Exaudi Kigahe (Mb) ametoa rai kwa watumishi wa kituo cha pamoja cha huduma za forodha Kasumulu kutimiza wajibu wao

Exaudi Kigahe (Mb) ametoa rai kwa watumishi wa kituo cha pamoja cha huduma za forodha Kasumulu kutimiza wajibu wao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Mhe. Kigahe: Watumishi wa Mpaka wa Kasumulu Timizeni Wajibu Wenu kwa Weledi na kwa Wakati

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Exaudi Kigahe (Mb) ametoa rai kwa watumishi wa kituo cha pamoja cha huduma za forodha Kasumulu kutimiza wajibu wao kwa wakati na weledi ili kuwahudumia wateja ndani ya muda mfupi.

Kigahe amesema hayo Desemba 19, 2023 wakati wa ziara yake katika mpaka wa Kasumulu wa nchi ya Tanzania na Malawi uliopo wilayani Kyela.

Aidha Kigahe amesema lengo la Serikali ni kuona wafanyabiashara wanafanya shughuli zao katika mazingira rafiki ili waweze kunufaika na biashara zao

Vilevile Naibu Waziri amebainisha lengo la ziara hiyo ni kuona shughuli zinazofanywa pamoja na kuona Changamoto za Wafanyabiashara ili kama Serikali iweze kuzitatua na kusiwepo na vikwazo vyovyote vya kuwakwamisha ili kuboresha Biashara za mipakani.

Vilevile, Mhe. Kigahe amesema ujenzi wa kituo cha pamoja katika Mpaka huo umesaidia kupunguza muda mrefu uliokuwa unatumika kwa wafanyabiashara kuhudumiwa na Serikali inaangalia namna ya kujenga masoko ambayo yatadhibiti njia za panya ambazo wafanyabiashara wanatumia kutorosha na kuingiza magendo Nchini.

Kwa upande wa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wa Mpaka wa Kasumulo Bw. Leonard Mapunda amesema TRA inaendelea kuweka mazingira rafiki ya ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara pamoja na kuwa karibu nao kwa kuwapa elimu kabla ya kulipa kodi.
 

Attachments

  • GBx0BDMWAAAuHpc.jpg
    GBx0BDMWAAAuHpc.jpg
    83.7 KB · Views: 5
  • GBx0BDLWkAAI1X_.jpg
    GBx0BDLWkAAI1X_.jpg
    102.4 KB · Views: 5
  • GBx0BDLXEAE1Go6.jpg
    GBx0BDLXEAE1Go6.jpg
    89.3 KB · Views: 5
  • GBx0BDOXMAAsJMg.jpg
    GBx0BDOXMAAsJMg.jpg
    104.8 KB · Views: 4
Asante kwa Bandiko Mkuu.

MAENDELEO HAYANA CHAMA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom