Ex wangu nampenda ila kampa mimba mwanamke mwingine

Ex wangu nampenda ila kampa mimba mwanamke mwingine

Kuweka mawasiliano na ukaribu na x ni sawa na kutembea na muwa kama mkongoja wako, mwisho utakua,haya sasa amua uendelee kua Mua ama utupe pingili na maganda yake usonge mbele!!
 
Sasa Kazaa na huyo anataka azae na mimi tena mpk sasa hajui nani anamuoa… huwezi kuwa seriously sizani Kama ningekuwa ndugu yako ungenishauri hivi
Anataka kuzaa na wewe huo ni uamzi wake hakuna kesi wal sheria inabana, wewe unashindwa nini kusema hutaki na mahusiano yaishe mpaka unalalama tu hapa umeshikiwa fimbo.

Wanawake munapenda mpaka kupangiwa maamuzi hayo maamuzi yake mwanaume wewe fanya yako.
 
Mambo flani flani kazini kwake, kwani ni mwanajeshi hajamaliza mkataba?

Halafu thread yako yote hii haujasema ulitaka nini katika mahusiano yenu hadi akakuona wewe ni mpuuzi akatafuta mwanamke mwingine?

Kuzaa unasema bado wewe mdogo, mwenzako alikuweka wazi kuwa umri wa kuzaa tayari na anataka mzae, wewe hukutaka na haukuweka wazi kwa mwenzako umri ambao ulitaka uanze kuzaa.

Mwenzako alikuona misimamo na malengo yenu haviendani ndiyo maana akatafuta mtu wanayeendana naye.

Kusema anaendelea kukupenda yawezekana anasema ukweli.

Chemistry ya kiume inaruhusu kupenda mwanamke zaidi ya mmoja na maisha yakasonga.

Sasa kuwa mke wake wa pili, maana sifa za kuwa mke wake wa kipekee uliipoteza.

Siwezi kukushauri vinginevyo mama, maana penzi la watu huwa halivunjwi na wapambe bali huvunjwa na wao wenyewe.

Sawa dear tutazaa akimaliza ujana nitakuwa mke wa 7
 
Yaani mwanamke miaka 23 unajiona mdogo kuzaa?
Mwanamke umri ukishafika miaka 21 tu ujue soko lako litaporomoka kila uchwao maana hapo unakimbilia kwenye 30's ambapo ni mshangazi tayari.

Usiniponze mimi nikajiona Mzee nikavaa kila dume… watu wanaolewa mpk Miaka 40 sembuse mimi mtoto wa jana

Unataka nizae na mtu ambayo yeye wenyewe ana Miaka 23 hajajielewa anataka nini kisa et ananipenda ama umri umefika unajua kama umri huo nilikuwa masomoni kwaiyo niache kusoma nibebe mimba kisa kuogopa kuwa shangazi
 
Hakuna tatizo hapo. Funga naye ndoa na mpe watoto. Hataki ndoa hapo ingia mitini. Njemba kuzaa hapa TZ kwa vijana wa kiume ni JANGA LA TAIFA! Ng'ang'ania hapo hapo! Raha kuzaa na mwanaume umpendaye dada. Uyo mwingine atajiju. Ila mtoto wa jamaa lazima mumtunze..
 
Binafsi nasimama na mtoa mada huwezi kubali kubeba ujauzito wakati hujui hatma yenu ya mahusiano

Mwisho wa siku aje kupondwa hapa kisa single mom kama hujaolewa na matumaini ya kuolewa epuka kuzaa mapema full stop.
Upo sahihi, ila sababu kuu ya mtoa mada umri kuwa bado eti ni haraka wao kuzaa.

Atakuwa sahihi akiwa na sababu yoyote ile mwili ni wake haranguing kinachoshangaza anakuja kuingilia maamuzi ya watu anaandika as if anashangaa wapenzi kuzaa mtoto ndani ya mwaka mmoja...Hii akili.
 
