Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
Pole sana kwa uchovu wa safari za kampeni, nikupongeze kwa dedication na determination yako ya kupambana bila Kukata tamaa na kuvuka vihunzi vyote vya wapinzani wako.

SWALI: Mikakati gani mmeweka kuhakikisha mnapata mapema kabisa nakala original za matokeo ya kila kituo kwa chaguzi za level zote ili kuepuka hujuma inayoweza fanyika.

2. Ikitokea Rais Magufuli ameshinda kihalali kabisa na ukaridhika. Upo tayari kumpa ushirikiano mf; kumtambua na kuhudhuria kuapishwa kwake ama utakua opposer kwa muhula uliobaki?

3. Ikitokea umeshindwa uchaguzi kihalali kabisa. Je una mpango gani wa kuendeleza vuguvugu la upinzani kwa miaka hii mitano hasa ukizingatia tutakukosa bungeni ambapo ulijizolea umaarufu kwa kujenga hoja nzito za kisheria? Kiufupi WHAT IS NEXT after elections in a worst case scenario?

Ubarikiwe na nakuahidi mimi na familia yangu na marafiki zangu wote wa karibu kukupa kura zetu zote hiyo tarehe 28.
 
Vipi kuhusu mpango wa Elimu Bure kwa wanafunzi endapo utafanikiwa kushinda uchaguzi na kuunda serikali? Uatendelea na utaribu wa sasa uliopo wa CCM au utakuja na njia mbadala?
 
Mhe. Tundu Lissu Kwanza nakupongeza Sana Kwa kuleta ushindani katika Uchaguzi wa Mwaka huu. Kimsingi umewapa watanzania Fursa nzuri ya Kuchagua.

Mimi ninaushauri ambao Nadhani unaweza ukakuongezea Kura katika kipindi hiki cha Lala salama.

1. Naomba utumie muda wa Kutosha kuelezea nini utafanya kwenye FAO LA KUJITOA katika mifuko ya Jamii. Ulielezea hapo Awali but Nadhani unahitaji uliweke vizuri hasa namna ambavyo kila mfanyakazi anaweza akajikuta katika Dhurma hiyo kubwa. Kimsingi Fao la Kujitoa linakulazimisha uache fedha zako kwenye Mfuko then hiyo hela ukutane nayo uzeeni Hali inayomfanya mfanyakazi anayetaka kuachankazi Ili afanye shughuli zake binafsi kupoteza Uhuru huo.

2. Kuna DHURMA kubwa Kwa wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba pamoja na Hifadhi za Jamii. Kumbuka Hifadhi zote Tanzania zinacover takriban theluthi ya eneo la Tanzania. Hivyo, zinawagusa wananchi wengi waishio vijijin. Fahamu kuwa Kama vile wanavyouwawa Wavuvi kule Maziwani, wananchi wengi wanaoishi pembezon za Hifadhi pia wanapata kadhia hiyo hiyo Kwa kigezo cha kufanya Ujangili na kudhurumiwa ardha zao Kwa lengo la kuhifadhi. Naomba utumia muda wa Kutosha kuliweka hili vizuri Ili wananchi waishio pembezoni za Hifadhi mbalimbali watendewe Haki.

3. FIDIA (Compansation) Kwa uharibifu na Vifo vinavyosababishwa na wanyamapori. Eneo hili ni kero kubwa Sana Kwa wananchi waishio pembezoni mwa Hifadhi zote Tanzania. Wananchi wengi wametiwa umaskini Kwa mazao Yao kuliwa na Wanyamapori au kuuwawa kabisa. Kwa Sheria zilizopo, wananchi hawalipwi FIDIA bali wanalipwa KIFUTA MACHOZI (Consolation) ambacho hakiendani kabisa na Mazao yaliyoharibiwa. Na Kama mtu kauwawa analipwa Tu 1m na Hadi uipate hiyo Consolation ni shughuli pevu. Pigilia msubari eneo hili utang'oa Kura nyingi Sana za vijijin/wakulima.

