Mh Lissu, Sera kuu iliyoko kwenye Ilani ya CHADEMA, 2020, chama kilichokupa dhamana ya kuwa mgombea Urais ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.
Kwenye hiyo Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2020 (Uk. 2), mmenukuu falsafa ya Baba wa Taifa ya Ibara ya 28 ya Mwongozo wa TANU wa mwaka 1971, kwamba; Kwa watu ambao walikuwa watumwa, au ambao walikuwa wakionewa, wakinyonywa, na kunyanyaswa kwa sababu ya Ukoloni, Ukabaila au Ubepari, “Maendeleo” maana yake ni “Ukombozi”.
Kitendo
chochote kinachowapa uwezo zaidi wakuamua mambo yao wenyewe, ni kitendo cha maendeleo, japo kama hakiwaongezei afya wala shibe. Kitendo chochote kinachowapunguzia uwezo wao wa kuamua mambo yao wenyewe na kutawala maisha yao
wenyewe, si kitendo cha maendeleo,ni kitendo cha kuwarudisha nyuma, japo kama kitendo chenyewe kinawaongezea afya na shibe kidogo.
SWALI:
Ni nini tafsiri sahihi na yenye uhalisi, nyakati hizi za Utandawazi, Soko uria, ili kuwaondoa maadui watatu (Umaskini, Maradhi na Ujinga) katika jamii?
SWALI:
Kwenye kampeni zako, na hata msimamo wa CHADEMA, Serikali ya CCM kwenye miaka 5 inayoisha, imeleta maendeleo mengi, ambayo mnadai ni "maendeleo ya vitu", je, mna Sera gani za kuondoa hao madui watatu katika jamii?
Ilani ya CHADEMA, imesheni mapendekezo ya mikakati mingi inayohusu "maendeleo ya vitu" kurasa za 56; 70; 72; 84 na 89.
SWALI:
Ni wakati gani wa kampeni utaongelea hayo, kwa msingi kwamba tayari kuna kiasi cha maendeleo ya vitu? Au mpango wa Serikali yako ni kuanza upya, na miradi iliyopo ikawekwa kando?
Utanisamehe kukuuliza maswali yafuatayo yanayogusa maisha yako binafsi:
1) Wewe ni muuamini wa dini? Kuna uthibitisho gani kuwa unaamini na kuishi kwa maandiko matakatifu?
2) Una jambo gani la kitaifa, lenye uzito mkubwa, umelifanya uweze kuaminika kukabidhiwa maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 60?
3) Maisha yako yote umekuwa huheshimu mamlaka na kwa maneno na vitendo unadharau, je, ukipewa madaraka makubwa ya Urais, unauthibitishaje WaTanzania, hutokuwa dikteta mwenye dharau ya kiwango cha juu kisicho na mfano katika dunia hii?