The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Courtesy: Mwanahalisi online TV
In summary:
1. Amkemea mwandishi kwa kusisitiza kuwa, serikali ilishafanya mabadiliko waliyoyataka ya kuundwa "Tume Huru ya Uchaguzi". Yeye amkemea na kumwambia:
"....kama unaamini kuwa kilichopitishwa na Bunge mwanzoni mwa mwaka huu ni Tume Huru ya Uchaguzi, basi wewe (mwandishi) hujui maana ya Tume Huru ya Uchaguzi...!"
2. Atumia muda huo kutoa elimu ya maana na mantiki ya "TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI" na uhuru ni upi. Mfuatlie mwenyewe kwenye video hii fupi...
3. Mwaka 2019 na 2020 tulishuhudia uchafuzi wa chaguzi hizo. Mwaka huu tumethibitisha pasipo shaka kuwa CHADEMA na vyama vingine vya siasa vilivyo nje ya serikali (vya upinzani) havishindani na CCM kwenye uchaguzi....
Amesema; ".....Sisi CHADEMA tulikuwa tunashindana na Majeshi polisi, TISS, JWTZ, Wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri za majiji, manispaa, wilaya, miji na watumishi wote wa serikali. Tumeshindwa katika uchaguzi huu na dola. CCM haipo, imeshakufa, haiwezi kushindana ktk sanduku la kura...!!
4. Mwisho amemaliza kipande hiki cha mahojiano yake kwa kusema;
".......kama hakutakuwa na mabadiliko muhimu ya mfumo mzima wa uchaguzi wa nchi na taifa letu kwa kubadili sheria na katiba, basi HAKUNA UCHAGUZI MKUU MWAKANI, yaani mwaka 2025...!
Watafanyaje kuzuia uchaguzi huo? Weka MB na kisha Mtazame, msikilize na mfuatilie mwenyewe kwenye video hii fupi ya dakika 15 hivi....