4. Sehemu nyingine muhimu ni kuelezea namna utakavyoongeza ajira if you are elected. Wananchi wengi wanaishi maisha aliyoyaida Dr. Chris Mauki kuwa ni ya Kibabaishaji. Tunahitaji Descent Jobs. Tunaomba uelezee namna utakavyolifikia hili na ukazie namna utakavyoboresha mazingira ya Kazi/ajira.

Ni matumaini yangu kuwa utazingatia ushauri huu.
 
Mheshimiwa Tundu Lissu, pole kwa changamoto ulizopitia na hongera kwa kuwa na moyo wa kuendelea kupambana kwa ajili ya HAKI.

Maswali yangu:

1. Watanzania wengi ni wakulima, zamani tuliambiwa 80% kwa sasa sijui ni kwa asilimia ngapi. Wengi wa hao wakulima ni wa kujikimu tu na hivyo kulima bila tija. Una mpango gani katika kuwezesha watu hawa kufaidika na kuendelea zaidi kwa kuwaongezea tija katika kilimo tofauti na ambavyo imekuwa ikifanyika chini ya serikali za ccm na hasa hii ya awamu ya 5?

2. Baada ya awamu ya tano kuingia, tuliona juhudi kubwa katika kuondoa sekta binafsi katika kuendesha uchumi. Matokeo yake shughuli za ujenzi zikahamishiwa kwenye taasisi za majeshi au katika idara za serikali na maeneo mengine wakitumia mtindo wa FORCE ACCOUNT kufanya miradi yenye thamani kubwa kinyume cha sheria za manunuzi ya umma. Matokeo yake sekta ya ujenzi hasa makampuni ya ndani, yaliyokuwa yameajiri maelfu ya vijana, kufilisika au mitaji yao kuporomoka na kufa kabisa.

Upande mwingine miradi mingi mikubwa yote imekabidhiwa makampuni makubwa ya nje. Je, una mpango gani katika suala hili? Na utafanya namna gani ili kuamsha tena kampuni za ndani na kuzijengea uwezo kimtaji ili ziamshe tena uchumi wetu na kuwapa vijana ajira?

Asante!
 
Je, upo tayari Kupokea nafasi ya kuteuliwa na Mh John Magufuli ,endapo atashinda uchaguzi?
 
Kuna wadau tuliosoma nje ya nchi na tulidhaminiwa na bodi ya mkopo. Mimi nilifanikiwa kumaliiza deni language lote.

Ila kwa wale ambao wanategemea kukatwa kwenye mishahara, Deni la kila mmoja HESLIB ( bodi ya mikopo ) ni milioni 90 kwenda juu.

Ukijumlisha na retention fee deni halimaliziki ila linajizalisha.

Swali:
Inawezekana kufuta hili deni kwa hawa watanzania ambao hata ajira zinazoeleweka hawajazipata?

Serikali ilitupeleka tukasome nje huku wakijua kuwa deni halitaweza kulipika.kuna uwezekano serikali yako ikafuta au kupunguza deni lote kwa sababu kama ulivyosema kuwa tutalipa 3% ni deni kubwa sana. Mil 80-90 sio pesa ndogo kwa mishahara ya Tanzania.
 
ASANTE SANA JF

SWALI LA KWANZA
Kwanini Lissu ametafuta ukimbizi wa kisiasa wakati yeye si mkimbizi wa kisiasa?

SWALI LA PILI
Kwanini ana tiketi ya kurudi Ubelgiji au ndio kusema ana uhakika hatashinda Urais au nia yake nini hasa?

Pili kwanini watoto wake kawapeleka nchi nyingine? Je, ana lengo la kuleta machafuko na kukimbilia nchi nyingine?
 
Nina Maswali mawili ..

1. Mosi, Mmejipangaje kuwa na uraia pacha na sera nzuri za uraia pacha maana kuna wataalamu wengi sana huku watanzania wameshindwa kuja kulitumikia taifa baada ya uwepo wa sera mbovu kuhusu uraia.

2. Pili, Serikali ya CCM imetudanganya sana kuwa wawekezaji wanamiminika kuwekeza huko nchini ilhali uhalisia mahusiano ya Tanzania na nchi za kigeni kwa awamu hii yako taabani hadi kupelekea nasi kuwa tuna "trend" kwenye matamko ya kimataifa kwa namna hasi je umejipanga vipi kurejesha mahusiano mazuri ya kidiplomasia yatakayopelekea wawekezaji kuja kam hapo awali?
 
