EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

15:35

Mgombea wa pili wa urais nchini Kenya Dkt Ekuru Aukot amekubali kushindwa.

Ndiye wa pili kutangaza kushindwa baada ya Dkt Japheth Kavinga Kaluyu kukubali kushindwa jana.

Dkt Aukot amesema anaamini "Wachache walipata fursa ya kusikika, na wengi walishinda."

"Jiwe la Daudi halikumuweza Goliathi wakati huu, na asiyekubali kushindwa si mshindani," amesema.

Ametoa wito kwa Raila: "Hatungekuwa hapa bila wewe, demokrasia ya Kenya ya sasa haiwezi kuzungumziwa bila wewe kuwepo.

Kenya yataka kusonga mbele, Wakenya wanataka kurejelea shughuli za kawaida.

Kwa kuchunguza Fomu 34A tulizopata, tumegundua kwamba hakuna sababu ya kuamini kuna chochote kitabadili matokeo ya sasa."

Amemtaka Rais Kenyatta, akitangazwa mshindi, aunde serikali yake kwa kujumuisha wote.

Dkt Aukot amedokeza kwamba huenda akawania tena urais mwaka 2022.
Credit:bbc
 
Namwamba na munya wameshafutika kisiasa baada kuangushwa..... mutua na ruto sio wakikuyu hivyo hawaendi kokote

Kwa siasa za kenya zilivo usishangae 2020 ruto akawa timu moja na kina musyoka and family

Ruto ndo mgombea urais wa jubilee 2022
 
but i agree, there are still some idiots in our country, Kenya...for example, those who went to the streets to protest in Mathare, Kisumu and led to the deaths of 4 people now....very sad that there are still very foolish ppl in this world....but i blame Raila for those killings...saying that the election has been rigged without proper evidence is very wrong...such kind of inflammatory statements is what caused the protests and the subsequent deaths of innocent Kenyans...
 
but i agree, there are still some idiots in our country, Kenya...for example, those who went to the streets to protest in Mathare, Kisumu and led to the deaths of 4 people now....very sad that there are still very foolish ppl in this world....but i blame Raila for those killings...saying that the election has been rigged without proper evidence is very wrong...such kind of inflammatory statements is what caused the protests and the subsequent deaths of innocent Kenyans...
He will become the villain soon. Hope Kenyans dont spill blood
 
OFFICIAL PRESIDENTIAL RESULTS:

01:20am August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) Imetangaza matokeo ya vituo 29,209 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 6,044,745 (55.27%) na Raila Odinga kura 4,805,159 (43.93%).

09:00am August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 36,912 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,511,454 (54.62%) na Raila Odinga kura 6,124,426 (44.53%)

12:00pm August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 38,341 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,776,101 (54.4%) na Raila Odinga kura 6,394,921 (44.74%)

3:00pm August 09, 2017 UPDATE:

Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza matokeo ya vituo 39091 kati ya 40,883. Uhuru Kenyatta kura 7,915,044 (54.35%) na Raila Odinga kura 6,520,918 (44.78%)

August 10, 2017 - 06:30am UPDATE:

Uhuru - 8,030,150 (54.27%)
Raila - 6,634,331 (44.84%)

Valid votes: 14,795,377
Reporting Stations: 39,755 out of 40,883

LIVE VIDEO FEED:



fe7a316c97d3b4563a4c2cbca91a7a97.jpg


c6e580981b0395e5277b6f9e203969ff.jpg


FACT 1: Kenya spent 49.9billion Kshs to organize this election and it's the most expensive since country's independence

KENYA: Uchaguzi Mkuu unafanyika leo, Wapiga kura milioni 19 watachagua Rais, Wabunge, Maseneta, Magavana, Madiwani na Wawakilishi wa Wanawake.

Raia wa Kenya wataamua nani atakuwa Rais wao na Makamu wa Rais kwa miaka 5 ijayo.

Ushindani mkubwa sana uko kati ya vyama vya Jubilee na NASA na wagombea wake wa Urais, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Pamoja na kura ya urais pia watapiga kura ya kuchagua magavana wa Kaunti, wawakilishi wa kata(madiwani) na wawakilishi wa Seneti na Bunge.

Fuatilia hapa kupata updates za uchaguzi huu unaohusisha takribani wapiga kura milioni 20 waliojiandikisha.

