu🤔
Mafuta hata ikifika lita 10000 wabongo furesh tu mbona,kwani wamelalamika mbona muda wote tunawaona na kuwasikia wakishukuru na kutoa asante kwa mama

Ova
 
Ona kitu

Mafuta hata ikifika lita 10000 wabongo furesh tu mbona,kwani wamelalamika mbona muda wote tunawaona na kuwasikia wakishukuru na kutoa asante kwa mama

Ova
Ewura wana kiwango cha bei wanataka ifike hii mambo wanayoenda nayo haipo soko la Dunia mafuta yakishuka huko huku wanatangaza shilingi 30 ila kupanda huwa inapanda mamia na cents zake hao jamaa wapo kwa ajili ya watu wachache ambao ndio wanahusika na hii biashara ya mafuta juzi nimeshangaa nimeenda kituo kimoja mashine zao zote huwa zinakua busy ila siku tatu nyuma wakawa wanatumia mashine moja leo asubuhi baada ya kupanda hiyo bei waliyoambiwa itapanda mashine zote zipo na wafanyakazi na mafuta yanauzwa tena..
 
Ndiyo maana siku hizi vituo vya kuuzia mafuta vinajengwa mpaka kwenye makazi ya watu! Yaani vimetapakaa kila kona! Maana wanajua vinalipa.

Kwa hali hii twafa!! Na hapo tulipigwa porojo eti kila mwezi kuna bilioni 100 zinatumika kama ruzuku kwenye hayo mafuta!! Aisee wahuni siyo watu poa hata kidogo.
 
Tunamshukuru mama kwa kupanda bei ya mafuta hakika anaupiga mwingi.
 
Back
Top Bottom