Asante mkuu kwa kutoa mafunzo mazuri ya computer
Swali- kwa ambaye tayari ana uelewa wa zile course za introduction to computer, kama anataka kujiendeleza hususani kusoma kozi itakayomuwezesha kuandaa data zake za kibiashara Yaani mapato, matumizi, kujua loss& profit n.k unamshauri asome course gan?, na mnaifundisha kwa bei IPI na itachukua muda gan?
Asante sana ndugu "mensaah", kwa mtu anayejua kutumia computer vzr kwa maana ya kumsaidia kufanya kazi zake kwa ufasaha.Kozi zifuatazo zaweza kuwa msaada tosha kwa tatizo lako tajwa hapo juu;
1. Microsoft Excel for Professional.
Hii Software nathani ulisha isikia,kama ukiisoma vizuri na kuielewa inaweza kukithi maitaji yako muhim kama sio yote kuhusu data zako za kimahesabu.
Faida:
1.Inapatikana kwa uraisi sana, maana ni moja wapo kati ya package ya Microsoft Office. Kwa iyo huna budi kuinunua yenyewe kama yenyewe.
2.Inatumiwa na watu wengi wanaofanya kazi za data kama uhitaji wako ulivyo. Hivyo hata uhamishaji wa data ni mwepesi.
3.Uelewa wako ndio limitation yako.
Hasara.
1.Kila kitu utaitaji kukifanya wewe,na lazima ukiandikie fomula ya kukiwezesha kifanye unachotaka.
2.Kwenye kutoa Report,wewe utachagua ni kipi unakiitaji na kinapatikana vipi,ili kiweze kutumika
2. QuickBooks & Tally
Hizi ni software maalum kabisa kwa ajili ya kuhainisha data na kuzifanyia uchakataji kulingana na unacho kiitaji.
Faida:
1.Ni rahisi kutumia hata kama mtu asipokuwa na uelewa mkubwa wa mahesabu/muhasibu.
2.Zipo automated kwa maana kuwa kila kitu kilishatengenezwa(background) so wewe ni kuclick na kuendelea na mahitaji yako.
3.Zimekuwa intergreted/kuunganishwa mfano. Store na duka/uuzaji au store na usambazaji.
Hasara.
Ni garama kununua na zinaitaji malipo ya mwaka kama utaitaji kuendelea kuitumia kwa ufasaha zaidi.
Sisi hapa kwetu, hizi kozi zote tunaziendesha kwa muda wa wiki mbili (20hrs) kila moja na bei yake ni 350,000/= kila moja.
Ndani ya wiki mbili maximum au wiki moja minimum utakuwa ushakuwa mtaalum na kuweza kujua jinsi ya kuzifanaya data zako zikufanyie kile unachokiitaji kwa matumizi yako.
NOTE: Hatukuachii ivi ivi,utaendelea kuwa kwenye uangalizi wetu kwa miezi mitatu kwa maana kwamba, ndani ya kipindi hicho ukipata tatizo lolote linalohusiana na ulichojifunza darasani,sisi tutakusaidia kutatua bure.
Asante na karibu sana.
Ofisi zetu zipo: Makumbusho Business Complex,2nd Floor,
tupigie: 0717 71 85 19 | 022 270 1320
tuandikie: training@comskills.co.tz
tembelea: www.comskills.co.tz