Waliojiandikisha: Milioni 19
Vituo vya kupigia kura: 40,000
Idadi ya Wakenya: Milioni 48

WASIFU WA WAGOMBEA KWA UFUPI

Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) iliwaidhinisha wanasiasa wanane ambao watawania urais katika uchaguzi mkuu huu wa Agosti mwaka huu.
Walioidhinishwa ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee ambaye atakuwa anawania kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili, na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Bw Raila Odinga ambaye anawania urais kwa mara ya nne.

Bw Odinga, aliyehudumu kama waziri mkuu katika serikali ya muungano ya Rais Mwai Kibaki kati ya 2008 na 2013, anawania urais chini ya umoja wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA).

Katika uchaguzi huu wa tarehe 8 Agosti, kutakuwa na wagombea wanne pia ambao ni wagombea huru (hawana vyama).

Abduba Dida

Anawania urais kupitia chama cha Alliance for Real Change (ARK) na muungano wa Tunza Coalition.
Alikuwa mwalimu wa shule ya upili ya Lenana jijini Nairobi.
Hii ni mara yake ya pili kuwania urais baada ya mwaka 2013 ambapo alipata kura 52,848 na kumaliza wa tano.

Cyrus Jirongo

Ni mwanasiasa na mfanyabiashara ambaye ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Anawania kupitia chama cha United Democratic Party (UDP).

Alipata umaarufu kisiasa mwaka 1992 alipokuwa katika kundi la vijana wa chama cha KANU, Youth for KANU 1992 waliokuwa wakimfanyia kampeni Rais Daniel arap Moi wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka huo.

Ekuru Aukot

Anawania urais kupitia chama cha Thirdway Alliance Kenya (TAK), na ni mara yake ya kwanza kuwania urais. Alihudumu kama katibu katika Kamati ya Wataalamu waliosaidia kutunga Katiba Mpya ya Kenya ambayo iliidhinishwa na kuanza kutekelezwa mwaka 2010. Asili yake ni Kapedo, Turkana kaskazini magharibi mwa Kenya na amejitangaza kama mtu anayeleta mwamko mpya katika uongozi nchini Kenya. Amekuwa pia akitetea makabila madogo.

Japhet Kaluyu

Ni mgombea huru ambaye amerejea nchini Kenya hivi majuzi kutoka Marekani. Amejieleza kama mwalimu, mshauri na mwandishi ambaye ana uzoefu wa kufanya kazi Wall Street. Anasema amebobea katika utafiti katika sekta ya afya na msomi. Ni mara yake ya kwanza kuwania urais.

Joseph Nyagah

Ni mwanasiasa wa muda mrefu nchini Kenya ambaye alihudumu kama waziri wa vyama vya ushirika chini ya Rais Mwai Kibaki, na baadaye akawa mshauri wa Rais Kenyatta. Babake, Jeremiah Nyagah, alikuwa waziri wakati wa utawala wa mwanzilishi wa taifa la Kenya Jomo Kenyatta.

Bw Nyagah, ambaye alikuwahi kuwakilisha Kenya katika Umoja wa Ulaya, alihudumu kama mbunge wa eneo la Gachoka, Kaunti ya Embu mashariki mwa Kenya kabla ya kuteuliwa waziri. Anasema ndiye pekee anayeweza kutatua matatizo yanayoikumba Kenya, kutokana na uzoefu wake katika uongozi.

Akihojiwa na runinga ya NTV baada ya kuidhinishwa, alidokeza kwamba aliacha kazi yake ya kuwa mshauri wa rais baada ya kugundua kwamba ushauri aliokuwa anaoutoa haukuwa unafuatwa.

Prof Michael Wainaina

Yeye ni mgombea huru ambaye amekuwa mhadhiri wa fasihi katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Amekuwa mkosoaji mkuu wa mfumo wa sasa wa kisiasa Kenya na pia mchanganuzi wa siasa. Anasema aliamua kuwa mgombea huru kwa sababu vyama haviwapi nafasi vijana na wanawake.

Raila Odinga

Ni kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ambaye anawania chini ya muungano wa vyama vya upinzani kwa jina National Super Alliance (NASA). Aliwahi kuhudumu kama waziri mkuu wa kwanza wa Kenya, wadhifa ulioundwa kufuatia Mkataba wa Kitaifa ulioafikiwa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008, ambapo aligawana mamlaka na Rais Mwai Kibaki.

