Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Exclusive: Jay Dee afunguka, atoa sababu za kuitosa ndoa yake

Duuu hakika dunia ina mambo mengi sana hasa linapo kuja swala la mahusiano..huyu dada pengine hakupendwa na G bali alikuwa anatumiwa tuu! Hizi tuhuma zina mdhalilisha sana G duu!

Lakini pia ni kweli ulio wazi Jide ana tatizo kubwa na kisaikolojia ni wazi kabisa hana furaha kabisa pamoja na kuachana na G maana tangu aanze kuonge hajawai kumaliza!

Hakika Jide nilikuwa namchukulia kama mwanamke jasiri sana na wakuheshimika lakini nilipo muona kakimbilia kwa mpiga ramli na kukubali kudanganywa hakika niliamini Jide ni mwanamke mwenye matatizo makubwa sana na ana hitaji msaada

Hata hivyo ni wazi alikuwa na haki ya kuachana na G.

Kila mtu ana weakness yake Ruta..
 
Walivyokuwa wana act kwenye DIARY, utadhani kweli wako kwenye ndoa ya furaha+
Mapenzi haya!

Unajua jide alicho kuwa anafanya sio kipya kabisa 60% ya maisha ya ndoa yamejaa unafiki tuu...watu wanaumia hawana jinsi inabidi waendelee kunyamaza na kubaki kwenye moto..hadi wanapo karibia kutokwa roho ndio wana kimbia!
Usione watu wanacheka kumbe ni unafiki tupu na sanaa!
Kuna mada moja alileta lara 1 ilisema-ndoa ni taasisi iliyo jaaa unafiki wa hali ya juu watu waliwaka sana! Lakini mimi niliilewa sana tena na huo ulio ulikuwa ukweli..nadhani ushahidi wa mada hile unaanza kupatikana ..

Kama ujui kuigiza na kuwa mnafiki sidhani kama unaweza kudumu kwenye ndoa hasa za kiafrika ambazo kifo ndio hutenganisha ndoa!

Kama uwezi kuwa mnafiki au kuigiza usijiingize kwenye ndoa kabisa maana baada ya mwaka itavunjika!
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa alivyosema kaacha kila kitu inamaanisha ile nyumba,envoque na murano kamuachia gadner? Mbona gadner aliondoka kwenda kukaa m/nyamala akiwa na fuko la Rambo? Juzi Juzi jide alipiga picha na prof jay akiwa na gari zake zote mbili au wakati anaenda USA alipanda nazo kwenye ndege then akarudi nazo? Kama gari still anazo kwanini asema kwamba hajaondoka na kitu?

Haaaaaa King Kong umeongeza chumvi hapo kwenye kuondoka na mfuko wa rambo

Alivyoenda USA hakuondoka navyo bana ila ndugu zake ndio walienda kuvichukua huko Kimara.. baadhi wakagawana na Gardner.. nasikia moja ya alivyoachiwa ni ile costa ilioandikwa machozi band.. ilikua yapaki MOG sana... Nyumba yake kapangisha mwezi uliopita na leo naona kaweka wishes za valentine alizopewa na mpangaji wake IG.

Ye ndio akaenda zake kukaa Masaki though nyumba ya masaki sio ya kwake kwa sasa labda aje ainunue hapo baadae
 
Lady Jaydee afunguka, avunja ndoa na Gadner

jide_na_g.jpg
 
Jide ukimwona saivi ni kama mtu anayepungukiwa kitu fulani ila anashindwa kukicover....Hakuwa mtu wa kujichanganya kiivo ila leo usishangae anakupigia hodi kwako aje mpige story.

Yani namna alivyomsema Gadner sijapenda kabisa ameongea kijinga sana, labda anahisi itampunguzia maumivu moyoni maana kumuacha mtu ambae bado unampenda na amekuwa zaidi ya mume sikia tu kwa wenzio.

All in all maisha ya mwenzie bado yanaendelea labda alifikiri atakwama.

wewe nawe umelikomalia ishu ya jaydee,eti amekuwa zaidi ya mume ...umeambiwa alikuwa anampiga,anamuonyesha vituko vya kipuuzi wazi wazi......bado unataka dada wa watu aendelee kusuffer kisaikolojia,kulia kila siku kwa kuonyeshwa hajaliwi/hapendwi............ bado mnaexpect mtu aendelee kuishi ndoani kuwaridhisha nyie, na akitoka msione wote wako rensponsible kwa ndoa kuvunjika, mnamnyooshea mtu mmoja kidole,........SAY NO TO UNHAPPY MARRIAGE....:embarrassed1:
 
Haaaaaa King Kong umeongeza chumvi hapo kwenye kuondoka na mfuko wa rambo

Alivyoenda USA hakuondoka navyo bana ila ndugu zake ndio walienda kuvichukua huko Kimara.. baadhi wakagawana na Gardner.. nasikia moja ya alivyoachiwa ni ile costa ilioandikwa machozi band.. ilikua yapaki MOG sana... Nyumba yake kapangisha mwezi uliopita na leo naona kaweka wishes za valentine alizopewa na mpangaji wake IG.

