EXCLUSIVE UPDATES: Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, 2017

Tuwaachie majirani zetu wachague viongozi wanaowataka yoyote atakaye chaguliwa tuungane nae kuendeleza umoja wetu!!

sisi kama watz tuishie tu kupongeza hata kama hatukubaliane naye!
 
Nawapongeza azam kwa kutuletea live habari za uchaguzi kenya.

Lakini nmesikitishwa na kitendo cha mtangazaj wao mmoja ivony kama sijakosea jina kuvaa socks za miguuni mkononi. Halafu akaamua kutoboa sehemu ya kutolea vidole gumba...

Ina maana hawajamuona kuwa amefanya kitu cha kipuuzi?kwa nini avae socks ? Kama ni baridi ingawa nmeshangaa watu wengi wamevaa kawaida. Basi kwa nini hakununua socks maalum kuliko kuvaa kituko kama hicho? Azam ina maana mmeshindwa kumwambia upuuzi huo?lazima ajue hiyo siyo comedy
 
Hii mpya mkuu em tupia hiyo picha tafadhali ...
 
Huyo pengine atakuwa na tatizo la kiafya la kuathiriwa na baridi hivyo tusimlaumu sana
 
Only Tanzania ambapo watu wanaangalia jambo kwa negative side. Kwa taarifa ivona kamuntu ndiyo best presenter wa kike kwa uwasilishaji habari.
 
Naona Uhuru na Odinga ndio wanaenda kupiga kupiga kura misafara yao ya magari ipo live citizen tv
 
Hakika kila kona ya nchi hii habari zinazobamba ni kutoka nchi jirani ya Kenya, mbali na hii mitandao ya kijamii Twitter, jf &group za whatsap zote habari kuu ni uchaguzi kenya

Hivi watanzania hatuna ya kwetu ya kuyashadadia hadi tuyashikie bango siasa za kenya?
Apite Uhuru au Raila, sie twafaidika nini?

Hebu tuwache unafiki watanzania, leo ni nane nane na kitaifa inafanyika lindi huko kwanini tusilijadili kwa upana hata hili maana linagusa wengi wa watanzania wakulima

Au ndio kusema kenya ni taifa kubwa kulikoa Tz
 
Only Tanzania ambapo watu wanaangalia jambo kwa negative side. Kwa taarifa ivona kamuntu ndiyo best presenter wa kike kwa uwasilishaji habari.
Watanzania tunapenda kufuatialia mapungufu ya kijinga tunaacha maswala ya msingi.

Ivona ni mtangazaji wa kimataifa.
 
Kila la kheri wakenya katika uchaguzi wenu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…