Ni mara yake ya nne kuwania urais Kenya. Mwaka 2013, akiwa bado na mgombea wake wa sasa Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka, alishindwa na Rais Uhuru Kenyatta. Alipinga matokeo hayo mahakamani lakini mahakama ikatupilia mbali kesi hiyo.

Uhuru Kenyatta

Anawania kwa muhula wa pili kupitia chama cha Jubilee Party ambacho asili yake ni muungano wa Jubilee wa vyama vya TNA na URP alioutumia kushinda urais mwaka 2013. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ni mwanawe mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta. Mgombea wake mwenza ni Bw William Ruto kutoka eneo la Bonde la Ufa la Kenya. Wawili hao wanawaomba wapiga kura kuwachagua tena kuendeleza maendeleo ambayo wanaamini serikali yao imetekeleza katika kipindi cha miaka minne ambayo wamekuwa madarakani.

Bw Kenyatta aliwania urais mara ya kwanza 2002 dhidi ya Mwai Kibaki kupitia chama kilichokuwa kinatawala wakati huo, chama cha KANU cha Rais Moi aliyekuwa anaondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 24. Alishindwa na akawa kiongozi wa upinzani na kwa pamoja na Bw Odinga wakafaulu kupinga Katiba Mpya iliyopendekezwa mwaka 2005. Mwaka 2007, alimuunga mkono Rais Kibaki uchaguzini.

========

UPDATES:

View attachment 560756
Vijana wa Kaunti ya Kisumu wakiwa kwenye mstari wakisubiri kupiga kura.

View attachment 560757
Kaunti ya Siaya nao hawajataka kuwa nyuma.

d8a791dd363227292d5e7e5d0038f123.jpg

Man on a life support machine casts his vote at Dandora Primary School

LIVE TEXT FEED:

08:50am updates

> Rais Uhuru Kenyatta amewataka wakenya wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wanaowapenda

> NASA wameamua kufuta kauli yao dhidi ya KDF baada ya kuhakikishiwa kuwa kila kitu kitaenda kwa mujibu wa taratibu na sheria

> Waangalizi wa EU wameridhika na mwenendo unaoonekana hadi sasa

> Wakenya wengi wamekiri kuwepo kwa propaganda kwa njia ya mitandao ya kijamii na hivyo kuwachanganya wengi

09:50am updates

df39ac57afe4eb0c080a6da1047863ce.jpg

> Takribani Wafungwa 167 wameruhusiwa kupiga kura na hata wanahabari wameruhusiwa kuhojiana nao kupata maoni yao juu ya uchaguzi huu (picha inajieleza)

> Tume ya Uchaguzi(IEBC) imekanusha kukwama kwa zoezi la Uchaguzi huko Kisumu. Wamesema kila kituo kuna vifaa vya akiba

> Gavana Wycliffe Oparanya amepiga kura katika Shule ya Msingi ya Mabole, Butere. Amewataka Wakenya kufanya uamuzi wa busara

11:30am updates:

> Waziri wa Kilimo katika Kaunti ya Meru, Genaro Gatangugi na Mbae Kiugo wameshambuliwa na wananchi baada ya kufumaniwa wakinunua vitambulisho eneo la Imenti Kusini

12:00pm updates:

> Mgombea Urais, Raila Odinga(NASA) anaelekea kupiga Kura katika kituo cha shule ya msingi Kibera

> Mgombea Urais kwa tiketi ya Jubilee, Uhuru Kenyatta amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Mutomo, Gatundu Kusini

> Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 64, Patrick Wame amezirai na kufariki dunia baada ya kupiga kura ktk kituo cha Lela, Nyando.

> Maafisa wawili wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujaribu kubadili majina ya makarani wa vituo. Maafisa hao walitaka kuwaweka Makarani wanaowataka wao kinyume na utaratibu. Tukio limetokea Kandara, Murang'a.

> Watu 24 wamejeruhiwa katika kituo cha Shule ya Msingi Moi Avenue baada ya kukanyagana wakati wakisubiri kupiga kura.

======
3: 00 PM UPDATES


> Mwanamke mmoja amejifungua Mtoto wa Kike katika kituo cha kupigia kura kilichopo Pokot Kaskazini. Mtoto huyo amepewa jina la Chepkura kwasababu amezaliwa siku ya uchaguzi.