Nimerudii tena mimi kadogo2 safari hii nina majonzi


Kuna story nilishaitoaga hapa kuhusu kumuacha Ex wangu kwa mambo Fulani fulani.. sasa bhn sababu kubwa niwe mkweli huyu ex wangu alikuwa anashauku sana ya kuwa na mtoto yaani hii ndio sababu ilifanya nikamuacha

Mimi na ex wangu Kama hajanidanganya Miaka yake basi tupo Sawa 25 kanizidi miezi michache tu yaani wote tuna Miaka 25

Kipindi tunakutana tulikuwa na Miaka 23 alitaka nimzalie ila sikufanya hivyo.. ugomvi ulipotokea tukaachana Kama mwaka hivi ila ndani ya huo mwaka tunatafutana tunarudiana tunaachana tenaa

Sasa mahusiano yalirudi rasmi kuanzia mwezi wa 3 mwaka huu tena yeye akilazimisha zaidii turudiane nikaona Hakuna tatizo maana mimi pia nilikuwa single

Kilichonileta hapa ex wangu nimegundua kuwa anaishi na mwanamke mwinginee tena huyo mwanamke ana ujauzito wake.. niligundua kupitia ndugu yake maana huwa nawasiliana nae nikaomba anichunguzie maana kuna vitu niliona sivielewi.. maana yeye kapanga mkoa X na anafanyia kazi mkoa mwinginee.. nilimuulizaga kwake anakaa nani akawa hana majibu ya kueleweka ikabidi nimuulize ndugu yake ndio kuniambia kuwa kuna mdada anamuonaona pale inasemekana wanaishi wote ila hakuniambia suala la kuwa mjamzito hilo niliambiwa na muhusika mwenyewe

Sasa ex wangu katika kuongeaongea akaanza kunilaumu kwanini nilimuacha mwaka mzima.. ikabidi nimuulize kama kuna mtu yupo nae.. akaniambia kweli anae mtu na hawezi kumuacha kwasababu ana mtoto wake tumboni..

Imebidi nishangae ndani ya mwaka mtu katafuta mwanamke na kampachika ujauzito alikuwa na haraka gani ya kufanya hivyo.. kumbuka ndani ya huo mwaka sio kwamba tuliachana moja kwa moja tulikuwa tunawasiliana sana na tunarudiana tunagombana tena tunapumzishana

Namuuliza kwanini umefanya hivyo anasema kwamba mimi nilimnyima mtoto na yeye hajui atakufa lini Akifa ghafla nani atarithi mali zake… kusema ukweli hili jambo limeniumiza sana sanaa sijaumia yeye kuwa na mtu kilichoniuma ni yeye kumpa na mimba juu huyo mdada… kusema ule ukweli mimi tangu niachane nae niliamua kutulia tu sikuhitaji mwanaume… maana nilijipa muda wa kutuliza akili ila sikutegemea mwenzangu amemoveon kiasi hiki

Nimemuuliza kuhusu mimi na yeye uhusiano wetu unakuaje anasema mimi ananipenda na hataki kuniacha ila yule mwanamke ana mtoto wake hivyo hawezi kumuacha pia.. kiufupi ni kuwa anatutaka wote

Mimi huyu mwanaume nina mpenda ila sasa nitakuaje nae na tayari kuna mwanamke ana mimba yake na mbaya zaidi kamuweka kwake Halafu anataka na mimi anipangie sehemu nyingine

Daah hata Kama ni malipo ila haya ni too much.. kwani mimi nilifanya makosa gani Miaka 23 kweli anataka tuzae hata ingekuwa ni wewe ungenishauri nimuache

Naombeni ushauri wowote tu nifanye nini juu ya hili jambo
Navoandika hapa ananitumia sms kila saa na nimeshamwambia sitaki anitafute ila bado hakomi huyu anataka nini kwangu jmn [emoji24][emoji24]


Hivi watoto mnafanya mambo ambayo hata wazazi wenu hatufanyi, kijana wa miaka 25 anaishi na mwanamke x, anataka ampangishie mwanamke Y nyumba, anazaa kisa atafuta mrithi akifariki.
 
Utoto raha sana....kwahiyo utapindua na mimba ya mwenzio au unataka akuhamishie [emoji1787]

Nipo kwenye novena liwalo na liwe… nipo namuombea hapa hiyo mimba awe amesingiziwa mtoto sio wake yaani kiufupi mwanamke ampige tukio kubwa zaidii [emoji2]
 
Sawa mimi siwezi kuzaa na mwanaume ambae sio mume labdaa itokee bahatii mbaya siwezi ku risk maisha yangu anaenipenda na mwenye utayari wa kuoa kwa wakati huo hanaga hizo slogan za nizalie mtoto kizazi changu sio cha majaribio
Kwa sababu zako ulizosema hapa unaweka Excuse, hata akikwambia muaone huyo mwanaume ungesema mapema yote umri huu unawahi nini mtu wa miaka 25....Seems una twist kulingana na kuzodolewa.

