Ezekiel Kamwaga: Hata kama tuna uchungu na bandari ndiyo tumfokee Rais?

Napenda Sana makala zako.... Lakini kwenye hili la bandari... Sikubaliani na wewe kabisa.....nadhani uko mbioni kupata uteuzi sio bure
 
Najiheshimu sana mkuu siwezi kuweka au kupost vitu vya hivyo. Labda,mfano hivi unawezeje kumuita Spika wa Bunge kua huyo ni mtoto..
Huyu Dk.Shala anafikiri yeye alijifunza mwenyewe au alifundishwa na watu?
Mtoto sio tusi, pia naamin hakuna tusi wala kejeli kwa Rais!! Hakuna ✔️
 
Huyu Kamwaga ni bure kabisa! Nilimdharau sana wakati alipokuwa anashabikia akihamasisha eti watu wasijadili kadhia ya USHOGA,kwa sababu in his opinion kuwa ni jambo dogo halina madhara kwa Taifa la kesho
 
Siamini kabisa katika fikra za Ezekiel. Kilichofanyika kina madhara. Kinahitaji marekebisho. Wanadamu siku zetu chini ya jua zinahesabika. Kwanini tuwaachie majanga watoto na wajukuu zetu kwenye maamuzi ambayo kusema kweli yamejaa excuses ambazo hazina mashiko
 
..tusipindishe pindishe.

..madudu yaliyoko kwenye mkataba wa Tanzania na Dubai ndio yaliyosababishwa watu wazungumze kwa lugha kali, au maneno magumu.

..Rais amepoteza heshima yake kwa kuonekana hajali na hana uchungu na rasilimali za nchi yetu.
Na haya yanawafanya wengi waone kama ni matendo ya Mama wa kambo. Linaweza kuja kudefine legacy yake. Maisha yetu yana kiasi. Ipo siuku tutakaa pembeni na kuanza kusimuliwa
 
Ndio laizima afyokewa kwani ni lazima awe raisi kama anaona anafokewa achie ngazi
 
Unapokuwa na Rais ambaye ni wa jinsia ya kike na kutumia maneno ya kumkosoa, kwa mfano, “badala ya kuchutama, yeye anachanua”, linatuma ujumbe ambao haukubaliki hata kwa mila na desturi zetu za Kiafrika
Huyu Rugemeleza ni mhuni na hana adabu, hawezi kumwambia mama yake maneno kama hayo, huyu anatakiwa atiwe adabu.🪓⛏️⚒️🗡🔫🔫🚑
 
Kugombana na mfumo unaoongoza nchi ni sawa na kupiga ngumi ukuta. Alikuwepo mwanaharakati mmoja miaka ya tisini mpaka elfu mbili alifanya shughuli ya kupeleka wanafunzi kule Ukraine masomoni.

Kwa asili alikuwa ni radical sana kila akiandika makala ni kuishambulia na kuikosoa serikali ya CCM ya kina Kikwete, Mkapa. Sasa hivi amekuwa sawa na mtu aliyechanganyikiwa, kila akimuona mtu anamtazama kwa uoga kana kwamba amekuja kumdhuru.

Kila anachokifanya anaona hakisogei, Namuona Nshala akiingia kwenye kundi hilo hilo la yule mwanaharakati. Mfumo unakupiga mpaka unaumia na humuoni nani aliyekupiga, Na hivi ni mwanasheria wanajua namna ya kumpoteza kuanzia huko huko mahakamani.
 
..tusipindishe pindishe.

..madudu yaliyoko kwenye mkataba wa Tanzania na Dubai ndio yaliyosababishwa watu wazungumze kwa lugha kali, au maneno magumu.

..Rais amepoteza heshima yake kwa kuonekana hajali na hana uchungu na rasilimali za nchi yetu.
Hakuna mkataba wa Tanzania na Dubai uliosainiwa, yapo makubaliano ya kutaka kufanyika biashara pale bandarini.

Upotoshaji ukiwa ndio utangulizi wenyewe hiyo habari nzima inapoteza heshima ya mwandishi.
 
Nidhamu ya CCM ipo pale pale licha ya mashambulizi machache kutoka juu kwa viongozi waandamizi.

Urais wa Samia ni imara sana tofauti na namna anavyoonekana na kuchukuliwa na wanaharakati haswa hawa wa humu jukwaani.
 
Andiko reeefu lakini limejaa mashudu tupu.
Dr Nshala kusema Bunge limefanya kitendo cha uhaini Kwa kupitisha mkataba unaofuja na kufifisha sovereignty ya Nchi yetu amelidharaulisha Bunge? Yaani wewe nyumbani kwako mnaingia urafiki na jirani yako kiasi kwamba ukitaka kuongeza chumba kwenye nyumba yako lazima uombe ruhusa yake lakini yeye akitaka hata kujenga mji mwingine Hana haja ya kukuuliza unaona ni Sawa?
Mwelevu akivuliwa nguo huchutama lakini mwelevu wetu yeye alipovuliwa nguo kasimama.
 
Huyo mwandishi lau angejua matamshi mazito yanatolewa na wananchi ambao hawasikiki kama huyo dr nshala na wengine asinge andika andiko hili.

Huku mtaani viongozi wa juu serikalini wanatukanwa matusi ambayo kamwe hawataweza kustahimili kuvumilia kusikia .

Hii ni kwa sababu ya kukatishwa tamaa na wale waliojiminisha kuwasadia wananchi kuvuka au kutoka kwenye umaskini.
 
Hakuna mkataba wa Tanzania na Dubai uliosainiwa, yapo makubaliano ya kutaka kufanyika biashara pale bandarini.

Upotoshaji ukiwa ndio utangulizi wenyewe hiyo habari nzima inapoteza heshima ya mwandishi.

..iwe ni mkataba au makubaliano lakini ni jambo linalotufunga KISHERIA.

..na limepelekwa BUNGENI maana yake lina nguvu ya kubadilisha SHERIA za nchi yetu.

..ndio maana unasikia serikali imeazimia kupelekwa mswada utakaobadilisha sheria za rasilimali na uwekezaji zilizotungwa mwaka 2017 na Prof.Kabudi na Rais Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…