> Mawakala watatu wa Jubilee wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuendesha zoezi la kuhesabu kura ktk Kituo cha Heshima Shule ya Msingi.

> Gari moja lenye namba za usajiri bandia za KBY 840C likiwa katika msafara unaolindwa limekamatwa na Maafisa wa Jeshi la Polisi na kukutwa na karatasi za kura ziliwe zimewekewa alama kwa Wagombea wa Jubilee. Limekamatwa huko traveling under escort found carrying (KIEMS) Mandera, Banissa.

>
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chebukati atoa taarifa fupi ya namna Uchaguzi unavyoendelea nchini humo.
  • Wafula Chebukati akiongea na Waandishi wa habari asema zoezi la Uchaguzi linaendelea vyema kwa maeneo mengi nchini humo.
  • Zoezi la kupiga kura linaendelea vyema Magerezani, kwa yale maeneo yaliyochelewa kuanza kupiga kura wataongezewa muda.
  • Chebukati: Vituo vitatu vilivyopo Laikipia vilipata changamoto za kiusalama lakini changamoto hizo zimetatuliwa na zoezi la kupiga kura linaendelea.

=====

4: 00 PM UPDATES

> Rais mstaafu wa Kenya, Mwai Kibaki, amekwama kupiga kura baada ya kukosa jina lake kwenye orodha ya majina ya wapiga kura iliyotolewa na Tume

> Katika vituo vipatavyo 40,883 vya kupigia kura, vituo sita vilikuwa na mpiga kura mmoja aliyeandikishwa.

> Raia wa kenya 4,300 walijiandikisha katika nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Afrka Kusini. Wamepiga kura katika nchi hizo.


5:34 PM
> Hatimaye Rais Mstaafu, Mwai Kibaki afanikiwa kupiga kura ikiwa ni dakika 34 baada ya muda wa kupiga kura kuisha.

> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Wafula Chekibukati amesema vituo 300 vimeongezewa muda wa kupiga kura kutokana na changamoto mbalimbali.

Ametoa mfano wa baadhi ya vituo hivyo na changamoto zilizojitokeza;
  • Huko katika Kaunti ya Turkana vituo 18 havikufunguliwa kwa wakati kutokana na kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia usiku wa kuamkia leo.
  • Jimbo la Ndia ambalo linavituo vya kupigia kura vipatavyo 70 ambavyo vilikumbwa na changamoto ya kuishiwa na karatasi za kupigia kura. Pia Vituo vya Nakuru Mashariki(Eneo lenye vituo 185) vilikumbwa na changamoto hiyo.
01:30am UPDATE:

Viongozi wa NASA wayakataa matokeo yote yaliyokwishatangazwa na IEBC kwa madai kuna faulo zinachezwa kwani fomu nambari 34A haijatumika kama sheria inavyoelekeza.



======

9th August, 2017

UPDATES 12:00 PM


> Kiongozi muandamizi wa NASA, Kalonzo Musyoka amewataka Wakenya kuwa watulivu. Wanaendelea kufuatilia malalamiko ya udukuzi.

> Askari Polisi wamewatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa Raila Odinga waliokuwa wameanza kuandamana.

