Ezekiah Wenje ahudhuria mkutano wa kamati kuu CHADEMA

Ezekiah Wenje ahudhuria mkutano wa kamati kuu CHADEMA

"Usijitenge nao,Wewe rudi jiunge nao tupate kujua yanayojiri".Bado Wenje sio wakuaminika,Sio sasa tangu awali Wenje sio wakuaminika.
 
Hizi ndizo ajenda muhimu mnazotaka CHADEMA izipe kipaumbele wakati huu, ili wafadhili wenu Oktoba wasitokwe jasho!
Hili suala linapigiwa debe na mashabiki wa Lissu. Kwa vile mliwaaminisha kuwa Mbowe ni fisadi, aliyepokea rushwa kutoka kwa Abduli basi ni haki akichukuliwa hatua. Hiki kigugumizi mnakitoa wapi?

Amandla...
 
"Usijitenge nao,Wewe rudi jiunge nao tupate kujua yanayojiri".Bado Wenje sio wakuaminika,Sio sasa tangu awali Wenje sio wakuaminika.
Hamna hata hoja moja ya Wenje iliyothibitishwa kuwa ilikuwa uongo. Kuanzia kuwa alienda na Abduli kwa Lissu kwa lengo la kumsaidia alipwe pesa anazodai. Lissu alithibisha hili katika mahojiano kuwa ni kweli alimuambia Abduli kuwa akifanikisha alipwe madai yake atakuwa rafiki yake wa maisha. Alisema kuwa Lissu alimsingizia Mbowe kuwa alihongwa gari. Kwa vile hamna aliyekanusha basi inaelekea kuna ukweli. Alisema kuwa palikuwa na mpango wa muda mrefu wa kumtoa Mbowe katika uongozi, hamna aliyeweza kuthibitisha kuwa alikuwa anasema uongo. Lema alijaribu kuelezea lakini ndio alizodi kuharibu!

Amandla...
 
Hili suala linapigiwa debe na mashabiki wa Lissu. Kwa vile mliwaaminisha kuwa Mbowe ni fisadi, aliyepokea rushwa kutoka kwa Abduli basi ni haki akichukuliwa hatua. Hiki kigugumizi mnakitoa wapi?

Amandla...
Nimekwisha kueleza ninapo simamia mimi; na kama hutaki kunielewa na kushikilia unayotaka wewe hilo halinisumbui; lakini ni dalili za kukosa hoja kwa upande wako.

Mimi sijui kama Mbowe alipokea kitu toka kwa Abdul, ila sina shaka yoyote na Mbowe kuwa karibu zaidi na Samia kwa sababu yoyote wanayoijuwa wao.
Kwa mtu kama wewe, ni wazi kuwa mnasubiri msuguano mkali ndani ya CHADEMA, ndiyo sabau ya kuhimiza jambo la namna hii lipewe kipaumbele ndani ya chama wakati huu.
 
Hakuna haja ya kubebelea vinyongo hadi Oktoba 2025. Usifikiri kumshinda Wenje na Mbowe ndio kuishinda CCM
Ishu nimkuwa yeye Wenje ndiye bado amekunja hadi leo kuna maneno machafu anaendelea kuongea mbona wenzake kina Boniyai wamekubali matokeo na wanatoa ushirikiano?Usitete jambo usilolijua.
 
Huyo katumwa na hao maboss wake aendelee kufanya surveillance ndani ya vikao vya CDM, Ni lini na wapi uliona Malaya akaacha au akastaafu kazi yake pendwa?
Kwq mfano huo umevuka mipaka nje ya mada sasa hiyo.
Malaya hastaafu nani kakwambiaaa?
Kuna kustaafu kwa hiari na kustaafu kwa lazima utambue!
 
Huyo katumwa na hao maboss wake aendelee kufanya surveillance ndani ya vikao vya CDM, Ni lini na wapi uliona Malaya akaacha au akastaafu kazi yake pendwa?
Acheni ujinga, walau muwe mnajifunza mifumo inavyofanya kazi. Hicho sio kikao cha maandalizi ya harusi, kwamba kila anayechangia hela anaweza kuhudhuria. Wenje ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, iweje useme amehudhuria kwa sababu ametumwa?
 
Sifurahishwi na lisu kufanya kaxi na mafisadi wapambe wa DJ hatuwezi kufika popote tukiwa na hawa timu mbowe..
 
Nimekwisha kueleza ninapo simamia mimi; na kama hutaki kunielewa na kushikilia unayotaka wewe hilo halinisumbui; lakini ni dalili za kukosa hoja kwa upande wako.

