jembehusler
New Member
- Feb 15, 2017
- 4
- 0
Duuhhhh!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio wakenya tu.. Afrika ndo inaelekea huko.Tunaweza tusiwe na uhakika lakini haina shaka kifo cha huyu bwana kilipangwa. Wakenya wakitafuta uongozi UTU huwaondoka kabisaaa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sikubaliani na hoja zako mbili... eti alifanya kosa kuuhakikishia umma usalama wa kura.....akili za makinikia hizo...sheria ipi kavunja?Lakini Msando sikuona sababu ya yeye kusema wazi kwenye media kuwa hakuna atakaye ingilia mfumo wa matokeo labda akatwe kiganja....Kwangu mimi niliona kama alikuwa amewapa mbinu wauwaji kabisa na zile zilikuwa tambo zisizo na msingi na hapa kusema kweli kabisa ndipo niliamini hakuna kitu kinaitwa Tume huru...
Kama mtu alipata wasaha kutazama mahojiano ya Msando atagundua kabisa kuwa alikuwa na upande wake na ndio maana alikuwa anaweka tambo na katika maongezi yake alionesha wazi kabisa uchaguzi uliopita uliingiliwa na wazi alikuwa ana watuhumu Jubilee...
Kwa hiyo Msando angeliweza kuhakikisha hakuna anaye ingilia mfumo wa matokeo kwa kuonesha vitendo na sio lazima kuweka tambo na kuonesha jinsi ambavyo wanaweza kuingilia matokeo...hilo ni kosa alilo lifanya pale kwenye usaili wake.
Halafu Kifo chake kina utata sana maana upande wa pili ule unaweza kuwa umetekeleza hii mission ili kuonesha kuwa wahusika ni watu fulani na kuhalalisha kuwa kura zimeibiwa na kabla ya kifo chake NASA walisema wamegundua kuna mpango wa wizi wa kura sasa najiuliza kwanini wasiwe NASA wame usika kwenye hili jambo ili kuthibitisha madai yao kuwa kuna mpango wa wizi wa Kura?
Halafu ni jana tuu NASA wamehoji usalama wa Kura zao baada Msando kuuwawa...
Bado naamini kuna mengi sana nyuma ya kifo cha Msando.
DUh!Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IECB Bwana Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ' Kitaarifa ' zaidi kutoka kwa ' Wadau ' mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ' Wabobezi ' wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea Kifo hiko cha ' Kikatili ' kabisa.
Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu zilizopita kabla ya hayo ' Mauaji ' yake ya ' Kikatili ' kutokea hivyo nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ' tathmini ' mwenyewe ' Kimoyomoyo ' kisha mwishoni wote tutajua ni nani ' Kamuua ' Marehemu Chris Msando.
Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa ' Oparesheni ' za IECB alijibiwa na kupewa ' Ushirikiano haraka sana.
Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa za Yeye ' Kutishiwa ' maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ' Ulinzi ' aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.
Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ' Onyo ' kali la kutozungumza na Chombo chochote cha Habari nchini Kenya na ' Mamlaka ' na kuambiwa kwamba Mtu pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa Habari na Mawasiliano.
Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ' alikaidi ' hiyo amri kutoka katika ' Mamlaka ' ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ' mauaji ' yake.
Tukio #5.
Wakati akiwa ' mubashara ' kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha Habari Marehemu alisikika ' akiwahakikishia ' Wakenya wote kuwa kwa jinsi alivyotengeneza ' Mfumo ' wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ' Kuudukua ' hata iweje na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ' hack ' taarifa zozote za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ' Kiganja ' chake kwani ili upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ' Kiganja ' chake cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.
Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ' Kimafia ' na labda pengine alijisahau kuwa siku zote ukitaka tu ' Kuuawa ' Kimafia basi Mtu wako wa Karibu sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ' Mwanamke ' ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ' Mwanamke ' kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ' Kimafia ' ndipo akamtega Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ' Wauaji ' wake wale ' Mafia ' walikuwepo.
Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ' Wauaji ' wake wa ' Kimafia ' walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ' Udukuzi 'wowote utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ' chake ndipo hata katika ' mauaji ' yake ya juzi ' Kiganja ' chake cha Mkono ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ' Wauaji ' na kuuacha mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.
Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule ambaye atakuwa kafanikisha ' mauaji ' ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi wote kitu ambacho ' Wauaji ' hawa walikifanya kwa ' Kumuua ' na Yule Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ' Mission Accomplished '.
Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ' Muuaji ' Mkuu wa Marehemu Chris Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ' Ushirikiano ' mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ' wamechoka ' na haya mauaji ya ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti.
Nawasilisha.
That is a movie mzee. Now kuna advanced security backups ambazo pia huitaji blood ku-circulate. Incase hujui...sidhani kama circulation ya damu inahusika.
my experience kutoka move ya 24 HOURS Jack bouer alikata kidole cha mtu ili kkitumia kupata access.
that is just my thinking
Kabisa the same fate,
Tom Mboya.
Josiah Mwangi Kariuki.
Dr. Robert Ouko.
Prof. George Saitot, etc, etc.
Sent using Jamii Forums mobile app
Soon we will be there..Kwani na Tanzania Kwetu hii ' Kitu ' ipo?
Don't jump into conclusion kwani hizi ni campaign zinazohusisha caucuses and syndicate and a lot of mobsters. ...it might as well involves a lot of blackmailing against each other. ..Kenyan politics a bit different. ...alway bloodshedNilikuwa nampenda uhuru ila nimeanza kudevelop chuki kwake baada ya kuisoma habari hii
Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
Kijana acha kubishana na wahenga.. wakati Burundi wanarekebisha katiba ili Nkurunzinza agombee kwa mara ya tatu ulijua kama soon na Rwanda watafata nyayo?!.. wakati huo na sisi tushaanza kampeni kama masihara ya kumbakisha Magu atawale mpaka kifo kama Mugabe.. bado tu hujasoma alama za nyakati?!.Acha kuhisi mambo / vitu na usitake kulazimisha kinachotokea nchini Kenya basi ni lazima na huku Kwetu Tanzania kije / kitokee. Wakenya wana tatizo lao Kubwa la Ukabila ambalo kwa bahati nzuri sana hata Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alishawahi kumuonya sana Rafiki yake wa wakati huo Jomo Kenyatta kuwa asipolidhibiti mapema basi huko mbeleni ( ambapo ni sasa ) Kenya ingekuwa ni Taifa la Kikabila mno badala ya kuwa la Umoja kama letu la Tanzania.
Kijana acha kubishana na wahenga.. wakati Burundi wanarekebisha katiba ili Nkurunzinza agombee kwa mara ya tatu ulijua kama soon na Rwanda watafata nyayo?!.. wakati huo na sisi tushaanza kampeni kama masihara ya kumbakisha Magu atawale mpaka kifo kama Mugabe.. bado tu hujasoma alama za nyakati?!.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekaa na Wakikuyu Zanzibar, hao ndio walinifanya niwachukie Wakenya na Kenya na ndiyo sababu katika nchi zilizoko Afrika Mashariki, Kenya haipo katika list za nchi nitakazoenda kuzitembelea. Wanapenda madaraka, ubinafsi, kutukuzwa, kubebana, ubaguzi na wizi. Ruto walimsongeza tu ili kupata kura za Wakalenji. Nitukaneni, nizomeeni lakini ukweli ndo huoWatu hawajui duniani twa pita tu na fahari zote za dunia tutaziacha......pumzika kwa amani Ndg....hakika kila mwana wa Adam ni lazima ayaonje mauti.
Albert Msando?