1: 30 PM
> Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
  • Wanaharakati wameungana na Raila Odinga kuyakataa matokeo ya Uchaguzi. Wameituhumu IEBC kumpendelea Uhuru Kenyatta.
  • Chini ya Kempeni ya 'Kura Yangu Sauti Yangu' wamesema matokeo yamekiuka Katiba kwani hayajaambatanishwa na Fomu 34A.
  • Kiongozi wa Wanaharakati hao, amedai Sheria inaitaka Tume ya Uchaguzi kutoa Fomu namba 34A lakini hawajafanya hivyo.
  • Kundi hilo limeenda mbali na kudai Tume ya Uchaguzi(IEBC) imepunguza kura za Raila Odinga na kumuongezea Uhuru Kenyatta.
  • Mfano matokeo ya Uchaguzi ktk vituo vya Dagoretti, Langata, Nandi, Kisumu na Kepchebor yametofautiana na nakala za Fomu.
2:40 PM
> Mtu mmoja amefariki kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa nje ya kituo cha kujumlishia kura cha Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nduru kilichopo Kusini mwa Jimbo la Mugirango.
  • Mmmoja wa mashuhuda bwana Evans Okemwa amesema Mwanaume huyo amepigwa risasi mgongoni huku akilalamika kuwa hakukuwa na sababu ya msingi ya Askari huyo kufanya unyama huo.
  • Kamanda wa Polisi wa Kisii, Abdi Hassan amesema kuwa Askari huyo aliyefanya tukio hilo tayari amewekwa rumande kwa hatua zaidi za kisheria.
  • Shuhuda mwingine Bi. Evelyn Nyaboke amesema alimuona marehemu akijaribu kuwaamua wenzie wawili waliokuwa wakipigana lakini chakushangaza ni kwamba Askari huyo ambaye alikuwa mbali na tukio hilo alifyatua bomu la machozi kisha kumpiga risasi kijana huyo.
3:15 PM
> KENYA: Tume ya Uchaguzi(IEBC) imetangaza kuyafuta matokeo ya Uchaguzi ktk kituo cha Enenkeshui Jimbo la Kilgoris.
  • Akitangaza hatua hiyo Afisa wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Elijah Ombogo amesema kuwa wamebaini idadi ya walioandikishwa ni 285 lakini kura zilizopigwa siku ya uchaguzi(Jana) ni 325.
> Mgombea binafsi wa Kiti cha Urais, Japhet Kavinga amekubali kushindwa katika kinyang'anyiro hicho. Amesema si rahisi kutoka kura 10,000 alizonazo hadi kura 9,000,000.
  • Ameahidi kumuunga mkono mgombea yeyote atayeibuka mshindi pia ameahidi kumpatia ushirikiano.
> Viongozi wa Dini wameitisha mkutano na Waandishi wa Habari huko Bomas ili kuongelea mwenendo wa matokeo ya Uchaguzi.

  • Tutafanya mazungumzo na Wanasiasa, pia tutahusishwa katika kujumlisha kura mwisho tutatoa mtazamo wetu.
  • Tunawaomba Wananchi wawe watulivu na sisi tutatoa mtazamo wetu utakao kuwa huru kabisa.
4:00 PM
> MACHAKOS: Mgombea wa nafasi ya Ugavana, Bi. Wavinya Ndeti ameyakataa matokeo ya awali yanayoonesha mpianzani wake bwana Alfred Mutua anaongoza. Amelalamika na kudai ameibiwa kura.

> Makamu Mwenyeiti wa Tume ya Uchaguzi(IEBC), Consolata Nkatha ametangaza kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura za Urais kupitia Fomu namba 34A.

> NAIROBI: Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya waandamaji kuwashambulia Askari wa Jeshi la Polisi katika mitaa ya Mathare.

======
10th August, 2017 UPDATES
8:00 AM

> KENYA: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu, John Mwirigi(24) ashinda Ubunge Jimbo la Igembe Kusini. Hakuchapisha karatasi za kujinadi kutokana na kukosa fedha.
  • Kijana huyo ambaye ni yatima aligombea kama mgombe binafsi na kumshinda mgombea kutoka chama cha Jubilee.
  • Mwirigi amepata jumla ya kura 18,659 ambazo ni sawa na asilimia 39.09 ya kura zote huku mpinzani wake Joseph Miriti Mwereria amepata 15,635 sawa na asilimia 32.76.
  • Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 wananchi wa Meru walimchagua bwana Boniface Kinoti Gatobu kuwa Mbunge akiwa na umri wa miaka 26 na kuliwakilisha jimbo la Buuri.
10:15 PM
> Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) wameipongeza Tume ya Uchaguzi nchini Kenya(IEBC) kwa kuendesha uchaguzi huru na haki.
  • Utaratibu wa kupiga kura uliendeshwa kwa haraka kitendo kilichowapa Raia wengi fursa ya kushiriki kupiga kura. Vituo vilifunguliwa kwa wakati.
  • Wananchi wamepiga kura kwa amani na tunawapongeza Maafisa wa Tume ya Uchaguzi(IEBC) kwa kufanya kazi kwa Ueledi.
  • Tumefanya uangalizi katika jumla ya vitu 289 na tumeshuhudia hali ya utulivu.
  • Vyombo vya Habari vya hapa Kenya vimetoa taarifa kwa Ueledi na kufanya kazi kubwa sana.
  • Tunawaomba walioshindwa kuyakubali matokea au kufuata taratibu za kisheria katika kutatua malalamiko na changamoto zilizojitokeza.
> Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika(AU) kupitia Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki wamesema Uchaguzi ulikuwa huru na haki na Uchaguzi umekidhi viwango vya kimataifa.
  • Thambo Mbeki: Sisi ni waangalizi na si Wachunguzi tumekutana na NASA wametupa taarifa ya udukuzi ktk mfumo wa matokeo wa IEBC.
  • Thambo Mbeki: Lakini tunawaomba NASA na Jubilee waipe muda Tume ya Uchaguzi(IEBC) kukamilisha kujumlisha matokeo yote.
> Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola(Common Wealth): Waliojitokeza kupiga kura ni wengi na walikuwa huru. Tume ya Uchaguzi inapaswa kupongezwa.

> Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Jumuiya ya Ulaya wazitaja kasoro kadhaa zilizojitokeza ikiwepo vitisho kwa wagombea Wanawake.
  • Marietje Schaake(EU): Kulikuwa na muda mchache wa kufanya maandalizi ya Uchaguzi kutokana na changamoto za kisheria.
  • Marietje Schaake(EU): Tume imeonesha nia thabiti ya kuendesha uchaguzi kwa uwazi kwa kuweka fomu za matokeo mtandaoni.
  • Marietje Schaake(EU): Wakati wa kampeni matusi na lugha za chuki na zile zenye utata zilitamalaki kwa Wagombea na wafuasi.
  • Marietje Schaake(EU): Tumebaini kuwepo kwa kutokuaminiana na kutoamini Mamlaka za Uchaguzi. Pia tunalaani kifo cha Msando.
  • Marietje Schaake(EU): Tunasisitiza uchunguzi juu ya mateso na kifo chake vifanyike.
  • Marietje Schaake(EU): Kuna matatizo ya Usalama na kutokuwepo kwa kumbukumbu za kutosha za kuwatambua wapiga kura.
  • Marietje Schaake(EU): Baada ya Uchaguzi huu uliokuwa na ushindani Viongozi wanapaswa kuwarudisha Wananchi kuwa kitu kimoja.
  • Marietje Schaake(EU): Demokrasia ni zaidi ya Mtu mmoja kura moja.
2: 30 PM
> LUHAMBI: Jeshi la Polisi linamsaka Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi aliyetokomea bila ya kukabidhi masanduku ya kura.

> Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (IEBC), Wafula Chebukati asema walipendekeza Watu wapakue Fomu 34A kutoka katika tovuti.
  • Wafula Chebukati: Kutoka siku ya jana hadi leo Fomu 34A zipatazo laki tatu(300,000) zimepakuliwa.
  • Wafula Chebukati: Tumepokea Fomu 29,000 za 34A na 117 za 34B kutoka maeneo mbalimbali. Tumezipokea pongezi za Waangalizi.
  • Wafula Chebukati: Kulikuwa na majaribio ya Kudukua mfumo wa matokeo lakini majaribio hayo hayakufanikiwa.
  • Tume ya Uchaguzi(IEBC) imesema kuwa matokeo ya Mshindi wa kiti cha Urais yatatangazwa siku ya kesho(Ijumaa) jioni.
  • Tume itakamilisha zoezi la kuhesabu kura za majimbo yote 290 ifikapo kesho. Mpaka sasa bado vituo 1,032 havijawasilisha matokeo.
4:30 PM
> Mmoja ya Viongozi wa Muungano wa Upinzani(NASA) Musalia Mudavadi: asema wameiandikia barua ya malalamiko Tume ya Uchaguzi.
  • Musalia Mudavidi : Tunaitaka Tume ya Uchaguzi(IEBC) iwatangaze Raila Odinga na Kalonzo Musyoka kuwa washindi katika uchaguzi.
  • Musalia Mudavadi: Tunataka Raila Odinga atangazwe kuwa mshindi na Kalonzo Musyoka kuwa Makamu wa Rais.
  • NASA, tunauhakika kutoka katika chanzo chetu cha uhakika Raila Odinga amepata kura Milioni 8.4 na Uhuru Kenyatta kura Milioni 7.75.



FUATILIA HAPA MATOKEO YA UCHAGUZI

RESULTS

Mbona Raila kajitangaza???

Na anawezaje ku access server za tume ya uchaguzi?
 
