"Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaiomba radhi sana serikali kwa kashfa hii iliyotokea mkoani na tutakuwa tayari kuwajibika kisiasa kama hapana budi," imesema sehemu ya taarifa ya Njoolay aliyoitoa kwa waandishi wa habari.
Taarifa ya tume hiyo ya watu tisa iliyofanya uchunguzi kwa takribani mwezi mmoja, imebainisha kuwa waliohusika na ufisadi huo ni watendaji 43 wa vijiji, mawakala 23, watumishi wanne wa kilimo ambao wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kwa mujibu wa Njoolay,wenye nyadhifa za kisiasa waliobainika kuhusika na kashfa hiyo wakiwemo madiwani na wakuu wa wilaya watafikishwa kwenye vyama vyao vya kisiasa ili washughulikiwe huko.(say whaaaaaaat!)
Tunashukuru kwa kuombaradhi
Ila kwa nini wengine mahakani na wengine kwenye chama? Ina maana kama ni mwenyekiti au diwani apelekwi mahamani ila kwenye vikao vya chama? kwani wameiba hela za chama? ACHENI UTANI BWANA!! Pinda yu wapi jamani? KILIMO KWANZA? Huu mkoa ndio kati ya mikoa .... inayotegemewa kulilisha taifa yenyewe inatambulika kama big ...., Sasa itakuweje mwakani? Si njaa tu?