Asante sana

Swali: Je, utafanya nini kuhakikisha kwamba nchi inajenga mifumo imara, endelevu inayofanya nafasi ya Uraisi kuwa taasisi kuliko kuwa mtu.
 
Jumbo LA Same linaloongozwa na mama Kaboyoka limekuwa na bara bara yenye kero kubwa sana.

CCM wameitupa hii bara bars na ila kilometa karibia 50.

Je, serikali yako itaweza kuweka lami hii bara bara inayoanzia mkomaz mpaka same na kuanzia hedaru kupandisha milimani kupita mamba myamba mpaka ndungu -kihurio-mkomazi?
 
Lisu hapa atakimbia tu:

1. kila siku unasema utawataja walikupiga risasi na unasema unawajua kwa nini huwataji?

2. Polisi wanasema umlete dereva wako ili wamhoji, kwanini hutaki?

3. Unasema utawaingiza vijana mtaani kudai matokeo kama utapigwa na JPM, vipi na wewe utakuwa frontier?

4. Mbowe anadaiwa kupiga pesa za chama na baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamekubali kuwa kuna wizi wa ruzuku. Vipi uko tayari kuweka kila kitu peupe?
 
Mh. Lissu, swali langu ni juu ya wafanyabiashara ndogo ndogo ambao kwa sasa wameruhusiwa kufanya biashara kila sehemu bila kujali usalama wao binafsi, wateja wanaowahudumia, watumiaji wengine wa maeneo hayo au hata mazingira husika mfano ulio dhahiri ni pembezoni mwa barabara.

Je, Mkakati ulionao ni upi ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kujitokeza lakini pasipo kuwaathiri kibiashara na wakati huo huo mazingira yakibaki safi na salama?
 
Mh. Tundu lissu

1. Utachukua maamuzi gani kama tume hii ya uchaguzi isipo kutangaza kama umeshinda kiuhalali?

2. Utachukua uamuzi gani Kwa tume ya uchaguzi kama wagombea wa ubunge na madiwani wa chadema wasipo tangazwa kushinda kama ikiwa wameshinda uchaguzi kiuhalali?
 
Kwanza nikupongeze kwa jinsi unavyokabiliana na vikwazo unavyokumbana navyo."umenifunza kutorudi nyuma kukitetea kilicho halali kwangu"

Swali: "Wamezoea kugeuza matokeo". Je, Utateteaje kura zako halali ikiwa mawakala watanyimwa nakala halisi toka vituoni maana tushasikia hawataruhusiwa kuingia na simu ambazo zingesaidia kupiga picha hizo nakala kama ushahidi?

Ahsante!
 
Hatujasikia marekebisho yoyote yaliyofanyiwa tume kwa kiwango cha kuwaridhisha upinzani. Ni kwanini unajiandaa kutoiamini tume na matokeo ya wewe kushindwa lakini unaitambua sasa kwa kufuata taratibu tume ilizotoa ili kura zipigwe?

Kwa kuwa sheria haikuruhusu wewe kuwa na tume au bodi au kituo cha kuhakiki kura zako. Ni vigezo vipi na kwa kutumia taasisi zipi halali utatumia kuwaonyesha wafuasi na uma kuwa hujatendewa haki wakati matokeo yatakapokuja kuwa umeshindwa?
 
Mbowe alisema kuwa mkishika madaraka mtaunda tume ya maridhiano na hamtapeleka MTU yoyote mahakamani na hamtalipa kisasi kwa mtu yoyote.

Ila kwenye kampeni zako umesema kuwa utafuta vitambulisho vya magufuli na pesa lazima irudishwe, sasa hio pesa itatoka kwenye hazina au itatoka kwa magufuli former president?.
 
Habari mgonbea urais
Swali? Mmejipanga vipi na mawakala na mbona siskiii uktoa morali kwa mawakala kuuza kura umejipangaje na hili mueshmiwa?????

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…