Ye ndio akaenda zake kukaa Masaki though nyumba ya masaki sio ya kwake kwa sasa labda aje ainunue hapo baadae

Daa jf rocks hii ya kuondoka nafuko wa rambo ilinichekesha sana....nilivuta picha G kabeba mfuko wa rambo daaa.

Kwani hivi G na J hawajapeleka shauri mahakamani la kuachana? Kama hawajapeleka na hawana mpango basi Jide hawezi kuruhusiwa kufunga ndoa bila kuvunja ndoa iliyopita!
 
Media love, yanaishiaga hivyo!

This has nothing to do with media love bali hii ni hali halisi ya ndoa nyingi za Waafrika ni za kinafiki,maigizo na kiunafiki hata kama uonekani kwenye media unapo ingia kwenye ndoa lazima uwe mnafiki,muigizaji na mvumilivu ndio utaweza kudumu japo hata miaka 11 kabla ujamwaga manyanga.
 
hapo tangu mwanzo palikua hakuna mapenzi walikua wanaviziana kwenye chapaa tu
 
Huku Flora...huku Jide

Nadhani kuna haja hii taasisi ya ndoa iandaliwe mtaala chuo kikuu...wanaohitimu tu ndio waingie.....muda si mrefu tutamsikia na yule binti mwenye Quarter Faraja naye anamwaga ya kwake...."yaani nimeteseka na yule baba mpaka yamenifika kooni"

Duuh!!
 
Dar es Salaam. Mwanamuziki nyota wa kike nchini, Lady Jaydee jana aliamua kuwaburudisha mashabiki wake kwa staili ya kipekee; kuzungumzia kuvunjika kwa ndoa yake na Gadner Habash.
Kwa muda mrefu kumekuwa na minong’ono kuwa wawili hao wametengana, lakini hakuna aliyekuwa tayari kuweka wazi kuhusu suala hilo. Hata hivyo, jana, Jaydee, ambaye jina lake halisi ni Judith Wambura aliamua kutoa ya moyoni, akisema kuwa kwa sasa ametengana rasmi na mtangazaji wa kituo cha redio cha E-fm cha jijini Dar es Salaam.

Jaydee ambaye wakati mwingine huitwa ‘Jide’, kwa wiki moja sasa ameamua kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii. Kati ya maswali aliyoulizwa na mashabiki wake ni kama ni kweli ametengana na mumewe na ni sababu za kutengana.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, mwanadada huyo alisema: “Nimemvumilia vya kutosha, kuhusiana na tabia zisizokuwa na nidhamu wala heshima ya ndoa na sasa imefika kikomo. Msanii huyo anayemiliki Machozi Band, alibadili picha ya wasifu ya mtandao huo na kuweka jicho linalotoa machozi na kidole kikivuja damu. Alisema kuwa yeye na Gadner hawajaachana kama ambavyo watu wanasema isipokuwa yeye ndiye aliyeamua kumuacha mwanamume huyo.

Hata hivyo, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Gadner alisema: “Sina comment katika hilo.”
Aliongeza kusema: “Aliyezungumza ni mtu mzima na amefanya juhudi kuzungumza alichozungumza. Ku-comment kwa kupinga au kukubali ni kuzidharau juhudi zake.”

Meneja wa mwanamuziki huyo maarufu kama Rapa Wakazi, alisema kuwa kilichozungumzwa na kuandikwa na mwanamuziki huyo ni kati ya mwimbaji huyo na mashabiki wake, hivyo hakuna cha kuongeza. Meneja huyo alisema ingawa mwanamuziki huyo hakuhusisha uongozi wakati anaandika, lakini hayo ni mawazo yake na yabaki kuwa hivyo.

Wakati Habash akisema hayo, Jide aliamua kufunguka na kusisitiza kuwa hatarudi nyuma kwa uamuzi aliouchukua. Na hii ni sehemu ya majibu yake:
Swali: Tumesikia umeachana na mumeo kweli au si kweli?
Jide: Hatujaachana, nimemuacha.

Swali: Kwa nini umeachana/ umemuacha mumeo?
Jide: Nimeamua kutokana na kuwa ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo… ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwepo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku nikipretend (kwa maigizo), ili kuridhisha jamii.