Mkuu nchi iko salama katika nyanja zote;
  • Mavuno ni ya kutosha kwa mazao ya chakula, hakuna mtanzania atakufa njaa taarifa za jana toka statistical bureau zina sema mfumuko wa bei umeshuka wa Tanzania ni bora kabisa kwa ktk ukanda wa EAC. uko 5% as compared to KENYA 7% rwanda 6% etc etc
  • Ukiongea na wachumi wabobezi watakuambia serikali huwa inatumia pesa zake katika nyanja hizi; matumizi mengi yanapofanywa kwenye recurrent mzunguko wa pesa huongezeka na maisha kuwa rais, rejea awamu ya nne. Kwa upande mwingine serikali inapoamua kutumia zaidi ktk capital expenditure, maana yake ni serikali kuwekeza katika miundo mbinu, kama reli, barabara, bomba la mafuta ghafi HOIMA-CHONGOLEANI, Hudma za afya kama ujenzi wa zahanati, umwagiliaji kwa kujenga irrigation schemes, miundo mbinu ya umeme kama REA, ujenzi wa viwanja vya ndege na mengine mengi. HAPA WACHUMI WETU HAWAELIMISHI WANANCHI KWAMBA SERIKALI YA WAWAMU YA TANO IMEAMUA KUWEKEZA KWA KUFANYA CAPITAL EXPENDITURE KWA MAANA HIYO UWEKEZAJI HUU UNA TABIA YA KUPUNGUZA PURCHASING POWER LAKINI KUNA LONG TERM BENEFITS PALE MIUNDO MBINU HII ITAKAPOANZA KUTOA MATUNDA. IT IS LONG TERM INVESTMENT. NI SAWA NYUMBANI KWAKO UKIZOEA KUPOKEA MSHAHARA NA KUTUMIA KWA CHAKULA, NGUO NA VIPODOZI, SIKU UKIAMUA KUANZA UJENZI WA NYUMBA WATOTO WATAKOSA MAYAI NA JUICE PIA MAMA VIPODOZI HATAVIONA NA KUMBUKA UJENZI NI KATI YA MIAKA 3 HADI TANO SO TEGEMEA UKATA KWA KIPINDI HICHO. THE SAME NA JPM TUTAMCHUKIA LAKINI BAADA YA MIAKA KUANZIA TANO NA KUENDELEA TUTASHUHUDIA TAMBARARE
  • Ulinzi wa mipaka na mali za wananchi.
Huna unalojua, hivi hali ikiendelea kuwa mbaya kwa wananchi hiyo kodi italipwaje? Huwezi kulaza familia njaa ili ujenge kama ingelikuwa hivyo kila mtu angelikuwa na nyumba, unajenga ukiwa na uwezo wa kujenga. Mapato ya serikali yanapatikana kutokana na wananchi yaani kulipa kodi sasa kama watu wanafunga biashara hiyo pesa za kujenga hayo mabarabarani zitatoka wapi? Tumia akili ndugu.
 
Chekubeti naye anavizia kutangaza usiku nini kama yule wa mwaka 2007?
Chekubeti kazi anayo kwwa kweli.
 
there is no way out except for the loser to concede the defeat! Hiyo ndio itakuwa salama kwa wakenya wote! na pia huo ndio ukomavu wa kisiasa!
 
Let's respect our own institution, IEBC ndio chombo pekee kimepewa dhamana ya kutangaza matokeo sio vinginevyo,
 
Ikiwa Jubilee wali hack kunauwezekano na. Nasa nao wali hack ili kuona kama jubilee wame hack
 
Katika hali isiyo ya kawaida NASA wameitaka tume ya uchaguzi kumtangaza Odinga kuwa mshindi wa uchaguzi 2017 (BBC).

Huko Kisumu wananchi wako mabarabarani wakisherekea ushindi huo licha ya mvua kubwa inayonyesha!

My take: Kuna kila dalili za mapigano ya wao kwa wao kutokea endapo Odinga atatangazwa mshindi kwa kuwa tayari wananchi wakiaminishwa kuwa Kenyatta ameshinda!
 
Mleta mada utakuwa we ndo Bashite wa NASA, yaani hata jina la kinara wenu Raila huwezi liandika! Eti Laila, ndo maana tuliwanyima kura zetu!
 
Back
Top Bottom