Mimi sijui kama Mbowe alipokea kitu toka kwa Abdul, ila sina shaka yoyote na Mbowe kuwa karibu zaidi na Samia kwa sababu yoyote wanayoijuwa wao.
Kwa mtu kama wewe, ni wazi kuwa mnasubiri msuguano mkali ndani ya CHADEMA, ndiyo sabau ya kuhimiza jambo la namna hii lipewe kipaumbele ndani ya chama wakati huu.
Mimi simo kichwani mwako kwa hiyo naenda na kile unachoandika humu. Kama vile wewe unavyotumia ninayoandika ( na nisiyoandika kunipinga).

Humu ndani yamejaa mabandiko kuhusu Mbowe kulamba asali na kupokea kitu kutoka kwa mama Abduli. Msimamo waku kuwa huna uhakika na tuhuma hizo zinaonyesha wazi uko upande gani.

Mbowe alikuwa ni Mwenyekiti wa Chadema na Samia ni Mwenyekiti wa CCM. Kwa nafasi hizo ni lazima ilibidi wawe na ukaribu wa angalau kuweza kuwasiliana. Hii hali ni pamoja na kuwa mmoja alimweka rumande mwenzake. Mbowe alionyesha ukomavu kwa kutokubali tukio hilo na mengine kumuondoa kwenye reli ya kutaka kuleta mabadiliko nchini.

Jambo unalonishutumu nalo linapigiwa debe na watu wa upande wako. Kutotaka lizungumzwe ni kwa sababu mnajua kuwa zile tuhuma zilikuwa ni za uongo na sehemu ya kampeni chafu iliyoendeshwa na walioshinda uchaguzi.

Mimi msimamo wangu ni kuwa kuna majeraha ambayo yalisababishwa na kampeni. Kujifanya hayapo ni kujidanganya. Mtu yeyote aliyeangalia sherehe za Bawacha atajua wazi kuwa wakina mama wengi wa Bawacha hawakufurahia alivyotendewa Mbowe. Ndio maana wakasisitiza kwa sauti kubwa jinsi wanavyothamini mchango wake kwa Chadema. Na kutia chumvi kwenye kidonda wakampa ngao yule ambae Mwenyekiti amesema hajachangia chochote Chadema.

Chadema haitasambaratika kwa sababu kuna watu wana mapenzi ya dhati na chama hicho na hawataruhusu hali hiyo itokee. Ndio maana unawaona wakina Boni Yai wakiweka tofauti zao pembeni na kushiriki katika kukijenga chama chao. Na hata kikisambaratika, wapo watu wa kutosha wenye uwezo wa kukijenga upya.

Watu kama wewe hali ikiwa mbaya mtakimbilia nyota nyingine inayong'aa.

Nimeifanya ndefu ili usiisome.

Amandla...
 
Mimi simo kichwani mwako kwa hiyo naenda na kile unachoandika humu. Kama vile wewe unavyotumia ninayoandika ( na nisiyoandika kunipinga).
Unarudi huko huko kwenye "magazeti". Sisomi!
Haya ya "kuwa vichwani" sijui hata niyajibu vipi!
 
Unarudi huko huko kwenye "magazeti". Sisomi!
Haya ya "kuwa vichwani" sijui hata niyajibu vipi!
Na ndio maana naandika gazeti kwa sababu wengi wenu ni wavivu wa kusoma na mnapenda mtafuniwe kila kitu. Hiyo ndio tragedy ya taifa letu ambalo linaamini uelewa unapatikana kwenye TikTok, X na Instagram. Na nzuri zaidi ikiwa na picha kuliko maandishi.
Hauna haja ya kunitaarifu kuwa haujasomq nilichoandika. Puuzia tu. Wako watakaosoma kama wewe hausomi. Au unataka vindication kutoka kwangu?

Kuandika gazeti namna hiyo maana yake hujui kujieleza kwa kutumia maneno machache.
Muda wa kusoma gazeti ambalo lingewasilishwa katika maandishi machache ni kupoteza muda na siyo kuwa mvivu wa kusoma.
Utasemaje "kutafuniwa kila kitu" wakati unaandika kwa mizunguko kueleza jambo jepesi tu!
 
Hii sio snapchat au X. Hakuna limit ya maneno. Sasa kama hauna muda wa kusoma text ndefu it's your loss. Nasema kuwa unataka utafuniwe kila kitu kwa sababu mara nyingi majibu na maswali yako haya make sense. Labda kwa sababu unataka brevity zaidi ya kila kitu unashindwa kujenga mazingira ya hoja yako. Ila yote hayo hayana umuhimu wowote maana umetangaza kuwa hautasoma magazeti yangu. kinacho nishangaza ni kwa nini unakazania kutaka niandike unavyotaka. Nishakwambia kuwa kama hauwezi kusoma ( ingawa najua unasoma ila unashindwa kula matapishi yako) yapuuzie na usiseme lolote. Naamini kuwa kuna wengi tu wenye mtazamo kama wako. Just do me a favour, usinijibu lolote.

Amandla...
 
Back
Top Bottom