Swali: Huoni kama umejishushia heshima kuachana na mumeo?
Jide: Sioni hivyo ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asiye na heshima… amekuwa akiwapa mademu (vimada) magari yangu na kuyagonga wakati nipo safari, ukiachilia mbali vipigo. Kifupi ilikuwa ndoa ya mateso.

Swali: Baada ya kuachana unatarajia kuolewa tena?
Jide: Ni mapema kujihakikishia kuolewa na mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Nahitaji kuwa makini zaidi kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

Swali: Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?
Jide: Nilidhani angebadilika, nilikuwa natoa nafasi, iliposhindikana nikaona isiwe tabu, kila mtu aubebe mzigo wake. Ukizingatia ananizidi umri miaka mingi, alitakiwa yeye anielekeze zaidi kuliko mimi kumwelekeza maisha mtu mzima.

Swali: Uliwezaje kuondoka?
Jide: Nilipoamua iwe basi, niliondoka bila kubeba kitu, nikasafiri kwenda Marekani, nikakaa huko mwezi mzima kurefresh (kujiliwaza) na kujipima kama ninaweza kumove on (kuendelea)? Niliporudi Tanzania sikukanyaga tena nyumbani mpaka muda huu ninatype (kuandika) na kupost (kutuma) majibu haya. Kwa kifupi niliondoka bila kuaga sikuona sababu ya kuaga. Ahsanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.


Jay Dee alichomoza kwenye anga za muziki baada ya kurudia kibao cha mwanamuziki nguli, Marijani Shabani cha “Zuwena” ambacho kilimpa umaarufu mkubwa.

Mwananchi Jumamosi | Februari14 2015
 
Daa jf rocks hii ya kuondoka nafuko wa rambo ilinichekesha sana....nilivuta picha G kabeba mfuko wa rambo daaa.

Kwani hivi G na J hawajapeleka shauri mahakamani la kuachana? Kama hawajapeleka na hawana mpango basi Jide hawezi kuruhusiwa kufunga ndoa bila kuvunja ndoa iliyopita!

Bado hawajapelekana..... labda hapo baadae kama akipata mwenzi serious anaweza kuanza kufanya hizo procedures

Lawyer kwahiyo kama mtu mlifunga bomani mnatakiwa kwenda mahakamani kuvunja ndoa??
 
Kila mtu ana weakness yake Ruta..

Pamoja na yote mabaya ya Gardner aliyoyaeleza Jide, hili suala la kupiga mwanamke ni la kishamba sana! Sikuwa nimefikiri kwamba mpaka leo hii mjini kuna mwanaume anapiga mwanamke aisee!!!! Kumbe jamaa ni mshamba hivyo?!!!
 
Bado hawajapelekana..... labda hapo baadae kama akipata mwenzi serious anaweza kuanza kufanya hizo procedures

Lawyer kwahiyo kama mtu mlifunga bomani mnatakiwa kwenda mahakamani kuvunja ndoa??

Mahakamani ni hatua ya mwisho kabisa...hata hao walio fungia kanisani kwanza lazima waka suluhishwe huko..hikishindikana wana kwenda kwenye mabaraza ya wilaya ...na huko ndiko watashibitisha ndoa hii haiwezi kurudi kama mwanzo ndio mahakama inavunja! Na wengi hukimbilia mahakamani maana huwa ni vigumu kanisa kuvunja ndoa au kwingineko ..
Kwa hili la G na Jide itachukua muda mrefu sana kuachana kabisa maana itawabidi kwanza waanzie kwenye usuluhishi!
 
Pamoja na yote mabaya ya Gardner aliyoyaeleza Jide, hili suala la kupiga mwanamke ni la kishamba sana! Sikuwa nimefikiri kwamba mpaka leo hii mjini kuna mwanaume anapiga mwanamke aisee!!!! Kumbe jamaa ni mshamba hivyo?!!!

Lakini hili la kupiga mwanamke limemshushia sana heshima G ni aibu sana me mwenyewe huwa siamini kama ni kweli!
 
Lakini hili la kupiga mwanamke limemshushia sana heshima G ni aibu sana me mwenyewe huwa siamini kama ni kweli!

Gadner ana mapungufu yake, lakini kuishi na mwanamke kama Jide nayo inahitaji kipaji,mwanamke hajui kujishusha anapenda maugomvi angalia list ya aliogombana nao Clouds, Shigongo,FA, Matonya unaweza ukapata picha ni mwanamke wa aina gani. Nadhani Gadner alikuwa mtumwa ndani ya ndoa yao.
 
Back
Top Bottom