Short, your current institution ni ku date for fun na kuchezeana sio na upo tayari kudate na mwanaume hata miaka saba na usione tatizo.
 
Binafsi nasimama na mtoa mada huwezi kubali kubeba ujauzito wakati hujui hatma yenu ya mahusiano

Mwisho wa siku aje kupondwa hapa kisa single mom kama hujaolewa na matumaini ya kuolewa epuka kuzaa mapema full stop.

Wewe umenielewa wengi humu ni wanafki hivi kijana tupo age moja na anakwambia wenzangu wote wana watoto kasoro mimi naomba unizalie… maana yake mtoto ana thamani kuliko mimi Halafu nichanue tu nizae nae sina kazi nipo nipo tu aya ndy tukashindwana sasa akanizila mtoto analelewaje…. Tena kwa kazi afanyayo kila siku ana Hama huko anakutana na wanawake wapya na anakwambia nitaoa nikifika 30… sasa mna Miaka 23 mzae mpk anafika 30 anaoa kigori mimi ananitelekeza na mwanangu
 
Achana naye huyo mwanaume endelea na maisha yako na kama unakubali kuendelea naye kubali uke wenza na kumbuka huyo amekutangulia kumzalia huyo jamaa kwaiyo atakuwa na nguvu hata hapo baadae pengine yeye anaweza onekana ni mke wa kwanza wewe ndio mke wa pili...

Sawa
 
Unasema anashinda akikutumia message na kukupigia kwani simu yako Haina option ya " block this contact"?

Hata hivyo,huyo jamaa anataka tu kukufanya sex toy wake akikupangia chumba haimaniishi atakuwa amekuoa.
Akikosana na mke wako huko atakuwa anakuja kwako kupooza maumivu.

AKILI KUMKICHWA!!
 
Wamekuwa n mahusiano ya mwaka mzima, mtu ana umri wa 25 na Ana kazi then unasema amekurupuka kumpa mtoto.

"Mwanamke mwengine" minimize this act huyo ni mwanamke wake na si mwanamke mwengine bali mwanamke mwingine ni wewe hapa.

Unafosi maono yako kua maono ya wenzio, yeye anataka mtoto wewe hukutaka amempata aliyekuwa na maono sawa wamezaa why uje kufosi kuingilia maono yao na wewe si utafute asiyehitaji mtoto mwenzio.

Kitu pekee hapa ulikuwa na haki ya kuongea ni kukurudia huku akiwa na mwanamke mwengine sio blaa blame za mwak mmoj, kisasi, kisasi watu mmeacha as if mtu mkiachana bado unamiliki.

Komaa kiakili sio Hisia Hisia

Sasa hiyo comments uliotagg nilimjibu kutokana na alichoniuliza kwenye mada yangu nafikirii umeona nilichouliza… achana na comment maana najibu kutokana na mtu alivyouliza
 
Kuweka mawasiliano na ukaribu na x ni sawa na kutembea na muwa kama mkongoja wako, mwisho utakua,haya sasa amua uendelee kua Mua ama utupe pingili na maganda yake usonge mbele!!

Huyu tumerudiana since mwaka uanze sema huu ugomvi na wa majuzi so nimeita ex hivyohivyo
 
Anataka kuzaa na wewe huo ni uamzi wake hakuna kesi wal sheria inabana, wewe unashindwa nini kusema hutaki na mahusiano yaishe mpaka unalalama tu hapa umeshikiwa fimbo.

Wanawake munapenda mpaka kupangiwa maamuzi hayo maamuzi yake mwanaume wewe fanya yako.

Wewe mbona unakurupuka kwenye comments za watu si na wewe uchangie zako nikujibu
 
Kadogo2 mi nimeshakupenda sijui kwa nini anyway nimeona una upendo wa dhati ila ex wako kashindwa kuuona
 
Aliyepeana mimba yeye Kapokea, Kwani wewe ukipatiwa na wewe utakataa!? Mungu alihasa zaeni Muongezeke
 
Back
Top Bottom