Hako Katoto nimekuwa sikapendi tokea kalipokuwa kanacheza pale Lumumba Rovers Msimbazi Center kisha akahamia Boom FC zote za Ilala baadae ndiyo Comrades wangu akina Patrick Rweymamu na Suleiman Matola a.k.a Veron a.k.a Mzambia wakati wakiwa wanaisuka Simba B wakaamua kukachukua hadi pale alipopandishwa na akina Kibaden na Julio kipindi kile walipokuwa wanapiga deiwaka Simba SC.
Ni Kachezaji Kanafiki mno na sasa hivi ndiyo nitakapuuza kweli. Kumbe ndiyo maana hata Samora ( Mchezaji wa zamani wa Boom FC na Simba SC enzi hizi na Mdogo wake wa damu kabisa Mshambuliaji mahiri na mwiba kwa Yanga Dua Said Dua ) aliwaonya mapema na siku nyingi sana kuwa tusimwamini Ibrahim Ajib kwani ni Mwana Yanga FC lia lia akina Kaburu wakatuingiza mkenge na hatimaye leo kimeeleweka.
Nyie hamjiulizi tu ni kwanini hivi majuzi katika ASFC Final pale Jamhuri Stadium Mkoani Dodoma Waziri wa Mambo ya Ndani na mwana Yanga FC Kindakindaki Mwigulu Nchemba alivalia Jezi ikiwa imeandikwa jina la Ajib? Wenye kujua mpira wa Bongo na Fitna zake tuliyashytukia haya mapema sana na tuliyategemea.
Hivi Vitoto viwili Mkude na Ajib vimenikera mno na kuanzia leo mlio nao karibu viambieni kuwa iwe mwanzo na mwisho kukaa nasi Masela kule katika yale Majukwaa yetu kwani tutawapopoa bure. Wametufanyia usaliti mkubwa mno sisi Wanasimba. Na tutaona hata kama huko Yanga FC watacheza labda yule Mtaalam wetu wa Pemba awe ameishiwa Ndumba. Tulichomfanyia Ramadhani Singano Messi wa Temeke ndiyo tutakachowafanyia hawa Wanafiki na Wasaliti wawili Waliotukuka.